Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Utaishia kupigwa
 
Vijana mnachekesha sana!
Hivi hamuwaoni single mamas walivyokuwa na stress za kulea mtoto/watoto pasi na baba zao? Na hamjioni nyie watoto mliolelewa na single parent utofauti mlionao mkijilinganisha na wale wenzenu waliokulia kwenye ndoa? Tatizo lenu mnakimbilia kwenye material things ila kwa mwanaumme aliye kamilika na anayetambua na kuheshimu muda, utu na malezi kwa wanae lazima aoe, alee wanae katika misingi ipasayo na arithishe hiyo misingi kwa wanae. Sasa pasipo kuwa na mke, hayo mambo hapo juu yatapalanganyika.

Waulizeni watoto waliokulia mitaani na wale waliolelewa kwenye vituo vya watoto yatima athari za kutolelewa na baba na mama ktk maisha yao.

Wanandoa wanaopenda watoto wao, kamwe hawakimbilii kutalikiana. Wapo tayari kuishi ndani ya paa moja bila kupeana unyumba kwa kipindi cha hata miaka 15 ilmradi walee na kukuza watoto wao wakiwa pamoja.
 
Wanandoa wanaopenda watoto wao, kamwe hawakimbilii kutalikiana. Wapo tayari kuishi ndani ya paa moja bila kupeana unyumba kwa kipindi cha hata miaka 15 ilmradi walee na kukuza watoto wao wakiwa pamoja.[emoji1545][emoji23][emoji818][emoji817]
 
Kuna sheria ya ‘Alimony’ , yaani ni ujinga, unageuzwa mfuko wa pensheni kwa kumuacha mke wako , na unalipa kila mwezi, hata kama kaolewa, unaendelea kumlisha yeye na mme wake mpya na watoto wa mme wake mpya.., aisee, kataeni ndoa! Oeni na mzae, ila msifunge ndoa!
 
Mambo ya Beijing hayo. Wenyewe walisema "fifty fifty by twenty twenty" 50 kwa 50 by 2020.View attachment 2512581
Kumbe shida yote ilianzia hapa.., siku hizi hadi wanaume wanapigwa, na ukileta fyoko fyoko unajikuta mahakamani unadaiwa talaka, ili ulipe ‘Alimony’ na mgao wa mali zako ulizovujia jasho kama chizi
 
We jamaa, tofautisha kuoa na kufunga ndoa.., hakuna anae pinga kuoa hapa.., tunakataa ndoa!!
 
Tatizo sio mke, tatizo ni kufunga ndoa.

Unaweza kuishi na mwanamke bila ya kufunga naye ndoa mkalea watoto wenu vizuri tu...

Wapo wazee waliodumu na wake zao bila kufunga ndoa wakaishi nao vizuri tu.

Ndoa ina sheria ambazo zina egemea sana upande wa mwanamke kuliko Mwanaume.

Halafu sio kila mtoto aliye lelewa na single parent yupo tofauti na walio lelewa na baba na mama. Kuna watoto licha ya kulelewa na wazazi wote wawili bado wana maadili mabovu pia.

Mtoto kuwa na maadili mabovu sio swala la "single parent" ni swala la MALEZI gani huyo mtoto anapata kutoka kwa huyo mzazi haijalishi ni mmoja au wote wawili.

Maana pia kuna wanandoa wanafunga ndoa na mmojawapo unakuta anafariki kwa hiyo mtoro anabaki na mzazi mmoja "single parent". Kwa hiyo hapa huwezi kuhitimisha kusema kwamba kila mtoto aliye lelewa na "single parent" yupo tofauti na aliye lelewa na wazazi wote. Inategemea ni malezi gani aliyopewa huyo mtoto...


Sheria za ndoa zi angaliwe upya ikibidi ziwe na usawa kwa wote mwanamke na mwanaume sio kuegemea upande mmoja..
 
Una akili sana kaka mkubwa,,jamaa leo kachalala,,hakuna hoja yenye mantiki hata moja.
 
Mimi siyo mpinga ndoa ila jamaa hoja zako hazina mantiki kabisa,,ulichokifanya ni kuendeleza mashindano yaleyale yanayoendelea kila siku humu JF,,ungetoa hoja zenye uzito wa kuweza kumfanya mpinga ndoa ajaribu kubadili perception yake ningekuelewa,,ila kusema ety wanaopinga ndoa "hawajiamini, wana maumbile madogo sijui hawajiamini kuwa wanaweza kuwaridhisha wake zao" ni hoja dhaifu sana halafu pia ungetemea chini usitemee juu ili hizi hoja zisije kuonekana umejiongelea wewe mwenyewe,,kuwa makini na mkeo ni USHAURI.
 
mkuu hongera kwa kijitahidi kutetea hoja yako, natumani hata wadau wamekwambia nilichokuambia,hayo makundi umeyaandika kiushabiki sio kama wapinga ndoa wanavyodai kwenye hoja zao

wajibuni hoja zao bila kuwabeza kwa maneno ya kashfa
 
Mshana kila "era" fikra na mitazamo huwa inabadirika. Teknolojia nayo huwa inabadilisha mambo mengi.
Siku hizi huwa nashangaa hadi warabu wanavaa jinsi za kubana tena uarabuni ktu ambacho zamani haikufikirika.
Sisi tuliosogea umri tunadhani mambo yanatakiwa yabaki vilevile kumbe sio kweli. Wakati huamua mambo yaweje.
Wazungu walisha amua kuwa huru na mambo ya ndoa na hata kuachana bila kujali misinhi ya dini, tuliwashangaa sana! Sasa tunayashuhudia yakiyokea na mengi yusiyozoeleka yatatokea hata kama tutayazuia kwa mijeredi.
Navyoiona Dunia navyoenda kila mtu atakuwa huru na maisha yake sheria zitakazozingatiwa ni zile zinazoingilia uhuru wa mwingine.
Tukumbuke maafili ya sasa yalijengwa na Jesus , M.S.W ba akina Sokret,Plato,Cant, Ricaardo, Newton, Einstein nk.
Kuna wanafalsafa na wanasayansi wapya wanabadili fikra na kubuni fikra mpya hivyo tutarajie mambo mengi sana kubadirika tusivyotarajia.
Tutabaki kushika tama na kusikitika hiku tukiwa hatuna nguvu ya kuzuia yasitokee tusiyoyapenda.
 
Dah mkuu kumbe tulisahau kumjumlisha na lile kahaba la mengi , mengi alikua na uwezo wakuishi yae bila ndoa , ila alipofunga tu ndoa ameletea familia yake shida . Kataa ndoa mkuu ila kama hauna mpngo wa kutafuta pesa kubali ndoa kimkakati.
Tusimsahau Mrema pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…