Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Vijana acheni woga,tena vidume,au vidume jike nyie,uoga waachieni mashiii😀
 
Ukishaishi na mwanamke miezi mitatu kisheria hiyo ni ndoa ila hawajui yote haya na hoja yao nyingine ni kuogopa mgao wa nusu kwa nusu as if wanaingia kwenye ndoa kwenda kugawana mali
 
Your browser is not able to display this video.
 
Amini tatizo ni kubwa kuliko ulikojificha(sina maana ya kujificha) lakini wanume hao unaowazungumzia watatokea wapi kama hatukuwandaa...maana ukitazama tangu miaka ya 90+ tumejikita katika kumuandaa jinsia ke .....semina kibao, NGO, mashuleni nk. Ni kama mtoto wa kiume kazaliwa peke yake katika dunia hii au kashushwa kutokea mercury.....lakini tulishafikiri kuwa huyu binti anaeandaliwa anaenda kuishi na nani....maana mtoto wa kiume tangu anazaliwa hadi anakuwa kijana na kujikuta katika majukumu ya ubaba hakuna aliyemuandaa kwa namna yoyote zaidi ya yeye mwenyewe kupambana na vikwazo vyote anavyokutana navyo ajuavyo yeye....lakini tukirudi kwetu wababa muda umekuwa mdogo sana hata wa kukaa na hawa vijana wetu ili kuwaelimisha wapite wapi awasipite....so kujikuta na kizazi cha hovyo lawama zianzie kule tulikotoka, na ni aibu kuanza kuwanyoshea vidole vijana wa leo....!
 
Ahahahahahah Mshana anwzingua anaforce kua positive kwenye kila jambo, Mambo zingine aga tu hazibadilishwi ila zishapitwa na Muda.
Amini kuwa muda haupiti wewe ndie unapita....na muda utauacha...
 
Yaani watu wanapiga kampeni watu wasiingie kwenye ndoa na wakati huohuo wanapigia kampeni haki za mashoga.[emoji134]

Ama kweli, "Isaya 24
20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena."

Vv
 
Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela;[emoji2827]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…