Mafwele azuiwa kuingia Marekani. Ahusishwa na Utekaji, ukiukwaji wa haki za binadamu

Mafwele azuiwa kuingia Marekani. Ahusishwa na Utekaji, ukiukwaji wa haki za binadamu

Elewa ban ya Mafwele ni litmus paper tu reactants bado zinakuja.
nadhani pia itolewe elimu ya sheria ya kumiliki silaha(bastola) watu waelewe na wajue utaratibu wa kumiliki itasaidia pia, hizi ban za marekani ni upuuzi mtupu.
 
wanatakiwa wazuiwe wafanyabiashara na wanasiasa ndo linakuwa pigo sio kamanda wa polisi hana impact kwenye uchumi
Hata makamanda wa polisi wanafanya biashara ndani na nje ya nchi na wanamiliki makampuni makubwa tu ili wanafanya kwa kificho sana. Mfano mzuri ni babake meya fulani aliyekuwa rpc wa Dar siku hizi hatulii nchini kwani ana biashara zake dubai na china.
 
Haisaidii kitu kama wapo serious hiyo ban angepigwa kwanza head of the state na cream yake inayo fuata ya uongozi ingesaidia mnooo kupeleka ujumbe duniani kwamba viongozi hao ni Waharamia na pengine katika baadhi ya Nchi wangetengwa lakini ban kapigwa mafwele !!! Huko duniani ni nani anaye mjua mafwele period
Halafu marekani na tanzania bado zinafanya biashara zote muhimu. Sasa mafwele akipigwa ban inasaidia nini?
 
Hawana hofu wale , ili hofu iwepo inabidi mpaka top leader mmoja aliwe kichwa kinyume na hivyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu
Sijui kwanini hawa great thinkers wanashindwa kuelewa issue ndogo kama hiyo.
 
Kweli kabsa ya makonda ilikuwa ya tofauti na licha ya udogo wake magufuli alimwondoa kwenye mfumo wa uongozi wake
Magufuli hakumwondoa, alisema waziwazi kuhusu kutokuwa na tamaa na waliotaka kugombea walipewa options mbili, ubaki serikalini utumikie wananchi au uingie kwenye siasa uachane na utumishi wa umma. Makonda akachagua siasa ambapo aliangukia pua. So alijitengenezea mwenyewe mazingira ya kupigwa chini na mfumo.
 
Mkuu acha kuwa na kichwa kigumu, US katika lugha ya kidiplomasia hapo amesema serikali ya Tanzania inafuga majambazi , watekaji, wafiraji na wauaji, hio ndio maana yake.. hio ni picha mbaya tayari kwa serikali ya Tanzania duniani..

Makonda kuzuiwa kuingia US madhara yake huwezi kuyaona leo, lakini imeshamuharibia katika safari yake ya kisiasa.. kuwekwa kwenye list ya wahalifu na nchi kama US ni pigo.. kwanza kunabaadhi ya vyeo atabaki kuvisikia tokana na ban aliyonayo, mfano huwezi kuwa waziri wa mambo ya nje halafu una ban US..
Kwani lazima awe waziri wa mambo ya nje, na je unafahamu kwa sasa ni waziri wa maigizo na michezo?
 
Naomba kujuzwa athari ya hivi vikwazo vya kuzuiwa Kuingia Marekani. kwa mfano, mtu kazaliwa Tanzania,ni mtanzania ,kasomea na kukulia Tanzania na anafanya kazi hapa Tanzania kwa nafasi yoyote ile na hana mpango wala hana ndoto ya kwenda huko Marekani.Vikwazo hivi vina maana gani ? Mfano waziri Makonda alishawekewa hivi vikwazo kitambo, yupo hapa nchini na amekuwa akipata nafasi mbalmbali tena kubwakubwa tu, na ndiyo kwanza anazidi kunenepa.Sasa hivi vikwazo vya hawa Wamarekani ninini athari yake ?
Au Marekani inachukuliwa kama ndiyo lango pekee la kwanza katika safari ya binaadam kuelekea peponi ? kiasi kwamba ukizuiliwa kuingia Marekani basi hata hiyo pepo ya Mungu ndiyo basi huipati tena ?
 
Hao jamaa nao bado wapo zama za giza!!

Kabla ya hiyo ban huyo bwana alishawahi hata kufika huko Marekani?

Nyakueni hizo raia kama Maduro au msukume agenda ya kuwapeleka ICC.
 
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeweka vikwazo vya usafiri kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Faustine Jackson Mafwele.

Taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio imesema kuwa kutokana na taarifa za kuaminika, Mafwele alihusika katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

“Mwaka jana jeshi la polisi liliwakamata, kuwatesa na kuwalawiti raia wa Uganda, Agather Atuhaire na raia wa Kenya, Boniface Mwangi, waliokuwa Dar es Salaam kufuatilia kesi inayomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu,” ilisema taarifa ya Rubio.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mahmoud Thabit Kombo aliambia BBC kwamba serikali bado haijapokea taarifa rasmi kuhusu hatua hiyo, ambayo inamzuia Mafwele kuingia Marekani.

Source: BBC.

 
Ulitaka Marekani wafanye nini ili huyo mtiz apate faida!?
Na wewe umefanya nini Cha zaidi!?
1. Marekani kwa capacity yao wana uwezo wa kumpoteza Fau kwenye uso wa dunia. Ila kwa kuwa nao wana mambo meusi hawawezi kufanya hivyo.
2. Huwezi kunifananisha mimi nobody na maamuzi ya taifa la marekani.
 
Back
Top Bottom