Kila ukiandika maandiko, 1000 ndivyo unavyo-prove ulivyo kiazi.
Kumsaidiaje Mwananchi?
Wananchi wanatakaje kusaidiwa??
Una akili timamu??
Watu wanataka usimamizi mzuri wa mali zao, sera na kodi ili wajiletee maendeleo, siyo msaada.
Siyo kusaidiwa.
Achana na huu uzamwamwa wenye ujasiri.
Unawezaje kuleta mabadiliko bila kuwa kwenye chombo cha maamuzi.
Unawezaje kukusanya kodi au kuingia mikataba ya raslimali nje ya vyombo vya maamuzi, wewe taahira??
Unaweza kutengeneza sera nzuri za mali asili, kupinga rushwa, usalama, sheria bipa.kuwa kwenye chombo cha maamuzi?
Una-sound kama juha fulani, lililewa chimpumu.
Lugha unayoitumia ni kiashiria tosha kwamba huna msaada kwa jamii.
Huwezi kutumia lugha ya kujiheshimu na kuonyesha hadhi ya juu ya heshima.
Unajaribu kutumia lugha ya hasira kuridhisha hisia zako. Kwa bahati nzuri sitakujibu kama mgonjwa mwenzako. Nitakujibu kama Daktari anayejua tiba yako.
Iko hivi kijana,
Wema, uzuri, maendelea na mambo yote mazuri hayahitaji upate nafasi ya juu ili kuyaonyesha na kuyafanya.
Unamuona Kijana Malisa, ni kijana wa CHADEMA anasaidia watu, hasubiri nafasi za juu.
Hoja yako kuhusu dhulma, ufisadi, ukosefu wa usawa, ubadhirifu n.k. ziko sawa.
Na hoja hizohizo walizutumia TANU ambayo sasa ni CCM walipokuwa wakipigania nchi dhidi ya Mkoloni. Nini kilitokea baada ya wap kufanikiwa?
Serikali ni Watu. Watu wanatamaduni. CHADEMA, CCM, ACT wanatoka kwenye jamii zenye tamaduni zilezile.
Wapo CHADEMA mama na ndugu zao ni CCM, wapo CCM ambao mama na ndugu zao ni CHADEMA.
Sio kwamba chama Fulani kinatoka ulaya au kinatoka mbinguni nope!
Ndio Maana Leo msigwa alikuwa TLP, Kesho akawa Chadema, Kesho kutwa CCM mtondogoo Chadema.
Suala la mabadiliko ya kisiasa yanategemea zaidi utamaduni, malezi ya familia,
Sio ajabu MTU anataka Uhuru wa kujieleza lakini ukienda kwake mkewe Hana huo Uhuru wa kujieleza.
Mtu anapinga ukandamizaji wa haki na utu wa binadamu lakini huyohuyo ndiye anatukana watu huko mitandaoni.
Fikiria wewe ndiye unayepigania Haki na Uhuru lakini muda huohuo unavunja haki za watu wengine kwa kuwatukana.
Ni kwamba unatoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako wakati unaboriti katika jicho lako