Mary Chatanda: Freeman Mbowe amekosa shukrani kwa Rais Samia pamoja na kumtoa gerezani. Huenda ameathirika kisaikolojia

Mary Chatanda: Freeman Mbowe amekosa shukrani kwa Rais Samia pamoja na kumtoa gerezani. Huenda ameathirika kisaikolojia

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa Mary Chatanda amemshukia vikali Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe kwa kile alichokieleza kuwa amekosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alimtoa gerezani alikokaa kwa muda mrefu tangu kipindi cha utawala wa serikali ya awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Dkt.John Pombe Magufuli

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara Mkoani Lindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara zake kwenye mikoa ya Kusini mwa Tanzania Chatanda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM amesema, hivi karibuni Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amekuwa akimtukana Rais Samia kwa kueleza kuwa ameuza nchi jambo ambalo halina usahihi na linachonganisha Wananchi, hivyo kutoa wito kwa Wananchi hao kuwapuuza na kutowasikiliza pale watakapoitisha mikutano yao

"...anazungumza, anamtukata, anasema ameuza nchi, kwani sisi tumeuzwa hapa tulipokaa?, Kuna mtu anayesema kuwa nimeshawanunua ninyi ni watu wangu?, Wakija msiwasikilize.., anasema anaenda kujiandaa mikutano 70..."

Ameendelea kueleza kuwa kinachotokea kwa Mbowe sasa inawezekana ameathirika kisaikolojia baada ya kuwa jela kwa muda mrefu hivyo alipaswa kutulia kwakuwa jela kuna mambo mengi.

Chanzo: Jambo TV
Swali. Kama serikali ya mama yetu haijafanya kosa,,kukosa shukrani kwa Mbowe kunakujaje Sasa? Kwamba angemezea tu? Mnatuchanganya ss wananchi
 
Viongozi waongo namna hii, CCM huwa inawaokota wapi?

Huyu Mama ni mwongo sana, sijui ni kwa makusudi au kukosa kumbukumbu. Anataka kuwadanganya watu kuwa Mbowe aliwekwa ndani na kutengenezewa kesi ya ugaidi na Hayati Magufuli, jambo ambalo ni uwongo mkubwa.

Samia alulitangaza kuwa masuala ya katiba yasimame kwanza mpaka ajenge uchumi. Mbowe akajibu kuwa hawatasubiri. Baada ya hapo wakamweka Mbowe ndani na kumtengenezea kesi ya ugaidi.
 
ameathirika kisaikolojia baada ya kuwa jela kwa muda mrefu hivyo alipaswa kutulia kwakuwa jela kuna mambo mengi

Jaji mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande akiwasilisha ripoti kuhusu mfumo wa haki jinai ikulu, mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisisitiza kuwa mindset fikra za tufanye kazi za haki jinai kwa mazoea ibadilike.

Sasa huyu mwenyekiti wa taifa UWT, Mary Chatanda kada wa CCM bado ana mabaki ya kulilia mfumo wa haki jinai mbovu uendelee kutesa raia wasio na hatia. Kweli ni ngumu CCM na viongozi wake wengi kubadilika. Maneno ya mheshimiwa rais Samia yalinukuliwa pia na gazeti la serikali la Daily News ukurasa wa kwanza

DailyNews.co.tz : Justice dispensation : We must change mindset - Samia

1 day ago — “I support the suggestion of the Chairman of the Commission, retired Judge Mohamed Othman Chande and Chief Justice

15 July 2023
Ripoti ya Tume ya Haki Jinai

Hotuba ya Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai akiwasilisha taarifa rasmi ya Tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai hapa Nchin

TOKA MAKTABA:

Wakiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu leo wametoa ripoti nzuri.

Hawamungunyi maneno na baadhi yao walipata kuyasema haya haya mbele ya Rais John Pombe Joseph Magufuli na leo 2023 kupitia ripoti kamili wanarudia mbele ya mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan.

Serikali iifanyie kazi haraka ripoti hii, kutengeneza framework ya utekelezaji wa mapendekezo haya na kupeleka muswaada wa dharura bungeni sheria kusapoti haya mapendekezo ili wale wote walio ktk kamati za ulinzi na usalama kuanzia ma- DC, wanasiasa na polisi wapewe vijitabu vikae ktk meza ofisini kwao na pia wakati wa vikao vyao vya ulinzi na usalama wavibebe.

Rais wa awamu ya tano Rais John Pombe Magufuli mwaka 2018 wazee hawa walimwambia 'live' mapungufu haya lakini hayakufanyiwa kazi awamu ya 5 ya serikali ya CCM.

Leo hii tena baadhi ya wazee haohao 2023 wamepata nafasi nyingine wamefika ikulu wanamuambia mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan mambo yaleyale.

Ni matumaini sasa ni wakati wa kutekeleza mapendekezo haya muhimu kwani serikali inaongozwa na chama kilekile, ilani ile ile na viongozi walewale wa kisiasa na kiserikali na wa mfumo wa utumishi katika taasisi za haki jamii waliokuwepo mwaka 2018 na leo bado wapo ktk utumishi mwaka 2023.

Kutoka maktaba:

Ni kweli kabisa mfumo wa Haki Jamii na taasisi zake nyingi haupo huru

Mfumo wa Haki Jamii unapaswa sasa kuanza kuacha kutumiwa na dola, ili ufanye kazi kwa haki ndiyo utakuwa mfumo Haki Jamii unaosimamia sheria na katiba bila kupokea amri toka mhimili wa executive (wanasiasa / serikali)

Kwa mfano Jaji Mkuu mstaafu jaji Barnabas A . Samatta ameandika kitabu kinachogusa sehemu ya mfumo wa haki jamii kuhusu uhuru wa mahakama na hakika inatakiwa raia wote ikiwemo jaji mkuu aliyepo ofisini, majaji, mahakimu kukisoma na kuwa rejea kuhusu umuhimu wa mhimili wa Mahakama katika nchi hususan yetu ya Tanzania

1689583873695.png

Barnabas A. Samatta, Jaji Barnabas A. Samatta, alikuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kutoka 2000 hadi 2007. Huko nyuma, 1984-1987, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe. Yeye ni mjumbe mwanzilishi wa Judicial Integrity Group (Kikundi cha Uadilifu wa Mahakama), chombo huru cha cha kimataifa kinacho jishughulisha na ukuzaji wa uadilifu wa mahakama duniani na ambacho kilitunga Kanuni za Bangalore za Mwenendo wa Mahakama. Kwa wakati huu, yeye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Bodi ya Kampuni ya Earth, Energy and Environment Mediation Limited yenye makao makuu yake London, Uingereza, ambayo inashughulikia njia bora za kuzuia au kutatua migogoro barani Afrika inayohusiana na ardhi, mafuta, madini, maji au mazingira. Vilevile, Jaji Samatta ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe. Katika baadhi ya hukumu, makala na hotuba zake amesisitiza sana juu ya umuhimu wa uhuru wa mahakama, usawa mbele ya sheria na upatikanaji wa haki kwa unafuu na wepesi kwa kila mtu katika jamii. Katika kitabu hiki, anazungumzia kwa ufasaha, lakini kwa lugha nyepesi kuelewa, na kwa namna isiyomchosha msomaji, masuala mengi muhimu sana katika uwanja wa utoaji wa haki. Miongoni mwake ni uhuru wa mahakama; rushwa; ugumu wa kazi na maisha ya jaji; mikwaruzano baina ya mihimili ya dola na utumiaji wa kiuonevu wa mamlaka ya dola. Hiki ni kitabu kwa mwanasheria na kwa mlei. Ni kitabu kwa mtawala na mtawaliwa. Kwa kweli, ni kitabu kwa kila mtu.

5 July 2018
Ikulu mbele ya John Pombe Magufuli

Umuhimu wa utawala wa sheria - Jaji Barnabas A. Samatta

Sheria zinazopelekwa mbele ya bunge (bills) lazima kwanza zichunguzwe kwanza kama zinakiuka katiba, sheria na haki anasisitiza jaji mstaafu B.A Samatta na kusisitiza kila mmoja ktk ngazi za maamuzi wasisitize haki ikiwemo maDC, maRC n.k maana nikusikiliza radio au kutazama TV amri wanazotoa watendaji zingine zina kukakasi mkubwa anamalizia jaji mstaafu B. A Samatta almaarufu "B.A.S" anavyojulikana na washikaji wenzie wa karibu.
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa Mary Chatanda amemshukia vikali Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe kwa kile alichokieleza kuwa amekosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alimtoa gerezani alikokaa kwa muda mrefu tangu kipindi cha utawala wa serikali ya awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Dkt.John Pombe Magufuli

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara Mkoani Lindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara zake kwenye mikoa ya Kusini mwa Tanzania Chatanda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM amesema, hivi karibuni Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amekuwa akimtukana Rais Samia kwa kueleza kuwa ameuza nchi jambo ambalo halina usahihi na linachonganisha Wananchi, hivyo kutoa wito kwa Wananchi hao kuwapuuza na kutowasikiliza pale watakapoitisha mikutano yao

"...anazungumza, anamtukata, anasema ameuza nchi, kwani sisi tumeuzwa hapa tulipokaa?, Kuna mtu anayesema kuwa nimeshawanunua ninyi ni watu wangu?, Wakija msiwasikilize.., anasema anaenda kujiandaa mikutano 70..."

Ameendelea kueleza kuwa kinachotokea kwa Mbowe sasa inawezekana ameathirika kisaikolojia baada ya kuwa jela kwa muda mrefu hivyo alipaswa kutulia kwakuwa jela kuna mambo mengi.

Chanzo: Jambo TV
Naamini huyo M/Kiti wa UWCCM anasoma JF. Namshauri, yeye na viongozi wenzake CCM, wajikite kujibu hoja za wanaopinga baadhi ya vifungu vya makubaliano ya ushirikiano (IGA) kuhusu uendeshaji bandari, badala ya kushambulia watu.

Akili ndogo huzungumzia/hujadili watu
 
Makada wa CCM baadhi yao wamenogewa na udhalimu na kutaka haki isiwepo nchini. Matamshi ya kiongozi huyu mkongwe kada wa chama dola CCM yanaakisi mioyo yao migumu ya kutotaka kubadilika haki iwepo nchini Tanzania kwa raia wote bila ubaguzi wa kiitikadi, chama au kanda n.k
 
1689585025659.png

Nimeingia katika nyaraka za kijiditali na kukutana na ushauri huu kwa mwenyekiti wa CCM taifa ambaye pia ni rais wa Jamhuri ya Muungano kuwa nchi hii ni ngumu kuna makada kama Mary Chatanda wengi sana

Jenerali Ulimwengu - Mh. Rais Samia nchi hii ngumu

Naamini huyo M/Kiti wa UWCCM anasoma JF. Namshauri, yeye na viongozi wenzake CCM, wajikite kujibu hoja za wanaopinga baadhi ya vifungu vya makubaliano ya ushirikiano (IGA) kuhusu uendeshaji bandari, badala ya kushambulia watu.

Akili ndogo huzungumzia/hujadili watu
Hawana Cha kujibu, wanamshambulia personally
 
Tupo kamili gado mwana, tunawazoom tu. Sisi ndiyo chama la nguvu. Kengeza wenu ni kichaa kabisa
Na kweli ni chama la nguvu za dola. Chama kina miaka 50+ kisha hakina uwezo wa kupambana kisiasa zaidi ya kutegemea vyombo vya dola!
 
Mbowe gaidi linapaswa lihukumiwe kunyongwa mpaka kufa kabisa na mzoga wake upewe fisi wa hai. Mpaka siku atakapoomba msamaha juu ya dhihaka yake kwa Dkt Magufuli he will never settle huyu kengeza mpuuzi
Shetani yoyote lazima adhihakiwe.
 
Shukrani gani wakati huyo samia wenu anauza bandari? Kum*m*ke watu wengine sijui wanatumia Makal*o kufikir?
 
Back
Top Bottom