Marekani, Israel wanashirikiana na ISIS kufanya ugaidi Iran. Huu ni uoga wa hali ya juu

Marekani, Israel wanashirikiana na ISIS kufanya ugaidi Iran. Huu ni uoga wa hali ya juu

Wacha kujitoa ufahamu huku ukijidai unafahamu.

İran na Iraq walipigana kwasababu gani?

Iran na Saudia kwasababu gani tena huku mmarekani akimsaisia Saudia dhidi ya Iran?

Unadhani ni kwanini Saddam ambaye ni Sünni aliweza kuondolewa madarakani na Shia ambao ndo wengi Iraq na ambao waliuwawa na Saddam kwasababu ya kutaka kusapoti ndugu zao Iran.

Pole sana.
Fitna za Mmarekani.
 
Wacha kujitoa ufahamu huku ukijidai unafahamu.

İran na Iraq walipigana kwasababu gani?

Iran na Saudia kwasababu gani tena huku mmarekani akimsaisia Saudia dhidi ya Iran?

Unadhani ni kwanini Saddam ambaye ni Sünni aliweza kuondolewa madarakani na Shia ambao ndo wengi Iraq na ambao waliuwawa na Saddam kwasababu ya kutaka kusapoti ndugu zao Iran.

Pole sana.
Saddam aliondolewa na shia!?..kawavalishe Pedi nguruwe mushi,wapo hedhi
 
Sasa kwanini dini yenu iwe kichaka cha kuunda makundi ya kigaidi?!
Isis, alqaeda, alshabaab, alnusra, Islamic jihadi, bokoharam, hamas, adf, Abu Sayyaf, Muslim brotherhood, Hezbollah nk.
Huoni kama kuna shida Majani?
Ukitaka kudili na mashariki ya kati tumia dini,latin America Kuna makundi mengi,kwa kuwa wao hawajali dini,panatumika fedha,the best way of predicting the future is creating it,ndiyo mtazamo wa mabeberu
 
Sasa kwanini dini yenu iwe kichaka cha kuunda makundi ya kigaidi?!
Isis, alqaeda, alshabaab, alnusra, Islamic jihadi, bokoharam, hamas, adf, Abu Sayyaf, Muslim brotherhood, Hezbollah nk.
Huoni kama kuna shida Majani?
Sasa ulitaka shetani aunde vikundi kutumia nini zaidi ya maadui zake?

Ataenezaje chuki adui yake achukiwe?
 
Ukitaka kudili na mashariki ya kati tumia dini,latin America Kuna makundi mengi,kwa kuwa wao hawajali dini,panatumika fedha,the best way of predicting the future is creating it,ndiyo mtazamo wa mabeberu
Alshabaab, bokoharam, adf, magaidi kule msumbiji na kibiti kote huko yameundwa na mabeberu?
 
Alshabaab, bokoharam, adf, magaidi kule msumbiji na kibiti kote huko yameundwa na mabeberu?
Magu alisema watanzania tuungane, mabeberu wanatamani rasilimali zetu,hiki ni kipindi kibiti panawaka moto,delta ya mto rufiji Kuna mafuta,msumbiji Kuna gas,mwambao wote wa afrika mashariki toka somalia palikua panawaka moto,huko mtwara Pana magaidi wasomali,wa kibiti walikimbilia msumbiji,unganisha dots
 
Wacha kujitoa ufahamu huku ukijidai unafahamu.

İran na Iraq walipigana kwasababu gani?

Iran na Saudia kwasababu gani tena huku mmarekani akimsaisia Saudia dhidi ya Iran?

Unadhani ni kwanini Saddam ambaye ni Sünni aliweza kuondolewa madarakani na Shia ambao ndo wengi Iraq na ambao waliuwawa na Saddam kwasababu ya kutaka kusapoti ndugu zao Iran.

Pole sana.idini
Kwann waisilam wanapo pigania ni razima muhusishe na mambo ya kidini ila nyinyi wakristo mkipigana hakuna anaye husisha migogoro yenu na dini.
Iraq iliivamia Iran kwa lengo la kupora ardhi ya Iran.
Vita ya uwakala kati ya Iran na Saudia huko Yemen ilikuwa ya kugombania ushawishi wa kusiasa.

Kwann Uadui kati ya Urusi na Marekani ahuusishi na dini?

Ila uadui wa Iran na Saudia Arabia unauhusisha na dini.
 
Ni mapenzi na utumwa wa kiakil.

Mwenyezi Mungu Anasema; Hawatakuwa Radhi na ninyi Mayahudi na Manaswara mpaka mfuate mila zao....Chuki na mambo Waliyoyaficha Manaswara na Mayahudi katika Vifua vyao Ni Makubwa Kuliko Mlima Uhud na Sinai.

Yarabbi Wahifadhi Ndugu zetu Wa palestina, Waepushe na Maovu ya Makuffar.
 
Kwann waisilam wanapo pigania ni razima muhusishe na mambo ya kidini ila nyinyi wakristo mkipigana hakuna anaye husisha migogoro yenu na dini.
Iraq iliivamia Iran kwa lengo la kupora ardhi ya Iran.
Vita ya uwakala kati ya Iran na Saudia huko Yemen ilikuwa ya kugombania ushawishi wa kusiasa.

Kwann Uadui kati ya Urusi na Marekani ahuusishi na dini?

Ila uadui wa Iran na Saudia Arabia unauhusisha na dini.
Fitna tu.
 
Mtume alipokufa hakusema mrithi wake Nani, matokeo yake wafuasi wake wakagawanyika makundi hasimu Maliki.

Kundi la kwanza Wafuasi wa baba mkwe (Abubakari) na mfadhili mkuu wa Mtume na most powerful person kwenye kundi la mtume

Kundi la pili ni mkwe wa mtume na kipenzi chake ( Ali)

Washia wanaamini Ali na familia ya mtume ndio walitakiwa/wanatakiwa kuongoza umma wa kiislam.

Washia wana hadhiti za masikitiko walivoteswa na wasuni, mfano kuharibika Mimba Mke wa All hadi vifo vyao, kibaya zaidi hadi Leo hukumbuka ni mauaji ya Kalbara, pia Washia wanadai wakati mtume wao Ana kufa aliomba pen na karatasi aandike mrithi na mali Akina Abubakari wakachelewa makusudi hadi alipokufa.

So Washia na Wassuni hawataacha kuuana
 
Hata Sheikh wetu nchini Tanzania, mwanazuoni Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania aliwahi kuonya juu ya dhehebu moja kuanza fitna, misuguano, kutishiana n.k dhidi la dhehebu jingine, wakati wote ni dini moja ya ki-Islamu..

19 January 2023
Dar es Salaam, Tanzania

SHEIKH ABUU - HATARI INAKUJA TUSIPOTOA TAHADHARI KWA HAYA YANAYOENDELEA



Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania ametoa tahadhari hiyo kwa kuwa inaweza kupelekea amani kuvunjika nchini Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi CV (wasifu) yake imesheheni nyadhifa kadha wa kadha sawia na maktaba yake binafsi iliyosheni mabuku juu ya mabuku ya elimu duniya na ilm ya dini pia ktk utumishi ulitukuka kwa dini na jamii.

Pia sheikh Abuu Iddi ni imamu mkuu msikiti wa Masjid Mnyamani Buguruni jijini Dar es Salaam. Pia kwa miaka 16 amekuwa akiendesha kipindi ktk kituo cha televisheni cha Channel Ten kutoa daawa na darsa, mratibu Al Risala Foundation, Mratibu wa Kudumisha Amani katika mkoa wa Dar es Salaam, Mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina Misingi 15 ya amani, mwandishi wa makala katika gazeti kubwa la Mwananchi pia ni Mshauri wa dini na jamii wa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi ameelekeza tahadhari hii hususan kwa madhehebu ya Sunni Saudia na Shia linaloegamia Iran yanayo shambuliana kupitia propaganda kutoka maeneo mbalimbali ya dunia ya mitandao ya kijamii wakiongozwa na viongozi wao wa ndani na nje ya nchi kuchochea misuguano
 
Watanzania tuache kukurupuka, mihemuko, chuki, jazba, kunyooneshana vidole, udhanifu, giliba n.k bali nuru ituongoze kuwakumbuka ndugu zetu jirani kabisa na hapa nyumbani yaani DR Congo, Darfur, Sudan, Cabo Delgado Mozambique n.k na hata hapa Tanzania wanaopitia changamoto kubwa.

BUSARA ZA MABABU ZETU KINA SHEIKH ABDALLAH SEIF BIN LINGANAWEKA, ZITUMIKE BADALA YA MIHEMUKO KUFUATA MKUMBO BILA KUULIZA MASWALI

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania na kwanini dhehebu la Shia lina kanuni la kukubali vijana wao kuuliza maswali (tabligh) wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1



KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.

Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi.

Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...

Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...

Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni kijijini. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu ya Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa yote hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo kijana Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.

Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa ustadhi, waalimu au masheikh wake.

Safari ya Sheikh Abdallah Seif, kundi lake wenzie katika msafara vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq

Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika alofikiri ni wamarekani weusi, ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kina Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.

Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke nchini Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.

Sheikh Abdallah Seif na kundi lake wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.

Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.

Hatimaye mwaka 1980 baada ya kusoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.

Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi aliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2



Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.

Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.

Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.

Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wenye umri wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika jumla ya miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.

Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.

Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia

RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif



Source : Asadiqmedia
 
Bibi una ushahidi ama unaropoka tu kufurahisha genge?
Hujamuelewa tu,hapo ni kwamba Kama sio Marekani kuivamia Iraq basi ISIS isingekuwepo! ni Kama vile useme Chadema imeundwa na CCM !
ikimaanisha Kama sio serikali ya CCM kukubali mfumo wa vyama vingi 1992 basi Chadema isingekuwepo
 
Back
Top Bottom