Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini hapa.

Msafara wa Samia umefika hospitalini hapa saa 11.43 jioni akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana.

Mwananchi lililokuwapo hospitalini hapo wakati Mama Samia, Balozi Chana na maofisa wengine wakiwasili hospitalini hapo.

Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.

Makamu wa Rais amefika hospitalini akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa Septemba 7.

View attachment 639832

View attachment 639833

Je Viongozi wa Kiislam wana hofu ya Mungu zaidi kuliko wa madhehebu Mengine ?
 
Hakika mama Samia Suluhu Hassan ni kiumbe aliyejawa na utu na huruma kwa watanzania.

Hii picha hapo chini inajionyesha kabisa kuwa yeye ni tofauti na wenzake.
Mungu akubariki mama yetu.
20190907_204138.jpeg
 
Hakika mama Samia Suluhu Hassan ni kiumbe aliyejawa na utu na huruma kwa watanzania.

Hii picha hapo chini inajionyesha kabisa kuwa yeye ni tofauti na wenzake.
Mungu akubariki mama yetu.View attachment 1200985
Kumbuka huyo ni mama na anatumbo la uzazi anayajua machungu ya kumlea mtoto hadi kufika hatua aliyo ifikia lisu , kwa mama hiyo ni kazia kubwa sana na yenye maumivu makali sana na ndio mana alitoa chozi
 
Hakika mkuu kweli nimeamini sana mama huyu ni hazina kabisa hapa kwetu na tumuombee kila la kheri

Back
Top Bottom