Mahakamani 29 Septemba 2026: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Hatimaye heka heka za vizimba vya mahakama kwa mwaka mzima zimetamatika hii leo.

Kila mtu amesikia na ameona mwenendo mzima wa case toka mwanzo hadi sasa, kila kitu kiko wazi pasi na shaka, kila upande utapata haki na stahiki yake, pasipo upendeleo wowote.

Kwenu majaji, tunategemea usomi na weledi wenu ktk kupitia hii case kwa umakini na usahihi, pasipo kuingiliwa wala kuyumbishwa na yoyote wala chochote, tunategemea kuona hukumu iliyo ya haki na ukweli halisi.

Binafsi yangu, nitoe rai kwenu majaji, hii case imebeba hatma ya mustakabali wa muenendo na maisha ya mtu baada ya hukumu yenu, sio hivyo tu imebeba dhamana ya heshima na hekima kwenu majaji na taasii ya mahakama km muhimili huru na unaojitegemea, km katiba inavyosema wazi.

Hukumu yenu itaakisi kile kilicho/kinacho sikika kwa umma, kuwa mahakama ni ya simu, na ili kukanusha kwa umma kuwa maneno Yale sio sahihi na ilikua bahati mbaya, basi toeni hukumu ya haki na ukweli kulingana mlolongo mzima wa shauri, ushahidi na case nzima kwa ujumla, vinginevyo umma utaamini yale maneno ni ya kweli, itapelekea mahakama kupoteza uaminifu, heshima na hekima mbele ya umma.

Niwatakie kila la kheri ktk jukumu lenu hilo kubwa na nzito ktk kutoa hukumu juu ya case hii.
 

..hakuna anayesema Katuga hajaongea jambo lolote la maana.

..mtizamo wa wengi ni kwamba Katuga hajaonyesha kwamba kuna kosa serious na baya la UHAINI.

..mazingira hayo ndiyo yanayofanya Katuga ajichanganye kwa kumuita Lissu anayemtuhumu kwa uhaini " mwenzake."

..kwasababu hakuna kosa la uhaini ndio maana kauli za hukumu ya miaka sifuri zinatoka kinywani mwa Katuga, muendesha mashtaka.

..Vyovyote watakavyoamua Majaji, ni mtizamo wa wengi kwamba Lissu sio mhaini na anastahili kuwa huru.
 
haya,
asante
 
Maoni yangu kulingana na submission ya Katuga.

Katuga anasema mikanganyiko ya kauli za mashahidi wa jamuhuri ni minor issues ambazo haziendi kuathiri mzizi wa kesi.

Katiga ametoa references za mkanganyiko wa Heche kuhusu orodha ya magari anayomiliki ambapo sehemu moja alisema ana magari matano na sehemu nyingine alisema 3.

Kwanza ifahamike kwamba ishu za magari hazipo kwenye kesi ya msingi na wala sio maelezo ambayo yapo kwenye kielelezo cha shahidi ambacho kimeingizwa kwenye rekodi ya mahakama.

Pili Katuga swali la Katuga haliku hoji specific kuhusu idadi ya magari bali alihoji kuhusu idadi ya magari ya kifahari ambayo Heche anamiliki.

Tukija kwenye mikanganyiko ya mashahidi wa jamuhuri, swala la dini ni moja ya Identity ya shahidi.

Ndio maana kwenye hati ya maelezo ya shahidi maelezo hayo yapo, na mahakama imeyachukua na kuyarekodi kama kielelezo cha shahidi.

Na kama hiyo haitoshi bado akiwa kizimbani alikula kiapo cha dini, hii ina maana kwamba taarifa kuhusu dini ni za muhimu katika kupima authenticity ya shahidi.

Mkanganyiko wa dini unaweza kutoa majibu kuwa hayo maelezo aliyodai aliandika, hakuandika yeye bali ni mtu mwingine alichukua hilo jukumu bila consent ya muhusika.
 
Leo yenyewe hii hadi muda huu hakuna ponit yoyote aliyo ongea zaidi ya kuwa mtafsiri wa lugha, au mdadavuaji ktk kamusi.
Kwa kuwa akili za maCCM ni zaidi ya akili za panzi, wao wanaona ametema madini. Machizi hawajui kupembua pumba kutoka kwenye mchele.....wanabugia zote pamwe!
 
Asante sana Mkuu kwa ufafanuzi. Hata hivyo nimejiuliza swali la: akina nani wanapaswa kuwa na kiapo cha utii kwa serikali? Natafuta majibu hapa mtandaoni lakini majibu ninayopata yana nivuruga tu. Tusubiri 6 Novemba 2026 majaji watasemaje.

..nimefuatilia kesi yote.

..nimeridhika kwamba Tundu Lissu sio mhaini.
 
Vipi yule aliyesema ana magari mawili chini ya kiapo, wakati ana magari matano? Yeye hajatoa contradiction?
Hivi kweli huyu katuga hafahamu kuwa haya mambo ya magari yapo nje ya kesi ya msingi au anajitoa ufahamu? Sasa wingi wa magari ya Heche unathibitishaje uhaini wa Lissu?

Yule mpuuzi aliyebadili dini kwenye ushahidi hoja yake ipo kwenye uaminifu. Kwamba ikiwa mtu anaweza kuikana hata dini yake anawezaje kuepuka kusema uwongo mahakamani? Hii ndio pointi ya msingi. Pia, mtu alishajitambulisha kuwa ni mkristo lakini akaja kudai yeye ni muislamu na yupo kifichoni, mahakama itaaminije kuwa shahidi hajabadilishwa na kuleta shahidi mwingine? Hii sio contradiction kama anavyotaka kutuaminisha katuga.

Na humu pia tuna makatuga wa kutosha ambao hawaelewi kitu wanapayuka tu kama wapo kwenye kijiwe cha kahawa. Unajua kwenye kibiwe cha kahawa ukiwa na sauti kubwa unaongea hadi unawafunika wote, utaonekana wewe ndiye unayejua kila kitu. Mahakamani hakuko hivyo. Tundu Lissu anatema madini kwa upole lakini katuga anapayuka tu. Ingekuwa mahakama ni kijiwe cha kahawa, hasi katuga angeshinda kesi hii misa ya kwanza tu.
 
Neno Serikali linapatikana katika Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kuanzia ibara ya 33 hadi 59.
 
Take note kwamba PW5 aliposema kuhusu dini mbili tofauti katuga anasema ni jambo dogo.

Kisha turudi hapa.
Katuga anasema Sheria hajipeleki kushughurikia mambo madogo kisha baadae anasema swala la dini ni jambo dogo yaani anasahau kabisa alichokisema hapo awali kisha anataka sheria ishughurikie jambo hilo la dini kwamba ni jambo dogo.

Yaani the law does not concern itself with trifles. Then your ask the court to use the law for the same minor issues (dini "shaidi anavyobadirika badirika kwenye dini")
 
Serikali si ccm wala tume ya uchaguzi.Kwa hiyo na mgomo wa mabasi leo Tanganyika nzima unaitishia Serikali???Kwa hiyo madai yao wenye vyombo vya usfiri kwa Serikali ni uhaini??
 
Na unapokula kiapo mahakamani unaapa kwa dini yako.Je kiapo hicho cha huyo shahidi mwislam-mkristo kilikuwa kuwa halali kwa mujibu wa sheria za nchi na za Katuga mwenyewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ