Yes, mshahara hauendani na muda wa kusoma. Hata hivyo, angalau kwa madaktari na manesi serikali imejitahidi si haba. Tatizo linakuja pale ambapo nurse wa diploma anamzidi mwalimu wa degree basic salary. Yaani mtu kaishia form 4, Tena passmark za chini. Kasoma 3 years deploma. Anamzidi mshahara mtu aliyesoma zaidi ya miaka 5. Kuna haja ya kupanga upya mishahara ya watumishi wa umma. Criteria za high risk na muda wa kusoma, si kigezo peke Cha kupanga salary. Yaani walimu wanaowafanya kuwa watumishi, tunawalipa mishahara ya chini, eti kwa kigezo Cha wingi wao! Mahitaji ya uwingi yanasababishwa na wanafunzi kuongezeka Kila mwaka. Hivyo tamisemi waangalie kuwa wanafunzi wengi pia ni high risk kwa mwl. Leo walimu wengi ni wagonjwa wa macho, vidonda vya tumbo, pressure n.k ambavyo vyote hivi wamepatia kazini.