Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Hali inazidi kuwa mbaya kwa vijana wetu hasa hawa wa kiume wanahamasishana kila kona na kampeni yao yenye hashtag #KATAA NDOA

Sababu wanazotoa zinachekesha mno na kwakweli hazina mashiko.. Kubwa ikiwa ni kuogopa kusalitiwa lakini pia kuna la uchoyo na kukwepa majukumu ila haya hawayasemi kwa uwazi

Hili jambo ni kama fasheni yenye mass hallucination ndani yake! Itapita lakini inaweza kuacha madhara kwa wengine hivyo hatuwezi kukaa kimya

Haya ndio makundi yao

1. Wasiojiamini..
Hawaamini kama wanaweza kutunza mke kutokana na story za vijiweni
Hawaajiamini kama wanaweza kumridhisha mwanamke kitandani
Hawajiamini kama wanaweza kutulia kwenye ndoa bila kuwa na vimada
Hawajiamini kwamba watapendwa na hawawezi kusalitiwa!


2. Wenye kasoro za kimaumbile
Wanaojihisi ni vibamia
Wanaojihisi hawawezi kumpa mwanamke ujauzito
Wasiotahiriwa
Wagumba kwa ithibati

3. Waathirika kisaikolojia
Kutokana na makuzi mabaya
Kutokana na malezi mabovu
Waliolelewa na walezi katili
Walioathirika na punyeto
Walioumizwa kimapenzi
Waliosalitiwa

4. Wasela na wakaa geto
Maisha hayajasimama
Wanaishi kwa kuungaunga
Wasiopenda majukumu

5. Wenye kasoro za kijinsia
Mashoga wa kujificha (mchicha mwiba)
Madomo zege
Wenye ulemavu uliojificha

6. Wapenda kitonga, dezo
Wanaolelewa na wake za watu
Wanaotunzwa na mashangazi
Wanaopenda vya bure toka kwa yeyote
Wapenda shortcut
Wavivu wasipenda kujishughulisha
Wapenda starehe

7. Bendera fuata upepo
Wanashadadia tu kwasababu fulani kasema
Wanafuata mkumbo kwakuwa fulani yumo
Wanadhani ndio usasa na ndio ujanja

Washauri wao wakuu
Walioshindwa kuhimili changamoto za ndoa
Walioachwa, waliopigwa kibuti
Walioharibu kwenye ndoa zao
Wapotoshaji

Nisiandike sana ngoja niweke kituo hapa
Vijana acheni woga,tena vidume,au vidume jike nyie,uoga waachieni mashiii😀
 
Mbona mnaji contradict wenyewe. Sielewi mpo upande upi wa kuoa? kutokuoa? Au kutokufunga ndoa? Make kuna vijana wenzako jana wamenikosoa kwamba kuoa fresh ila sio kufunga ndoa? Siwaelewi!?

Mi naona ni ujana na tu unawasumbua na wote tumepitia huko. But with time, hilo chama lenu la wapinga ndoa/kuoa mdogomdogo litapukutika tu na yatabaki majuto ya hela mlizotumia kula bata na wakati huo muda na umri utakuwa umewatupa mkono.

Itafikia mahala bata litakukataa hela nayo itakupiga chenga make savings kwako itakuwa kipengele kisichotekelezeka zaidi ya kuishi kwa mikopo.

Halafu kingine utakutana na ukinzani mkubwa toka kwa wazazi make matamanio yao ni kukuona kijana wao umeoa.
Nakumbuka mimi kabla sijaoa, kila nilivyokuwa namsalimia bi mkubwa kilio chake na nasaha zake ni msisitizo juu ya suala la kuoa. Nikajifanya nunda. Kilicho fuata ni mikosi, majuto na hatimae nikaoa.
Ukishaishi na mwanamke miezi mitatu kisheria hiyo ni ndoa ila hawajui yote haya na hoja yao nyingine ni kuogopa mgao wa nusu kwa nusu as if wanaingia kwenye ndoa kwenda kugawana mali
 
"Ndoa imara hujenga familia bora"
FB_IMG_1676051424313.jpg
 
 
wanaume wa kisasa wametoka kwenye nafasi zao kimwili na kinafsi,wababa wa leo mnamchango mkubwa kwa watoto/wadogo zenu wa kiume ksma kila changamoyo inayoletwa humu ingepewa uzito na ushauri positive basi hizi kampeni za kijinga zisingekuwepo,vijana wengi wamebaki kuwa wa kiume na si wanaume ndomana hawawezi kumudu familia ..........over
Amini tatizo ni kubwa kuliko ulikojificha(sina maana ya kujificha) lakini wanume hao unaowazungumzia watatokea wapi kama hatukuwandaa...maana ukitazama tangu miaka ya 90+ tumejikita katika kumuandaa jinsia ke .....semina kibao, NGO, mashuleni nk. Ni kama mtoto wa kiume kazaliwa peke yake katika dunia hii au kashushwa kutokea mercury.....lakini tulishafikiri kuwa huyu binti anaeandaliwa anaenda kuishi na nani....maana mtoto wa kiume tangu anazaliwa hadi anakuwa kijana na kujikuta katika majukumu ya ubaba hakuna aliyemuandaa kwa namna yoyote zaidi ya yeye mwenyewe kupambana na vikwazo vyote anavyokutana navyo ajuavyo yeye....lakini tukirudi kwetu wababa muda umekuwa mdogo sana hata wa kukaa na hawa vijana wetu ili kuwaelimisha wapite wapi awasipite....so kujikuta na kizazi cha hovyo lawama zianzie kule tulikotoka, na ni aibu kuanza kuwanyoshea vidole vijana wa leo....!
 
Ahahahahahah Mshana anwzingua anaforce kua positive kwenye kila jambo, Mambo zingine aga tu hazibadilishwi ila zishapitwa na Muda.
Amini kuwa muda haupiti wewe ndie unapita....na muda utauacha...
 
Yaani watu wanapiga kampeni watu wasiingie kwenye ndoa na wakati huohuo wanapigia kampeni haki za mashoga.[emoji134]

Ama kweli, "Isaya 24
20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena."

Vv
 
Yaani watu wanapiga kampeni watu wasiingie kwenye ndoa na wakati huohuo wanapigia kampeni haki za mashoga.[emoji134]

Ama kweli, "Isaya 24
20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena."

Vv
Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela;[emoji2827]
 
Back
Top Bottom