Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)

Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)

Hahahahhaaaa, dah huu uzi umenichekesha sana aise ila umenipa darasa kubwa pia mbali na lile nililolipata kwa wazee wa GOOD MORNING jana jioni.😂😂

Kiufupi hawa jamaa now wapo Zanzibar, wanawatafuta wazembe wenye tamaa za utajiri wa bila jasho wawapige. Juzi kati nilipokea simu toka kwa rafiki yangu wa karibu sana tena wa kitambo, baada ya salamu akaniambia kaka kuna fursa ya biashara ambayo unaweza kuifanya kwa kutumia muda wako wa ziada baada ya kazi zako (wakati ananiambia hivyo akilini mwangu ikaja picha ya forever living na oriflame😅)...nikajisemea kimoyo moyo maskini ndugu yangu huyu keshafanywa ndondocha tayari...ila nikaendelea kumsikiliza ndipo aliponiuliza ushawahi kusikia kuhusu kampuni inayoitwa QNET? Kiukweli hii kampuni ndo mara ya kwanza niliisikia kwake hiyo majuzi..nikamjibu hapana, nikahoji, inadeal na nini hiyo kampuni? Alipoanza tu maelezo meeengi na ndoto za utajiri wa kifikra nikamkatisha mazungumzo yake. Nikamuuliza, bro hii si ni zile biashara za network marketing (pyramid scheme) yani kadiri mtandao wako unapokuwa mkubwa ndipo nawe unapata credit (faida) zaidi? Akajibu kind of, ila hii ni ya utoafuti kdg...akaanza kunitajia baadhi ya watu wakubwa tu ambao wamejiunga na hiyo business, na wengine nawafahamu kbs maana hadi walimu wangu wamo, akaniambia kuna waajiriwa wengi tu wa serikalini wapo pia kujitengenezea kipato chao cha ziada (nikachoka). Nikamwambia na wewe unaamini utakuwa tajiri kweli kupitia hiyo biashara? Akanijibu ndio.

Nikamwambia watu fulani kuwa sehemu ya hiyo biashara haimaanishi kuwa iyo biashara ni inalipa kiasi hicho, inawezekana na wenyewe wamezidiwa tu na nguvu ya ushawishi ndo wakaingia...basi akaniomba bora niende ofisini kwao ili nikapate somo zaidi.. Nikamuahidi kwenda ila nikamwambia usinitarajie kuwa moja ya wadau wenu coz hizo ishu nilipokuwa chuo dodoma zilinipotezea sana muda na seminar zote za hamasa nilikuwa nahudhuria na hata zile za dar kwenye maghorofa ya posta nishahudhuria na hakuna cha maana nilichokiona zaidi ya kudanganyana kwa stori ambazo hata huyo anayekupa anajua kbs kwmb hapa jamaa namdanganya.

Baada ya hapo simu na sms zikawa hazikauki, nikasema ngoja nimridhishe jamaa yangu, ngoja niende huko ofisini nikawasikilize kdg huwenda wana jambo tofauti na forever living etc. Mwanzoni nilipofika ofisini sikuzingatia salamu yao, ila baadae nilipelekwa kwenye kichumba chenye viti vinne, akaja jamaa mmoja ndo nikasikia kwa uwazi jioni ya saa 11 akiwasalimia wenzake wawili (dada mmoja na yule rafiki yangu) ambao nilikuwanao mle chumbani kwa salamu ya GOOD MORNING...sikushangaa sana coz akilini ilinipitia kuwa huwenda ndo culture ya ofisi yao...sasa yule aliyeingia kwa goodmorning ndo akanifafanulia hiyo salamu japo sikumuuliza juu ya hilo.

Nikapigwa darasa la awali..nikapewa maelezo meeeengi na dada mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mwana uchumi (huyu alikuja baadae kdg baada ya mzee wa goodmorning kutoka mle chumbani)..wakati anafanya presentation akilini mwangu nasema huyu dada anajua lkn anaongea na nani huu upupu wake? Ila kwa kuwa niliambiwa nisimuingilie wakat anawasilisha nilivuta subra mpk alipomaliza na kunipa nafasi ya kuuliza...niliuliza maswali mengi ya msingi ila sikujibiwa nikaambiwa ili nijue zaidi inabidi nirudi mara ya pili ambapo ndo watanipa deep seminar...nikaahidi kurudi ila kimoyomoyo nikasema sitokuwa tena na muda wa kuja kusikiliza hizi stori za Alinacha. Sikutaka kumvunja moyo rafiki yangu japo nilishamuonya na kumcheka sana kwmb hakuna huo utajiri wa rahisi km munavyoaminishwa, akawa hana amani ila aliniomba nirudi siku pili na nimwambie muda wangu mwengine ili aongee na viongozi ili wajipange mapema.

Wakati darasa la awali linaendelea, nilitaka kujua tu bei ya chini kbs ya bidhaa zao ni kiasi gani, wakaishia tu kunambia bidhaa zipo nyingi na inategemea coz kila bidhaa ina bei yake...wakasisitiza ukija mara ya pili utajua yote haya. Lengo la kutaka kujua bei ya chini kbs ya bidhaa ni kutaka kutathimini kama naweza pata watu ktk jamii yangu ambao watakuwa na uwezo wa kumudu kununua hizo bidhaa ili nijipatie hizo wanazoziita Business Volume (BV) ili niwe milionea mie😂...Ila huu uzi ndo umenifungua kwmb kiwango cha chini kbs ni Milioni 4 ambazo rafiki yangu keshapigwa.

Hapa ndo najiuliza ikiwa mimi binafsi tu sina hizo milioni 4 za mchezo, je ntaweza kweli kumpata mtu mwengine wa kumlaghai alipe hizo milioni 4 kwa ajili ya saa (watch) tu!!🤔

NIMEAMUA SITOENDA TENA OFISINI KWAO, ila nitamuita privately rafiki yangu ambae keshatapeliwa na ndoto zake za kumiliki prado baada ya miaka miwili, ili nimfumbue macho kdg, maana nilishtuka dada mmoja aliponiambia kuwa ana undugu na huyo rafiki yangu, na yeye ndo aliyemshauri huyo rafiki yangu ajiunge huko, hlf anasema baadae anafikiria kumshawishi hadi mama wa rafiki yangu nae aingie baada ya kuanza kuonekana matunda ya biashara kwa mwanawe...nikajisemea mtumeee mama anaenda kupatiwa maradhi ya presha na kiharusi muda si mrefu...nna mpango wa kumuokoa mshkaji wangu aise, itoshe alipoliwa yeye asitake kuwaingiza na wanafamilia yake akakaribisha ufukara nyumbani kwao, maana naijua familia yao ni kama ya kwetu tu pangu pakavu. Ila sijui km atanielewa manake keshajazwa hasa na kutwa nzima anashinda kwenye hicho kijumba chao (wanaita ofisi) dah...maana yeye hana ajira rasmi, hao wanaojiita business partners wake walau walinambia wengine ni waajiriwa wa serikalini ikiwemo wizarani, benki na chuo kikuu. Najiuliza milioni 4 zake alizonunulia mtungi wa maji na disc ya kupunguzia nini cjui, kama angezifungulia banda la kuuzia kiepe yai si angefanya la maana kweli..dah🙆
 
Good Morning! hawa jamaa jumamosi nilienda ofisini kwao baada ya ushawishi mkubwa sana kutoka kwa rafiki yangu, kilichoniokoa siku ile na kuona utapeli mtupu baada ya rafiki yangu kunipa somo kuwa yeye anaingiza almost 7m per month, ilinibidi niombe ruksa ya kwenda kupokea simu kwa ahadi ya kurudi tena niliondoka pasipo ata kuaga.
 
Yaani stori zao haziendani na uhalisia. Anayelipwa 7m kwa mwezi ukikuamngalia mpaka mwenyewe unachoka na roho yako.
 
Jamani hawa watu wa QNET wapo kahama muwe makini.
Si Kahama tu, wapo countrywide. Hata Makambako wana ofisi ya kutapelia mazwazwa wanaopenda ku download pesa.
 
Hawa olymp trade Kuna mzee mstaafu walicho mfanya hawa jamaa baada ya kuchukua kiinua mgongo hana hamu nao hhh jamani cha bure duniani ni pumzi tu vijana tupige kazi.
 
Mkuu naomba hayo mambo 10 uliyosema ndio Utapeli wa QNET nipe kwa namba tafadhali mana hapa nilipo nimeshashawishiwa niuze hata kiduka changu ilimrandi nipate ile milioni 5,300,000/= ninunu ile bidhaa., yaani hivi naandika naamini majibu yako ndio yatakayonipa jibu rasmi niuze duka langu nikanunue au niachane na QNET kabisa.
 
We jamaa vip? Yani hujashtuka tu? Unawaza kuuza kiduka chako? achana nao hao japo najua kama sumu zao zimekuingia unaweza kuniona kama mchawi wa mafanikio yako
 
Mkuu naomba hayo mambo 10 uliyosema ndio Utapeli wa QNET nipe kwa namba tafadhali mana hapa nilipo nimeshashawishiwa niuze hata kiduka changu ilimrandi nipate ile milioni 5,300,000/= ninunu ile bidhaa., yaani hivi naandika naamini majibu yako ndio yatakayonipa jibu rasmi niuze duka langu nikanunue au niachane na QNET kabisa.
Ndio yaleyale wajinga hawaishi hapa bongo.

Hiyo pesa kwanini usiende kutanua na mademu, na kunywa bia.
Kuliko kuitoa sadaka kwa hao matapeli mkuu
 
Mkuu naomba hayo mambo 10 uliyosema ndio Utapeli wa QNET nipe kwa namba tafadhali mana hapa nilipo nimeshashawishiwa niuze hata kiduka changu ilimrandi nipate ile milioni 5,300,000/= ninunu ile bidhaa., yaani hivi naandika naamini majibu yako ndio yatakayonipa jibu rasmi niuze duka langu nikanunue au niachane na QNET kabisa.
Utaingizwa mjini, shauri yako
 
Ukisikia kupigwa miti ndio huko sasa.
 
Back
Top Bottom