Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Simbachawene ahamishiwa Utumishi na Utawala Bora, Jenista arejeshwa Sera, Bunge na Uratibu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Jenista Joakim Mhagama (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu). Mhe. Mhagama anachukua nafasi ya Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb). Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Amemteua Bw. George Boniface Simbachawene (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe. Simbachawene anachukua nafasi ya Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb). Kabla ya uteuzi huo Mhe. Simbachawene alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Aprili, 2023.

Mawaziri wateule wataapishwa tarehe 02 Aprili, 2023 saa 3 asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.

View attachment 2573265
Watanzania wenye sifa wameshaisha, itabidi tuendelee ku recycle haohao waliopo kwenye Uongozi
 
Kina kipindi hasahasa wakati jiwe yupo ulingoni alikuwa anafanya mabadiliko na kuhamisha mawaziri masikini walikuwa wanashangilia sana lakini kadri muda ulivyoenda hawakuwa na nafuu ya maisha zaidi ya kugundua walikuwa wanapigwa changa la macho. Samia naye anapita mulemule. Hv waziri aliyeshindwa wizara ya kilimo inamaana ataiweza wizara ya mifugo? Hv huyo Jenista hajawahi kuwa waziri wa bunge sera na uratibu na akahamishwa? Yaan sasahivi atakuwa na lipi jipya? Watanzania amkeni ukoo ni uleule wa panya
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Jenista Joakim Mhagama (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu). Mhe. Mhagama anachukua nafasi ya Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb). Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Amemteua Bw. George Boniface Simbachawene (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe. Simbachawene anachukua nafasi ya Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb). Kabla ya uteuzi huo Mhe. Simbachawene alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Aprili, 2023.

Mawaziri wateule wataapishwa tarehe 02 Aprili, 2023 saa 3 asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.

View attachment 2573265
Kwani hakuna wengine, au ndiyo ile we ukiharibu hapa tunakupeleka jimbo jipya. Ukiona tumekutoa kabisa juwa wew siyo mwenzetu.
 
Jenista Mhagama hafai kabisa hata kuwa mwenyekiti wa kijiji, ni muongo kuliko shetani, alafu chochote akisema, fuatilia ni muongo sana, ameharibu sana wizara ya Utumishi wa Umma, yeye na Ndumbaro kaka yake.

Jenista mafao ya watumishi kaumiza sana, Jenista anaweza kuahidi watumishi jambo fulani, kumbe anawadanganya, ni muongo sana, akisema atasaidia jambo mfano promotion etc ni muongo sana.. Mh. Rais angemuweka pembeni kabisa huyu.
 
Yaan hapa mimi ndio huwaga sielewagi kabisaaaaa yaaan hiinchi ngumu sana 🤔 sasa hapo kafanya nini😞 nchi Inawatu zaidi ya milioni 60 waziri kabolonga

Wewe unamuamisha wizara???!! Kisa tu ukimtimuwa ukaweka mzalendo mwingine na Uraisi wako unakomea hapahapa sio??! kama siiihivyo unaogopa nini

Au hii ndio changa la macho watu wasahau ripoti ya Cag?! Mimi tu nikuambie hata mjinga akida nganywa sana kunawakati unafika anakariri beti za huo wimbo na ukiona imefika huko jijuwe kabisa kinachofuata ni aibu yako
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Jenista Joakim Mhagama (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu). Mhe. Mhagama anachukua nafasi ya Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb). Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Amemteua Bw. George Boniface Simbachawene (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe. Simbachawene anachukua nafasi ya Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb). Kabla ya uteuzi huo Mhe. Simbachawene alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Aprili, 2023.

Mawaziri wateule wataapishwa tarehe 02 Aprili, 2023 saa 3 asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.

View attachment 2573265
Utumishi wangemrudisha Mchengerwa angalau kwa hii miaka miwili na nusu iliyobaki ashughulike na matatizo ya watumishi kwanza, alijitahidi sana mara ya kwanza alipopewa hii wizara.
 
Mi naona hakuna sababu ya kupewa viapo tena akifika aambiwe kiapo alichoapa aendelee nacho hii kila siku mtu anaapa tunamchosha Mungu bila sababu.
Hii imekaa poa sana
Kiapo cha mara ya kwanza mtu aendelee nacho 😄
 
Back
Top Bottom