Mimi nimeoa ila sina ndoa , akileta nyokonyoko natimua mara moja bila kupepesa macho navuta mama nyingne , na huyo mpya akitaka tufunge ndoa nikimuuliza ataje faida kumi ambazo nitazipata nikiwa na ndoa na ww ,akishindwa jibu nampotezea akilazimisha napiga chini navuta nyingne , kama ni spirit na mapepo yananiepusha na ndoa ili afya yangu ya akili iwe sawa yaendeleee tu wala sina shida nayo.Uzinzi ni ishu za Spirit zaidi yaani pepo au jini la ngono ulilonalo.
Tafuta elimu ya kuoa ukiwa nayo utampa mwema
Huwa hamuwezi kujibu hoja za wakataa ndoa kwa nini wanakataa ndoa?Toka lini shoga akaoa?
Suala la wewe kuolewa ni suala la muda tu, ila ikiendelee kukaza fuvu lazima uolewe.Upeo wako mdogo kumbe!
Kwa taarifa yako nna watoto zaidi ya wawili na "naichakata" kisawasawa ila sina mpango wa kuoa leo wala kesho labda mnipe faida ya ndoa nje ya sex, vinginevyo #KATAANDOA
Huu uzi mshana umeandika kwa jazba kidogo, matokeo yake umeshindwa kuweka hoja mathubuti kuelimisha vijana kuhusu umuhimu wa ndoaNdoa ni muunganiko kati ya mwanamume na mwanamke, walio amua kwa ridhaa yao wenyewe kuishi pamoja kama mke na mume mpaka mwisho wa maisha yao ya ndoa.
Aina za ndoa kwa mujibu wa sheria
Kuna aina mbili tu za ndoa zinazotambulika na sheria ya ndoa Tanzania
Ndoa ya mke mmoja na mume mmoja tu.
Ndoa ya wake wengi.
Ndoa hizo zinaweza kusheherekewa kufuatana na misingi na taratibu za kidini, kimila au kiserekali, kushuhudiwa na watu wasiopungua wawili na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria.
Hatua za kuchukua kabla ya ndoa kufungwa
Lazima taarifa ya nia ya kufunga ndoa itolewe siku 21 kabla ya ndoa kufungwa, kama kutakuwa na mwenye pingamizi budi litolewe itoe kabla ya ndoa kufungwa
Majina ya wale wanaotarajia kufunga ndoa, umri, majina ya wazazi wao na mahali wanapoishi yatajwe.
Tamko kwamba wanaotarajia kufunga ndoa hawana uhusiano unaokatazwa kisheria kufunga ndoa
KUSAJILI NDOA
Ndoa inaweza kufungwa Kiserikali au kwa madhehebu ya Kikristo au Kiislam au kufuatana na mila na desturi za wale wanaofunga ndoa.
Msajili wa ndoa atatoa cheti cha ndoa. Kila Ndoa inapofungwa lazima iwe na mashahidi wawili
Mambo ambayo sheria ya ndoa inakataza katika suala zima la kuoa au kuolewa
Mwanamke na au mwanaume kuolewa/kuoa bila ridhaa yake mwenyewe
Mwanamke na mwanaume wenye undugu wa damu kuoana
Mwanamke na mwanaume kuoana kabla ya kutimiza umri unaoruhusiwa kisheria (kwa mwanaume miaka 18 na kwa mwanamke miaka 18 au 15 kwa idhini ya wazazi/mlezi wake)
Kuoana watu wa jinsia moja
Mwanamke na mwanaume kutaka kuoana kwa mkataba wa kipindi maalum.
Haki za mume na mke katika ndoa
Wote wana haki ya kumiliki mali kama nyumba, shamba n.k. kwa majina yao binafsi;
Wote wana haki ya kutoa idhini katika uuzaji au kwa pamoja kuweka dhamana mali yoyote ya familia;
Wote wana haki ya kuishi katika nyumba ya familia iwapo mume/mke amemkimbia;
Mke ana haki ya kupewa matunzo yake na ya watoto wakati wa ndoa au iwapo mume amemkimbia, wameachana kwa amri ya mahakama. Na mume ana haki ya kupewa matunzo iwapo ana ulemavu hawezi kujiingizia kipato kutokana na ulemavu au ugonjwa wake;
Wote wana haki ya kutokupigwa na au kufanyiwa ukatili wa aina yoyote;
Wote wana haki ya kupeana unyumba;
Wote wana haki ya kutumia mali ya ndoa;
Wote wana haki kuomba amri ya talaka.
Ukomo wa ndoa Ukomo wa ndoa uko wa aina mbili:
Kifo cha mwanandoa mmoja wapo
Talaka ambayo imetolewa na Mahakama pekee pale inapojiridhisha kwamba kuna sababu ya msingi kufanya hivyo.
Baraza la usuluhishi la Ndoa
Baraza la usuluhishi la Ndoa, ni baraza lililoanzisha na kifungu 102 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, sura ya 29 kama sheria zilizopitiwa mwaka 2002, kwa madhumuni ya kusuluhisha wanandoa ambao wanaingia kwenye migogoro ya Ndoa. Kazi za Baraza la Usuluhishi la Ndoa:-
Kusuluhisha Wanandoa walioko kwenye Ndoa baada ya kupokea lalamiko toka kwa mmoja wapo wa Wanandoa
Kutoa hati maalum kuthibitisha kuwa suluhu imeshindikana na kuelekeza wanandoa kwenda Mahakamani kwa amri zaidi.
MUHIMU: Mahakama peke yake ndiyo ina mamlaka ya kutoa amri ya kutengana au talaka
Sababu zinazopelekea au kuishawishi mahakama kuvunja ndoa:-
Uzinzi kati ya wanandoa
Ukatili kati ya wanandoa au watoto wa ndoa
Dharau au kupuuza kulikokidhiri dhidi ya mwenzi
Kumtelekeza mwenzi kwa zaidi ya miaka mitatu Pale mwenzi anapofungwa kifungo cha maisha au kwa kipindi kisicho pungua miaka miaka mitano
Ikiwa mwenzi ameugua ugonjwa wa akili na imedhibitishwa na daktari kwamba hakuna uwezekano wa kupona.
Kubadili dini baada ya ndoa kufungwa pale wanandoa wote walikuwa wakifuata imani ya dini moja.
Haki za wanandoa zinazoambatana na amri ya talaka
Mgawanyo wa mali za ndoa /familia
Matunzo ya mke Hifadhi na matunzo ya watoto
Kizuizi cha kutobugudhiwa
Kuoa/Kuolewa tena
Fidia ya uzinzi
Gharama za kuendesha Shauri la Talaka
Haki ya Mgawanyo wa mali za familia/ ndoa Mali yoyote ambayo imepatikana wakati wa uhai wa ndoa na kwa nguvu na au machango wa pamoja wa wanandoa.
Iwapo mali iliyopatikana na mwanandoa mmoja wapo kabla ya ndoa au kwa nguvu zake mwenyewe lakini imeboresha/imetunzwa na mwanandoa mwingine mali hiyo itatambulika kama mali ya ndoa.
Lakini kama kuna mali yoyote ambayo mwanandoa mmoja amempa mwanandoa mwenzake kama zawadi, mali hiyo itakuwa ya yule aliyepewa pekee.
Aina za mchango
Kutekeleza kazi nyumbani hasa kutunza familia; mfano kuosha vyombo, kupika, kufua nguo, kubeba maji na kazi zingine zinazofanana na hizo kwa maslahi ya familia.
Kutunza mali za ndoa: mfano kufyeka, kulima, kuvuna shamba, kufanya marekebisho ya mali za ndoa kwa maslahi ya familia.
Mchango wa fedha wa mwanandoa katika kununua mali.
Haki ya Matunzo ya mwanandoa
Jukumu la kutoa matunzo kwa mke na watoto ni la mume, jukumu hilo litatekelezwa wakati wa uhai wa ndoa na baada ya talaka.
Haki ya Hifadhi na matunzo ya watoto
Hifadhi ya watoto hutolewa kwa mume au mke au mtu baki (mlezi) hasa kwa kuzingatia ustawi na maslahi ya wale watoto. Zaidi ya hayo, mahakama pia inaweza kuzingatia yafuatayo:
Umri wa wale watoto, mfano, watoto walio chini ya miaka saba kipaumbele cha hifadhi hupewa mama mzazi; labda kama kutakuwa na sababu za msingi za kuto fanya hivyo. Mfano kama mama mzazi ana matatizo ya kiakili, anaishi katika mazingira hatarishi.
Mazingira ya mahali watakapoishi watoto, mfano, kama mazingira ya upande mmoja ni hatarishi kwa ustawi wa mtoto, basi haki ya hifadhi atapewa mzazi mwingine bila kujali umri.
Matakwa ya wazazi wa mtoto nani kati yao angependa kupewa hifadhi ya watoto
Mila na desturi za jamii ambayo wanandoa wametokea.
Kama mtoto anaumri zaidi ya miaka saba na ana uelewa wa kutoa mapendekezo yake, basi matakwa/maoni yake yatasikilizwa zaidi.
Haki ya hifadhi ya mtoto haimnyimi mzazi mwenza haki ya kumuona na au kumtembelea mtoto/watoto. Haki ya hifadhi ya mtoto haiondowi jukumu la baba kutoa matunzo.
Huu uzi mshana umeandika kwa jazba kidogo, matokeo yake umeshindwa kuweka hoja mathubuti kuelimisha vijana kuhusu umuhimu wa ndoa, umeweka zaidi vijembe.Hali inazidi kuwa mbaya kwa vijana wetu hasa hawa wa kiume wanahamasishana kila kona na kampeni yao yenye hashtag #KATAA NDOA
Sababu wanazotoa zinachekesha mno na kwakweli hazina mashiko.. Kubwa ikiwa ni kuogopa kusalitiwa lakini pia kuna la uchoyo na kukwepa majukumu ila haya hawayasemi kwa uwazi
Hili jambo ni kama fasheni yenye mass hallucination ndani yake! Itapita lakini inaweza kuacha madhara kwa wengine hivyo hatuwezi kukaa kimya
Haya ndio makundi yao
1. Wasiojiamini..
Hawaamini kama wanaweza kutunza mke kutokana na story za vijiweni
Hawaajiamini kama wanaweza kumridhisha mwanamke kitandani
Hawajiamini kama wanaweza kutulia kwenye ndoa bila kuwa na vimada
Hawajiamini kwamba watapendwa na hawawezi kusalitiwa!
2. Wenye kasoro za kimaumbile
Wanaojihisi ni vibamia
Wanaojihisi hawawezi kumpa mwanamke ujauzito
Wasiotahiriwa
Wagumba kwa ithibati
3. Waathirika kisaikolojia
Kutokana na makuzi mabaya
Kutokana na malezi mabovu
Waliolelewa na walezi katili
Walioathirika na punyeto
Walioumizwa kimapenzi
Waliosalitiwa
4. Wasela na wakaa geto
Maisha hayajasimama
Wanaishi kwa kuungaunga
Wasiopenda majukumu
5. Wenye kasoro za kijinsia
Mashoga wa kujificha (mchicha mwiba)
Madomo zege
Wenye ulemavu uliojificha
6. Wapenda kitonga, dezo
Wanaolelewa na wake za watu
Wanaotunzwa na mashangazi
Wanaopenda vya bure toka kwa yeyote
Wapenda shortcut
Wavivu wasipenda kujishughulisha
Wapenda starehe
7. Bendera fuata upepo
Wanashadadia tu kwasababu fulani kasema
Wanafuata mkumbo kwakuwa fulani yumo
Wanadhani ndio usasa na ndio ujanja
Washauri wao wakuu
Walioshindwa kuhimili changamoto za ndoa
Walioachwa, waliopigwa kibuti
Walioharibu kwenye ndoa zao
Wapotoshaji
Nisiandike sana ngoja niweke kituo hapa
Unamjibu mtu ambaye hajawahi ona baba yake
Nadhani inabidi uandike uzi wa kuwakumbusha vijana, kuhusu swala hiliKwanini wanatuandama sanaa?
Kwani si kila mtu na life style yake?
#YNWA
kama muktadha ilikuwa ni kuyataja makundi,basi hujayataja ipasavyo,Hii ni mada ya tano ama ya sita naandika kuhusu ndoa.. Na muktadha ulikuwa kuyataja makundi na si kufanya uchambuzi wa faida na hasara za ndoa.. Kama ungezingatia kichwa cha habari usingeandika haya
Unfortunately kila ukinikoti unakosea, kwanza nikurekebishe kuwa mimi siyo ke'Hii mada najua kwa 100% watakao sapoti ni wanawake maana wanajua kwamba sheria za ndoa zina wa "favour" wao....[emoji1]
Tatizo si ndoa, Tatizo ni hizo sheria za ndoa zilizopo zinazo "favour" upande wenu zaidi na kukandamiza uhuru wa Mwanaume...
Mkitaka ndoa mkubali "mfumo dume"
AiseeeDaaah Dingi kaumia sanaaa, halafu haya mambo yananzaga Utani tu . Sasa watu now days ,Ukiwa shoga au Transgender wanakuona SHUJAAA, jamiiii imekuwaje..?
Wakataa ndoa
View attachment 2511993
Mkuu niishie kusema tu, hii ndio poste yangu bora kwa mwezi huu.Hali inazidi kuwa mbaya kwa vijana wetu hasa hawa wa kiume wanahamasishana kila kona na kampeni yao yenye hashtag #KATAA NDOA
Sababu wanazotoa zinachekesha mno na kwakweli hazina mashiko.. Kubwa ikiwa ni kuogopa kusalitiwa lakini pia kuna la uchoyo na kukwepa majukumu ila haya hawayasemi kwa uwazi
Hili jambo ni kama fasheni yenye mass hallucination ndani yake! Itapita lakini inaweza kuacha madhara kwa wengine hivyo hatuwezi kukaa kimya
Haya ndio makundi yao
1. Wasiojiamini..
Hawaamini kama wanaweza kutunza mke kutokana na story za vijiweni
Hawaajiamini kama wanaweza kumridhisha mwanamke kitandani
Hawajiamini kama wanaweza kutulia kwenye ndoa bila kuwa na vimada
Hawajiamini kwamba watapendwa na hawawezi kusalitiwa!
2. Wenye kasoro za kimaumbile
Wanaojihisi ni vibamia
Wanaojihisi hawawezi kumpa mwanamke ujauzito
Wasiotahiriwa
Wagumba kwa ithibati
3. Waathirika kisaikolojia
Kutokana na makuzi mabaya
Kutokana na malezi mabovu
Waliolelewa na walezi katili
Walioathirika na punyeto
Walioumizwa kimapenzi
Waliosalitiwa
4. Wasela na wakaa geto
Maisha hayajasimama
Wanaishi kwa kuungaunga
Wasiopenda majukumu
5. Wenye kasoro za kijinsia
Mashoga wa kujificha (mchicha mwiba)
Madomo zege
Wenye ulemavu uliojificha
6. Wapenda kitonga, dezo
Wanaolelewa na wake za watu
Wanaotunzwa na mashangazi
Wanaopenda vya bure toka kwa yeyote
Wapenda shortcut
Wavivu wasipenda kujishughulisha
Wapenda starehe
7. Bendera fuata upepo
Wanashadadia tu kwasababu fulani kasema
Wanafuata mkumbo kwakuwa fulani yumo
Wanadhani ndio usasa na ndio ujanja
Washauri wao wakuu
Walioshindwa kuhimili changamoto za ndoa
Walioachwa, waliopigwa kibuti
Walioharibu kwenye ndoa zao
Wapotoshaji
Nisiandike sana ngoja niweke kituo hapa
Ndoa ni ugani wa muhogo na kisanvu.Ndoa ni nini?
Zamani we ulizaliwa?zamani ukioa ilikuwa ni fahari ila kwa nyakati hizi hadi kuku watakushangaa
Story ya kutunga hii.Kuna mshkaji wangu mmoja tulikuwa tunakaa naye vikao mara kwa mara, sasa majuzikati kajichanganya akaoa! Hivi sasa kila weekend lazima aje kwangu anipe sim niongee na mke wake nimuombee ruhusa!!!
Nimemwambia weekend hii ndo mwisho atafute njia nyingine ya kutoka kwake au atulie na familia yake aenjoy (kama mnavyodanganyana) maana ndo maisha aliyochagua.
Kabisa mkuu tatizo si ndoa, Tatizo ni wanawake wenyewe na sheria za ndoa.Nakupa asilimia mia moja zote umepata, ila kwenye kibamia ondoa, kibamia kinafanya kazi vizuri tu hata kikikutana na shimo refu pana kinatia mimba. Ni kweli waliosalitiwa wanazolewa na kampeni hizi kukataa ndoa. Huu ni upande mmoja wa kiume, je upande wa kike nao wanakataa ndoa? Upande wa kike ndio walioanza kukataa ndoa baada ya kujiona wana uwezo wa kiuchumi japo watoto wanapata kiholela, ndio hawa ma single mother. Wanapenda mapenzi lakini kuishi maisha ya ndoa hawataki na hakuna aliyeandika kukataa kwao, sasa wameibuka wanaume wakataa ndoa kwa sababu zao za msingi wanaonekana ni wa ajabu. Kwanza kwa ujumla maadili ya kijamii na kidini yameshuka. Dini zilisisitiza ndoa iheshimiwe na watu wote lakini hayo maadili yameporomoka. Kama watoto walizaliwa wakaishi na mzazi mmoja watatamani vipi wakati hawakuona umuhimu wake? Single mother ni wa kulaumiwa kulea watoto wa kiume na kike peke yao wakati si wajane, waliozaa nao wapo hai. Huu ushenzi umeanzia kwa wanawake wanaojiona wana uchumi imara kulea peke yao.
Unajuaje kama mi sijawahi kumuona baba yangu?Unamjibu mtu ambaye hajawahi ona baba yake
Ana paranoia huyoUna uhakika?