Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu wastaafu watembelea Bwawa la Nyerere la mto Rufiji
Leo Marais wastaafu Mwinyi na Kikwete wamezulu Bwawa la maji la umeme aliloanza kulijenga Rais Magufuli

Aidha, Jakaya Kikwete amemsifu Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa kujenga Bwawa, Amesema wao waliishia kwenye mpango tu na mara ya mwisho mpango waliufanyia marekebisho mwaka 2014 kuhusu Bwawa hilo

Rais Kikwete ameuliza maswali magumu kwa Ma engineer na ameridhika na majibu yao, Aidha amewapongeza Ma engineer wa kitanzania Katika mradi huo

Rais Mwinyi, Amesema kwa mara ya kwanza ameona maajabu jinsi vijana wa kitanzania wanavyochapa kazi, Amesisitiza kuwa ni Furaha kubwa vijana waliosomeshwa na serikali wanachapa kazi kwa ufanisi mkubwa sana

Rais Mwinyi amesisitiza nguvu kubwa itumike kupeleka watoto shule kwa level kubwa zaidi

Kwenye ishu za ujenzi JPM alikuwa mwamba sana,Atakumbukwa kama mjenzi wa barabara nchi nzima kabla na baada ya kuwa Rais, Kwenye ishu za demokrasia hakuwa vizuri sana JPM
 
Kinyago kile Cha 420 mil kinapata nafasi kubwa ya kusimikwa rasmi .
 
Mzee wetu Mwinyi katumikia taifa kwa uaminifu na uadilifu ningetamani kuona anapata muda mwingi wa kupumzishwa kuliko kufanya mizunguko mingi ambayo si ya lazima kwake. Hivyohivyo kwa mjane wa JKN pia angeachwa kwa sasa apumzike.

Ushauri tu
 
Mradi unazikwa rasmi baada ya kumzika Engineer mkuu wa mradi huo!!!Sasa kampuni ya IPTL mpya inazaliwa upya!!jamaa wanakula maisha utadhani wataishi milele aiseh!!!Mnikumbuke na mimi sasa nile angalau !!!
 
Baadae wataenda kuangalia maeneo yanayopendekezwa kujenga Bandari huko Bagamoyo 😂😂
hahahaaaaaaaaa! umeona eee? ukiwa na akili hauhitaji mamisuli makuuubwa!

pia ni ishara kwamba, tofauti na yeye mwendazake ambaye kutwa kucha ilikuwa kuwaponda tu wenzake, wenzake wako poa tu, hawana shida yoyote na miradi yake katika kuipa credit! hata flyovers nakumbuka alizianzisha kikwete, lakini leo sifa zote kwa mwendazake na jk anachukulia poa.....tabasamu tele usoni.
 
Kwa kutambua umuhimu wa mradi wa kufua umeme wa Mto rufiji Marais wastaafu na mawaziri wakuu wastaafu wametembelea bwawa la kuzalisha umeme la NYERERE

Hii ni hatua kubwa za kuenzi legacy ya JPM Ndio maana tunasema JPM rest in power
===

Viongozi wakuu wastaafu Rais Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete,wameongozana na mawaziri wakuu wastaafu Cleopa Msuya, John Malecela na Mizengo Pinda kutembelea utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere.


PICHA: Marais Wastaafu Mzee Kikwete upande wa kulia na Mzee Mwinyi kushoto


PICHA: Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pind
View attachment 1842458
Huyu ni kama Malecela
 
Watanzania wasiposimlia mambo makubwa aliyoyafanya JPM kwenye nchi yake na kwa Watanzania, Aridhi itasema, mito itasema, anga litasimulia, maziwa yataisimulia kwamba huyu mtu hakuwa mtu wa mchezomchezo,

R.I.P JPM
Tahadhari:
Hiyo Stiglers Gorge ni kitendawili, yaweza malizika kujengwa nje ya muda na kusababisha cost overrun hata ya Mara 3 ya original bid. Then kukamilika ni kitu kimoja na kupata Megawati 2100 ni kitu kingine. Kumbuka umeme wa kutegemea maji hutegemea vilevile kudra za Mwenyezi Mungu.
Wacha kushona mbeleko kabla mtoto hajazaliwa. Ni mapema mno kusherehekea umeme wa Stiglers Gorge. Changamoto zilizoikumba miradi ya ya Mtera na Kihansi hamna namna Rufiji itazikwepa
 
Watanzania wasiposimlia mambo makubwa aliyoyafanya JPM kwenye nchi yake na kwa Watanzania, Aridhi itasema, mito itasema, anga litasimulia, maziwa yataisimulia kwamba huyu mtu hakuwa mtu wa mchezomchezo,

R.I.P JPM
Hakuna la maana alikofanya MWENDAZAKE zaidi ya kuharibu baioanuai ya Selous kwa kufueka miti yenye ukubwa sawa na Mkoa wa DSM.

Megawatt 2100 angezipata kwa gesi ya Mtwara tu.

Sioni kwa nini mnamtukuza yule kichaa ambaye alikuwa hasikii ushauri wa wataalamu. Alivyo bounce kwenye KOROSHO na COVID-19 ndiyo atakavyo bounce na kwenye umeme wa Stiglers japo tayari amekwisha kufa
 
Hakuna la maana alikofanya MWENDAZAKE zaidi ya kuharibu baioanuai ya Selous kwa kufueka miti yenye ukubwa sawa na Mkoa wa DSM.

Megawatt 2100 angezipata kwa gesi ya Mtwara tu.

Sioni kwa nini mnamtukuza yule kichaa ambaye alikuwa hasikii ushauri wa wataalamu. Alivyo bounce kwenye KOROSHO na COVID-19 ndiyo atakavyo bounce na kwenye umeme wa Stiglers japo tayari amekwisha kufa
Hivi unajua kusoma na ukaelewa ulichosoma..!!

Mimi nimesema, Ni mito, bahari, anga, maziwa na aridhi zitasimlia matendo ya JPM na siyo wewe...! Eboh!!
 
hao walileta ujuaji na kuanzisha vita na mtoto wa mjini, akawatawanya vibaya...hawaonekani tena mjini wamemuachia Mzee wa saigon mji..
Hivi wote walipanda hilo chopa? Nimeona ktk tv.
 
Back
Top Bottom