Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Nitaheshimu hilo mkuu , sio kwamba tuna nia mbaya tunakataa ndoa kama fimbo ya kuwarudisha kwenye mstari hawa dada zetu wamejisahau sana , na fimbo yetu ya moto ni ndoa kwa sababu ni ktu wanakipenda mno.
Shida ni elimu, mwanamke aliyelelewa kwenye misingi ya ndoa na akajifunza kwa mama yake hawezi jisahau.
 
Walio kwenye ndoa wanatamani kutoka, ndoa haina kitu cha ziada zaidi ya ngono. Nje ya ngono ni stress tupu, mifano tunayo mingi tu ( Manara, Dr.Mwaka n.k)
#KATAANDOA #NDOANIUTAPELI
Hao waliolea Jamii yaani wapate sifa hawawezi kuwa mfano halisi
 
Nafkiri umelenga kuwaumiza kihisia ama naweza sema umeamua "kujibu mapigo" maana hoja zao ni kama haujazijibu kabisa.
Ni kawaida sana kwa Binti kuonywa kuwaepuka wanaume kwamba wanaweza haribu maisha yake na hii imefanywa na jinsia zote kwa Miaka mingi lakini kwa Vijana wa kiume hali hua ni tofauti.
Hii kampeni ya Vijana kukataa ndoa haimaanishi wanaogopa mwanamke au majukumu.. wanahofia madhara yanayotokana na "Ndoa rasmi". Sheria za Ndoa zinambana Mwanamume na kumpendelea Mwanamke bila sababu za kueleweka. Na hii inafanya wanawake kutumia mwanya huu kuwafanyia ukatili Wanaume.. huenda Sheria na taratibu zikiwa updated Kampeni kama hizi hazitosikika.. Vijana wa kiume wana haki ya kujilinda kama wenzao.. usiwe ambassador wa Harmful masculinity Amigo. Change is inevitable
Kwenye kipengele kipi kwa mfano.
Mi nadhani zinamlinda mwanamke na mtoto.
Ukiacha hovyo watoto watatunzwa na nani
 
Nina marafiki wengi waliooa, naona na kusikia majuto yao. Nimesuluhisha sana migogoro ya ndoa na kujifunza mengi kupitia migogoro hiyo. Pamoja na yote ninekuwekea mifano michache ya watu maarufu wanaohangaika na ndoa zao kipindi hiki (Dr. Mwaka, Manara) na wewe nipe mifano ya watu wanaojuta kutooa.
Nje ya ndoa kuna uhuru, Sex (ngono) pia inapatikana kama kawaida, watoto unapata bila ndoa na zaidi unaepuka stress zisizo na ulazima.
Ndoa ni kichaka cha wanawake kuwanyonya na kuwavuruga wanaume.
#KATAANDOA

Lengo la ndoa ni kujenga familia bora kiroho na kimwili, familia ndio ujenga taifa bora.Duniani pote huwezi ukawa muhuni ukapewa uongozi haipo hio.
Viongozi wote wameoa
 
Lengo la ndoa ni kujenga familia bora kiroho na kimwili, familia ndio ujenga taifa bora.Duniani pote huwezi ukawa muhuni ukapewa uongozi haipo hio.
Viongozi wote wameoa
Lakini kuna watu wananyadhifa kubwa ndani ya serikali alafu hawajaoa wala kuolewa hapa Tanzania!!!!!!
 
Wanaopinga ndoa ni watoto wa masingle mother ,mtoto aliye lelewa na wazazi wake wawili hawezi kusema ndoa haina maana.
Kwakweli,kama mtu ulizaliwa ktk ndoa huwezi kubali kupita kuzaa zaa hovyo kama simbilisi.
 
Hali inazidi kuwa mbaya kwa vijana wetu hasa hawa wa kiume wanahamasishana kila kona na kampeni yao yenye hashtag #KATAA NDOA

Sababu wanazotoa zinachekesha mno na kwakweli hazina mashiko.. Kubwa ikiwa ni kuogopa kusalitiwa lakini pia kuna la uchoyo na kukwepa majukumu ila haya hawayasemi kwa uwazi

Hili jambo ni kama fasheni yenye mass hallucination ndani yake! Itapita lakini inaweza kuacha madhara kwa wengine hivyo hatuwezi kukaa kimya

Haya ndio makundi yao

1. Wasiojiamini..
Hawaamini kama wanaweza kutunza mke kutokana na story za vijiweni
Hawaajiamini kama wanaweza kumridhisha mwanamke kitandani
Hawajiamini kama wanaweza kutulia kwenye ndoa bila kuwa na vimada
Hawajiamini kwamba watapendwa na hawawezi kusalitiwa!


2. Wenye kasoro za kimaumbile
Wanaojihisi ni vibamia
Wanaojihisi hawawezi kumpa mwanamke ujauzito
Wasiotahiriwa
Wagumba kwa ithibati

3. Waathirika kisaikolojia
Kutokana na makuzi mabaya
Kutokana na malezi mabovu
Waliolelewa na walezi katili
Walioathirika na punyeto
Walioumizwa kimapenzi
Waliosalitiwa

4. Wasela na wakaa geto
Maisha hayajasimama
Wanaishi kwa kuungaunga
Wasiopenda majukumu

5. Wenye kasoro za kijinsia
Mashoga wa kujificha (mchicha mwiba)
Madomo zege
Wenye ulemavu uliojificha

6. Wapenda kitonga, dezo
Wanaolelewa na wake za watu
Wanaotunzwa na mashangazi
Wanaopenda vya bure toka kwa yeyote
Wapenda shortcut
Wavivu wasipenda kujishughulisha
Wapenda starehe

7. Bendera fuata upepo
Wanashadadia tu kwasababu fulani kasema
Wanafuata mkumbo kwakuwa fulani yumo
Wanadhani ndio usasa na ndio ujanja

Washauri wao wakuu
Walioshindwa kuhimili changamoto za ndoa
Walioachwa, waliopigwa kibuti
Walioharibu kwenye ndoa zao
Wapotoshaji

Nisiandike sana ngoja niweke kituo hapa
Huna akili wala upeo. Ndoa sio ya kila mtu, kuna watu wana sababu za msingi za kutokuoa. We unayedhani kila mtu lazima aoe ni mjinga na usieweza kufikiri. Sio lazima. Sio ya kila mtu, na hakuna dini inalazimisha. Kasome upya.
 
Mimi nimeoa, ninafamilia.

Ila wanaokataa ndoa wanahoja ya msingi Kwa kizazi cha SASA.
Mfumo unaoisapoti taasisi ya Ndoa ni mfumo wa kizamani.
Ukiona MTU anatumia mfumo wa sasa alfu muda huohuo anasema Ndoa ni muhimu ujue ni Mwendawazimu
Mfumo ni huo huo aujabadilika,sema ishu ya malezi na kutojua kuchagua.
Zamani ulichaguliwa na ndugu kwa sababu ndugu wanajua A to Z ya mwenza.
Kwa SAsa nani anatake action kwenda kuchunguza A to Z ya anapotaka kuoa au kuolewa, zaidi ya kutazama tako,ofisi,gari,muonekano wa nje,nk.
Asili bado Ina nguvu Sana juu ya maisha ya mtu labda mtu mwenyewe awe na elimu ya kutosha kuikataa asili.
1.unaoa mtoto wa msimbe msimbe ni mwanamke anaezaa hovyo hovyo na KILA mwanaume au asiyetulia na ndoa unategemea nini
2.Unaoa ukoo wa wezi, malaya, nk
3.Unaoa ukoo wenye hasira
4.Ukoo wenye maradhi ya kiroho na kimwili.

Lakini ukienda chunguza asili utayagundua.
Jiulize kwann dini na mila zinakataa sex before marriage ni sumu Sana na ndio chanzo cha talaka nyingi.
Ngono kabla ya ndoa uficha tabia mbaya za mtu.
 
Unaishi dunia ipi? Urijali haupimwi kwa ndoa maana hata mashoga wanaoa. Urijali hupimwa kwenye tendo lenyewe (ambalo hupatikana kirahisi hata nje ya ndoa) na namna mwanaume anavyoweza kupambana kimaisha.
Hao wake zenu kutwa wanachapwa na madogo mtaani, kama mngekuwa marijali kweli si mngewatuliza!?
Tunawaona wengi wenu mliooa mnashinda Bar mpaka night kali, mnarudi makwenu usiku mnene kulala tu kama ndoa zingekuwa na hiyo raha mnayohubiri msingejificha Bar na kwenye vijiwe usiku mnene.
#NDOANISTRESS #NDOANIUTAPELI
#KATAANDOA
Unapokataa ndoa unatoa nafasi ya kuolewa. Unalijua hilo ?
 
Lengo la ndoa ni kujenga familia bora kiroho na kimwili, familia ndio ujenga taifa bora.Duniani pote huwezi ukawa muhuni ukapewa uongozi haipo hio.
Viongozi wote wameoa
Kwahiyo ukioa unakuwa kiongozi Bora [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Akili za kipuuzi hizi


Kawasome wakina isack Newtown na wenzake Kwa waliyoyafanya kwenye dunia bila kuwa na hizo ndoa.

Elon musk Kwa mambo ambayo ameyafanya duniani wewe na kizazi chako hamuwez kuyafanya hata baada ya miaka 2000 ijayo na Hana ndoa.


Christiano ronaldo Hana ndoa na ni moja ya wachezaji waliofanikiwa kwenye soka.


Ulivyo mjinga na mbumbumbu unasema waliooa huwa Bora.


Mwigulu nchemba kaoa Ila kila siku anawawekea tozo maisha yanakuwa magumu Hadi akili zinawakaa sawa.

Diamond hajaoa Ila ana maisha mazuri kushinda wewe ulieoa
 
Watu kwa sababu wamekataa dini haya mbona ni madogo kuliko yajayo.
Dini imeweka miongozo yote mwanadamu aishije.
We huoni wazungu ni kama wanyama siku hizi
 
Sheria zipi za ndoa zina wafavour wanawake?
Mimi nafahamu kwa Tz kuna aina tatu za ndoa nazo ni ndoa ya kimila,kidini na kiserikali.
Hizo zote aina 3 za ndoa ulizotaja zinatambuliwa na sheria ya ndoa ya Tanzania...

Na ziko mahususi hasa hasa kuwapa
Haki wanawake kuliko wanaume.
 
Back
Top Bottom