Wewe ni mwongo sana!!Shida ni kwamba US imedhalilishwa.. wanachofanya sasa ni kutafuta namna ya kujitoa lakini kwa ku declare ushindi..
Sababu ya mapigano ya sasa ni kwa sababu Iran imeshambulia baadhi ya meli za mafuta zilizokuwa zinapita kwenye mkondo wa bahari wa Harmuz kwa madai kuwa hawajafuata utaratibu ulioweka na Iran. Marekani inadai kuwa mkondo wa bahari wa Harmuz, ni international water, haumilikiwi na nchi yoyote, na hivyo kitendo cha Iran kuzishambulia meli zinazopita kwenye mkondo huo kwa madai ya kutofuata utaratibu wa Iran ni uvunjifu wa mkataba wa kumaliza vita uliosainiwa. Hivyo Marekani ikashambulia vituo zaidi ya 140 vya jeshi la Iran, kwa madai kuwa inaondoa tishio la Iran kushambulia meli zinazopita kwenye mkondo wa bahari wa Harmuz. Zaidi ya hayo, Marekani imerudisha zuio la meli yoyote kutoka au kuingia kwenye bandari za Iran.