Mahakamani 28 Septemba: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 10.

LISSU: Waheshimiwa Majaji, mashahidi wote wa Utetezi walizungumza siyo tu mambo yaliyotokea tarehe 23 Aprili 2025, vilevile walizungumza na matatizo wanayokutana nayo.

Walizungumza kutoka kwenye mioyo yao.

Waheshimiwa Majaji, viongozi hao waliokuja kutoa ushahidi wamezungumza kila mmoja wao namna alivyokamatwa na Jeshi la Polisi na wakati mwingine bila kushtakiwa.

Walizungumza juu ya mauaji ya viongozi na wanachama wao.

Waheshimiwa Majaji, viongozi wote waliotoa ushahidi wa Utetezi waliiambia Mahakama kile ambacho hakikuambiwa na mashahidi wa Mashitaka.

Nini hicho?

Ni mazingira gani maneno yale yalitamkwa? (Context to those words).

Waheshimiwa Majaji, walisema wana maslahi na kesi hii.

Mwenyekiti wao yupo ndani kwa kesi ya uongo.

Kitu kingine walisema wana maslahi na haki.

Hakuogopa watafungwa, wakaja kutoa ushahidi tofauti na wale wa kificho.

Maslahi yao ni kutendeka kwa haki.

Mateso ya Mwenyekiti wao yakome.

Waheshimiwa Majaji, kwenye kesi ya Goodluck Kiando vs Jamhuri, Criminal Appeal No. 118 of 2003, [2006] TZCA 428, Mahakama ya Rufani ilisema โ€” na haya maneno ni muhimu, Waheshimiwa Majaji:

Kila shahidi anastahili kuaminiwa na ushahidi wake kukubaliwa, isipokuwa tu kama kuna sababu nzuri, za maana na zinazoeleweka za kutomwamini shahidi huyo.

Swali langu, Waheshimiwa Majaji, kati ya mashahidi wa Utetezi na mashahidi wa Mashitaka โ€” hao waliofichwa, hao waalifu, hao mapolisi ambao ni waongo...

Ushahidi unaojichanganya...

Au Mahakama iamini ushahidi wa viongozi wa juu kabisa?

Mashahidi wote wa Upande wa Mashitaka hawastahili kuaminiwa hata mmoja, kwa sababu nzuri na za maana ambazo nimezionyesha kwenye ushahidi huu.

Wapo 17, Waheshimiwa Majaji.

Nataka kumuondoa PW17. Kwa kiasi kikubwa, ushahidi wake ni wa kweli. Wengine wote hawastahili kuaminiwa.

Ushahidi wote wa Utetezi unastahili kuaminiwa na kukubaliwa kwa sababu ambazo nimezizungumzia vilevile kwa kirefu.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Hii ni Recap ya Kibabe
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 11.

LISSU: Waheshimiwa Majaji, kwa kusema hayo sina maana โ€” naomba nisichukuliwe vibaya โ€” nina maana kwamba ushahidi wote wa Utetezi haukuwa na mawaa.

Sina maana hiyo.

Hakuna ushahidi unaotolewa kwenye Mahakama kubwa kiasi hiki usiwe na shida. Siyo katika dunia hii ya Mwenyezi Mungu.

Na ushahidi wa mashahidi wote wa Utetezi ni ushahidi wa binadamu.

Hata hivyo, Waheshimiwa Majaji, mashahidi wengi wa Utetezi, hata mimi binafsi, tuliburuzwa kwenye cross-examination.

Kuna shahidi aliulizwa, โ€œUna magari mangapi?โ€ Akasema mawili, akaletewa documents za magari manne.

On all fundamental issues, mashahidi wa Utetezi were completely unshaken.

Huko kwenye, โ€œUmenunua jezi ya Arsenal wapi?โ€, โ€œUna magari mangapi?โ€ na โ€œUmelala Dubai?โ€ โ€” sawa.

Ishu ni, yana maana gani kwenye kesi ya uhaini?

Kesi ya Nguza Vikings @ Babu Seya. Walisema nini?

Ilisema yafuatayo, ukurasa wa 25, Madam Justice Natalia Kimaro:

โ€œA conviction on a criminal case, itโ€™s never based on contradiction in defence case but ratherโ€ฆโ€

In other words, the burden of proof in criminal case lies on the Prosecution, not in the defence.

Hata kama mashahidi wa upande wa Utetezi wamegongana kiasi gani, kesi haamuliwi na madhaifu au migongano ya upande wa Utetezi.

Mikanganyiko, kama ipo, inaisaidia Mahakama kupima kama Upande wa Mashitaka umethibitisha kesi.

Waheshimiwa Majaji, nilisema huo msimamo wa Nguza Vikings upo katika:

  • Mohammed Haruna @ Mtupeni (Supra);
  • Kesi ya Vitalis Joseph (Supra);
  • Samweli Siranga vs Jamhuri, 1993 TLR 148;
  • Nyabohe Nyagwisi vs Jamhuri, Criminal Appeal No. 243 of 2020, Court of Appeal.

Waheshimiwa Majaji, nimemaliza kuzungumzia ushahidi.

Na ushahidi ambao nimezungumzia unaonyesha wazi:

Hakuna ushahidi wa ku-convict.

Hakuna ushahidi wa kumtia hatiani Mshtakiwa.

Badala yake, kuna ushahidi wa kutosha wa kumuachia huru Mshtakiwa.

Mshtakiwa hawezi kutiwa hatiani kama kuna eneo linalotia mashaka.

Mashaka makubwa na ya msingi, Waheshimiwa Majaji, ni jinsi ambavyo Upande wa Mashitaka umejaribu kuficha mambo muhimu kuhusu hiyo hotuba ya tarehe 23 Aprili 2025.

Kuna kila sababu ya kuonyesha kwamba, basically, kesi imetengenezwa kwa kuficha, kwa kuyaondoa maneno ambayo yangeonyesha wazi pasingekuwa na kesi.

Upande wa Mashitaka umefanya kazi ya kuyaondoa maneno na kuyaondoa katika Hati ya Mashitaka.

Kwa sababu hiyo, wamefanya hati isomeke kama vile kuna mambo makubwa yaliyokuwepo, kwa sababu ya maneno ya kuokota- okota.

Waheshimiwa Majaji, naomba niwarudishe katika Hati ya Mashitaka juu ya maneno ninayolalamikiwa.

Ukiangalia hati, unaona kuna maneno yameondolewa.

โ€œWanasema kitu kimoja sahihi hapa, msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli kwambaโ€ฆโ€

Mtu kama hana akili anaweza asijue shida ipo wapi.

Shida ni pale wanapoweka dots tatu pale mwanzo โ€” (ellipsis).

Kuna maneno ya kabla yameondolewa, na uthibitisho ni hizo dots tatu โ€” (ellipsis).

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Nakumbuka hii cross exam na kamanda George Bagyemu.

Sikujua kama ilikuwa na umuhimu kiasi hiki
 
Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa PW5: Mtakumbuka, ndiyo ushahidi wa yule aliyedanganya kuhusu dini yake.

Mahakamani amekula kiapo kama Mkristo, na katika maelezo yake ni Muislamu, Kielelezo D4, ukurasa wa 342 wa rekodi.
Kwa maoni yangu: PW5 nae ni shaidi wa mchongo.
Sijawai kuona mtu aneweza kuikana dini yake, yani hata uniamshe usingizini nitasema dini yangu ni fulani tu, hata iweje siwezi kujiingiza kwenye sehemu isiyo yangu. Huyu ni shaidi muongo
 
Kwanini unakua hivi?
Mbona kina Luka ni machawa
Ila sometimes wanatulia?

Unanishangaza sana๐Ÿ™Œ๐Ÿผ
na ustashangaa sana mpaka uelewa kwamba upo kwenye jukwaa la siasa na sio nyumba ya ibada ๐Ÿ’
 
Majaji wamenyimwa sababu ya kutotenda haki, alichokifanya Lissu ni kuwasaidia jinsi ya kuandika Hukumu ya Kesiโ€ฆkwa kifupi amefanya kazi ya Majaji, uamuzi ni wao kuendelea kuwa MAJAJI au kuanza kuitwa MAJAGI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ