Nawasalimu wanajf wote wakubwa na wadogo,Natumaini Ni wazima na mnaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Okay,acha niende moja kwa moja kwenye mada husika .
Kuna Hawa jamaa wanaojiita QNET ,kwa kweli Hawa jamaa nashindwa kuwaelewa kabisa jinsi mfumo wao wa biashara jinsi ulivyo na njia wanazotumia
Nasema haya kutokana na kwamba mpaka Sasa ninaandika uzi huu ,
Dada yangu ameshajiunga huko kwenye hiyo biashara na huko ametoa kiasi Cha pesa ambacho Ni 4.5 M ,
Sasa swali ninalojiuliza Mimi,mbona mfumo wao wa biashara sijauelewa kabisa maana ,
Dada amejaribu kunielezea lakini sijaelewa hata kitu kimoja kutoka kwenye hiyo biashara zaidi ya harufu ya utapeli tu ambayo ninahisi
Kwa yoyote ambaye anaelewa hiyo biashara,hebu ajaribu kunielewesha Kama Ni biashara halali au Ni utapeli tu watu .
Samahani kwa uandishi mbovu.
Sent from my TECNO LB6 using Tapatalk