Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sukari inafanya kazi hiyo hata maharage yanaiva haraka
Utumbo, uwe wa mbuzi au wa ng’ombe kwa asili ni mgumu, hivyo kuhitaji muda wa kutosha wa kupika ili uive.
Baadhi ya watu katika mapishi ya utumbo, hutumia viungo kama vile tangawizi, limao, papai bichi, siki na ajinamoto ili kuufanya uive mapema.
Wapo pia wanaotumia sufuria isiyoruhusu mvuke kutoka wakati wa kupika (pressure cooker) ambayo huwezesha utumbo kuiva ndani ya muda mfupi.
Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni baadhi ya mamalishe hutumia dawatiba aina ya panadol wakidai inalainisha na kuwahisha utumbo kuiva.
Mamalishe anayefanya biashara Buguruni, aliyejitambulisha kwa jina la Mama Aziza anasema hutumia panadol kupika utumbo.
Anasema alianza kutumia dawa hiyo kutokana na ushauri aliopewa na rafiki aliyekuwa akifanya kazi kwenye mgahawa uliopo Kariakoo, jijini hapa.
“Sikuwa nafahamu matumizi haya ya panadol, rafiki yangu alipokuja kwenye biashara zangu aliniona naweka tangawizi na viungo vingine, ndipo aliponiambia ili mboga yangu iive haraka niweke dawa hiyo. Nilipojaribu niliona matokeo na ninatumia kidonge kimoja hadi viwili,” anasema.
Mama Aziza anasema hafahamu iwapo kuna madhara ya kuchemsha utumbo kwa kuweka panadol, lakini alitumia njia hiyo kwa kuamini ni kilainishi kama vilivyo vingine vinavyowekwa kwenye nyama.
Mamalishe eneo la Kimanga, jijini Dar es Salaam, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, anasema anatumia dawatiba hiyo ili kuokoa muda wa kuchemsha supu.
Anasema asubuhi ni muda wenye wateja wengi, hivyo hutumia kidonge kimoja kuivisha kwa haraka utumbo na pia kupunguza matumizi ya mkaa katika upishi.
Ernest Kimbau, mtaalamu wa ufamasia, anasema madhara yanaweza kuwapo kwa sababu dawatiba ina kiwango ambacho watu wanatakiwa kutumia.
Anasema panadol ina kiwango chake na kinapozidi ni kuwa mtu amejizidishia dawa na inabadilika kuwa sumu inayoweza kuleta tatizo kwenye ini. Anasema anayekunywa supu iliyowekwa panadol maana yake ni kuwa anakula dawa bila utaratibu, kitendo ambacho si kizuri.
Mwananchi
Inabidii tu hamna namna tenaKuanzia mwaka mpya 2024 naacha kula kwa mama lishe.
Anza sasa, the earlier the better.Kuanzia mwaka mpya 2024 naacha kula kwa mama lishe.
Wala hajatoa yeye hizo taarifa mkuu ametoa madhara ya huo mchanganyikoHuyu Dr alikua anamshauri Jiwe aweke kodi kwenye simu za nje za WhatsApp alipokua kwenye wizara moja hapo hata hizi mambo za panadol inawezekana ni Kiki tuu...
Na kuna ile kitu inawekwa kwenye chakula cha broilers mbona tutafika tumechoka sanaKule biscuits za bangi,huku Panadol inapikwa.
Acha tu waupige mwingi hata km uwanjani taa zimezima kutokana na umeme kutokuwepo.
Kuna kasumba imekuwa sugu sana kwa wauza mchele kuchanganya mchele na mafuta ya kupikia wengi ya nguruwe ili mchele uwe na mng'ao mzuri. Sasa mnaohusika na ubora wa vyakura vya binadamu yani mabwana afya na bi afya hebu tasaidieni tukifa
"mabwana afya na bi afya hebu tasaidieni tukifa"! Unataka wakuzike au wakununulie sanda?