Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu wastaafu watembelea Bwawa la Nyerere la mto Rufiji
Mzee wetu Mwinyi katumikia taifa kwa uaminifu na uadilifu ningetamani kuona anapata muda mwingi wa kupumzishwa kuliko kufanya mizunguko mingi ambayo si ya lazima kwake. Hivyohivyo kwa mjane wa JKN pia angeachwa kwa sasa apumzike.

Ushauri tu
Kweli kabisa Mzee Mwinyi binafsi nampenda kwa dhati kutoka moyoni ningependa kuwa namuona kwenye hafla za birthday siyo kumpandisha juu ya hivyo visima aanze kulala anaota bure. Mwacheni huyo mzee mjanja mjanja afanye hayo yanamfaa maana atatwambia ye ndo alianzisha huo ujenzi kimaandishi wakati hali alotuacha nayo tunaikumbuka. Sana sana mwendo wa power tiller ndo tulizokuwa tunaziona mtaani.
 
Mradi unazikwa rasmi baada ya kumzika Engineer mkuu wa mradi huo!!!Sasa kampuni ya IPTL mpya inazaliwa upya!!jamaa wanakula maisha utadhani wataishi milele aiseh!!!Mnikumbuke na mimi sasa nile angalau !!!
Hata haueleweki
 
sikia mwenyewe baada ya marais wastaafu na mawaziri wakuu wastaafu kutembelea mradi wa kufua umeme wa Stieglers.
Kikwete alikuwa na haya ya kusema.
 
Only that the dam. age is huge and permanent men. Does the global resistance to inadequately tested vaccines make sense? Sumu haionjwi!. Majuto mjukuu. Mwenda tezi an omo, marejeo ngamani!. Siyo hivyo.

Ahsante Mheshimiwa, ila nasikitika amechelewa kwenda kuona. Natamani, hizi pongezi zingetolewa wakati Mh. Magufuli yupo, pengine asingekuwa anatukanwa na kudhalilishwa wakati yuko mbele za Haki.
Naomba watu waone tofauti ya Magufuli na marais wengine.
 
Yapo mengi mazuri ya JPM.Apumzike kwa amani.
 
Watanzania wasiposimlia mambo makubwa aliyoyafanya JPM kwenye nchi yake na kwa Watanzania, Aridhi itasema, mito itasema, anga litasimulia, maziwa yataisimulia kwamba huyu mtu hakuwa mtu wa mchezomchezo.

R.I.P JPM
Hizi sifa ni za Mungu aliye juu ndugu yangu sio mwanadamu
 
Rais wa awamu ya nne wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete baada ya kutembelea mradi wa kufua umeme wa mwl Nyerere amekiri wazi kuwa Dk Magufuli rais wa awamu ya tano alikuwa na maamuzi magumu.

Kiwete amesema mradi huo ni mkubwa na unahitaji zaidi ya trillion 6 mpaka kukamilika kwake.

20210706_101451.jpg
 
Watanzania wasiposimlia mambo makubwa aliyoyafanya JPM kwenye nchi yake na kwa Watanzania, Aridhi itasema, mito itasema, anga litasimulia, maziwa yataisimulia kwamba huyu mtu hakuwa mtu wa mchezomchezo.

R.I.P JPM
Kama heza zilikua zake sawa. But kama ni hizi kodi zetu raia...huu utopolo tafuta mahali pa kuuweka.
 
Marais Wastaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. John Samwel Malecela na Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda wakisafiri kwa treni katika reli ya kisasa (standard gauge) kutoka Ngerengere Mkoani Morogoro hadi Pugu Mkoani Dar es Salaam leo Julai 06, 2021.

===

1625589209607.png

1625589283315.png
 
Back
Top Bottom