inawezekana Makonda amehusika au hajahusika. Hata kama alikuwepo Dodoma siku ya tukio haimaanishi kwamba alihusika. Inahitajika ushahidi mkubwa zaidi ya kuwepo Dodoma siku ya tukio ili kumtuhumu Makonda kwamba alihusika. Lakini kwasababu Makonda anasema hakuwepo Dodoma siku ya tukio, basi Lissu anapaswa kurudi kwa chanzo chake cha habari na akajipange upya.
Mbona unafikiri kama mtoto mdogo vile ambaye hata chekechea hawajafika aisee...?
Ni huyu huyu muhusika kwa maagizo ya boss wake aliyekuwa Rais hayati John P. Magufuli. Wewe unafikiri kwanini polisi hawachunguzi tukio hili la kishenzi kabisa kuwahi kutokea Tanganyika tangu uhuru...????
Ushahidi ni mlolongo wa matukio yasiyo ya kiungwana wala kubeba utu wa binadamu aliyotendewa victim (Tundu Lissu) na serikali ya Rais Magufuli (mtuhumiwa namba 1) wa unyama huo...
Aidha wote tunajua kuwa huyu jamaa (Paul Makonda) ndiye alikuwa "toto pendwa" wa Mwendazake na ndiye alikuwa anatumiwa kwenye kazi chafu chafu za viongozi wa serikali akiwemo Rais Magufuli personally..
Hata baada ya kuwa nje ya mifumo wa kiserikali kwa miaka kadhaa, wamemrudisha ndani ya serikali ili kuisaidia CCM kwa mikakati michafu ili kubaki madarakani. Si kwamba Samia Suluhu Hassan hajui uovu na uchafu wa bwana huyu....
Lakini afanyeje sasa na asingependa CCM imfie mikononi mwake? Cha kufanya ni hata kulazimika kumtumia shetani mwenyewe, basi ni lazima amtumie tu....
Na ndipo Samia kwa kubanwa na "establishments" (wakora) wa CCM, akaambiwa mlete yule kijana atusaidie. Ndipo choice ikawa huyu bwana arudi kazini na ndivyo ilivyo na yote mabaya yanayotokea, hapa nchini sasa yako chini ya uratibu wa huyu bwana aliyeshiba damu za watu kiasi cha mshipa wa aibu na woga kumtoka kabisa...!
Sasa turudi kwenye tukio la Dodoma 2017:
Kwamba, siku hiyo TL anakula risasi Dodoma, huko DSM ktk Ikulu ya Magogoni ndani ya mkoa wa DSM na bwana huyu akiwa RC, kulikuwa na tukio la Rais kupokea taarifa/ripoti ya makinikia ya almasi ya Mwadui - Shinyanga na kamati ya kina Ossoro (kama sijakosea)...
Ilikuwa ni ajabu kuwa, "toto pendwa" huyu kutoonekana kwenye tukio hilo tena likifanyika ndani ya mkoa wake....!!
Loooh..!!, Kumbe jamaa alikuwa Dodoma akiongoza kikosi cha mauaji ya Tundu Lissu bwanaπππ!!!!
Baada ya hapo, sasa angalia mlolongo wa matukio ya ushahidi wa kimazingira kuonesha uhusika wake na Rais wake (Mwendazake Magufuli...)ππ»ππ»ππ»
1. Kauli za Hayati Rais John P. Magufuli mwenyewe kuwa "....
Watu wote wanaoipinga serikali wakati ikiwa ktk vita ya kiuchumi, nyie askari mnajua huwa wanafanywa nini. Obviously, hawastahili kuishi...." Dakika chache baada ya kauli siku hiyo tarehe 7/9/2017, Dodoma eneo la AREA D, makazi ya viongozi, jamaa akamwagiwa risasi zaidi 37 akiwa ndani ya gari lake mchana wa saa 7 kweupe kabisa na majambazi hayo kuondoka chini ya ulinzi mkali hadi DSM....!!!!!
2. Eneo hilo la makazi ya viongozi ambalo huwa na ulinzi 7days & 24hrs mwaka mzima, siku hiyo na muda wa tukio hilo hakukuwa na mlinzi hata mmoja kwenye mageti yote..!
Swali rahisi tu ni hili: Hivi ni nani mwenye nguvu za kimsmlaka na uwezo wa kuondoa walinzi (askari polisi wote) kwenye lindo lao siku hiyo..???? Akili kichwani mwako...
3. Jengo - Apartment aliyokuwa akiishi Tundu Lissu alikuwa akiishi pia Waziri wa Nishati na Madini by then Meadard Kalemani na Waziri wa Afya (by then) Dr Haji Mponda. Aidha apartment hiyo ilikuwa na CCTV Cameras. Baada ya tukio, polisi walizichukua na mpaka leo polisi wanazo na hawataki kusema waliona nini...!!
4. Kunyimwa stahili na haki zake za matibabu huku akiwa mtumishi wa umma (mbunge....)
5. Kuvuliwa ubunge wake kwa sababu eti ni "mtoro kazini, hajulikani aliko..."
6. Job Ndugai (Spika wa Bunge by then) aliamuriwa na Rais Magufuli kuwa, akifa hata asiingizwe kwenye jengo la Bunge kuagwa na wenzake na badala yake maiti usiku kwa usiku ipelekwe kijijini kwao Singida na kuzikwa. ..
Duuh, hiyo βπ»βπ»βπ» ni chuki na unyama uliopitiliza viwango vya shetani mwenyewe...!!
7. Wananchi kuzuiliwa na kupigwa marufuku na serikali ya CCM chini ya Hayati John P. Magufuli ku - sympathize na victim, familia yake, ndugu zake, wanachama na chama chake, mashabiki na wapenzi wake (kina sisi) hadharani kuvaa t-shirt za "GET WELL TUNDU LISSU", kufanya maombi kwenye viwanja vya wazi, kuchangia fedha za matibabu nk. Waliofanya haya, basi ilikuwa ni kwa kificho sana....
8. Wabunge wa CCM kupigwa marufuku na serikali na chama chao kwenda kumuona na kumsalimu hospitalini Nairobi na Ubelgiji. Waliofanikiwa kwenda ni kwa kuwa walikuwa na roho ngumu tu na badae baadhi walitoka CCM e.g Lazaro Nyalandu...
9 Funga kazi ni DRAMA za serikali kupitia Jeshi la Polisi, kukataa kutenda wajibu wao wa kuchunguza tukio hili la kihalifu (political attempted assassination) kwa vusingizio vya mara dereva kakimbia, mara Tundu Lissu mwenye kakimbia na hataki kutoa ushirikiano na ujinga mwingine mwingi kuanzia polisi wenyewe, Rais, mawaziri, bunge na,mamlaka zingine...
##Mpaka hapo na kwa circumstantial evidences hizi tunakosaje kuwajua wahusika? Na serikali ni kwanini ilikuwa inataka kumuua Tundu Lissu kijinga na kishamba kiasi hiki..??