ameathirika kisaikolojia baada ya kuwa jela kwa muda mrefu hivyo alipaswa kutulia kwakuwa jela kuna mambo mengi
Jaji mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande akiwasilisha ripoti kuhusu mfumo wa haki jinai ikulu, mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisisitiza kuwa
mindset fikra za tufanye kazi za haki jinai kwa mazoea ibadilike.
Sasa huyu mwenyekiti wa taifa UWT, Mary Chatanda kada wa CCM bado ana mabaki ya kulilia mfumo wa haki jinai mbovu uendelee kutesa raia wasio na hatia. Kweli ni ngumu CCM na viongozi wake wengi kubadilika. Maneno ya mheshimiwa rais Samia yalinukuliwa pia na gazeti la serikali la Daily News ukurasa wa kwanza
DailyNews.co.tz : Justice dispensation : We must change mindset - Samia
1 day ago — “I support the suggestion of the Chairman of the Commission, retired Judge Mohamed Othman Chande and Chief Justice
15 July 2023
Ripoti ya Tume ya Haki Jinai
Hotuba ya Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai akiwasilisha taarifa rasmi ya Tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai hapa Nchin
TOKA MAKTABA:
Wakiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu leo wametoa ripoti nzuri.
Hawamungunyi maneno na baadhi yao walipata kuyasema haya haya mbele ya Rais John Pombe Joseph Magufuli na leo 2023 kupitia ripoti kamili wanarudia mbele ya mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan.
Serikali iifanyie kazi haraka ripoti hii, kutengeneza framework ya utekelezaji wa mapendekezo haya na kupeleka muswaada wa dharura bungeni sheria kusapoti haya mapendekezo ili wale wote walio ktk kamati za ulinzi na usalama kuanzia ma- DC, wanasiasa na polisi wapewe vijitabu vikae ktk meza ofisini kwao na pia wakati wa vikao vyao vya ulinzi na usalama wavibebe.
Rais wa awamu ya tano Rais John Pombe Magufuli mwaka 2018 wazee hawa walimwambia '
live' mapungufu haya lakini hayakufanyiwa kazi awamu ya 5 ya serikali ya CCM.
Leo hii tena baadhi ya wazee haohao 2023 wamepata nafasi nyingine wamefika ikulu wanamuambia mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan mambo yaleyale.
Ni matumaini sasa ni wakati wa kutekeleza mapendekezo haya muhimu kwani serikali inaongozwa na chama kilekile, ilani ile ile na viongozi walewale wa kisiasa na kiserikali na wa mfumo wa utumishi katika taasisi za haki jamii waliokuwepo mwaka
2018 na leo bado wapo ktk utumishi mwaka
2023.
Kutoka maktaba:
Ni kweli kabisa mfumo wa Haki Jamii na taasisi zake nyingi haupo huru
Mfumo wa Haki Jamii unapaswa sasa kuanza kuacha kutumiwa na dola, ili ufanye kazi kwa haki ndiyo utakuwa mfumo Haki Jamii unaosimamia sheria na katiba bila kupokea amri toka mhimili wa executive (wanasiasa / serikali)
Kwa mfano Jaji Mkuu mstaafu jaji Barnabas A . Samatta ameandika kitabu kinachogusa sehemu ya mfumo wa haki jamii kuhusu uhuru wa mahakama na hakika inatakiwa raia wote ikiwemo jaji mkuu aliyepo ofisini, majaji, mahakimu kukisoma na kuwa rejea kuhusu umuhimu wa mhimili wa Mahakama katika nchi hususan yetu ya Tanzania
Barnabas A. Samatta, Jaji Barnabas A. Samatta, alikuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kutoka 2000 hadi 2007. Huko nyuma, 1984-1987, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe. Yeye ni mjumbe mwanzilishi wa Judicial Integrity Group (Kikundi cha Uadilifu wa Mahakama), chombo huru cha cha kimataifa kinacho jishughulisha na ukuzaji wa uadilifu wa mahakama duniani na ambacho kilitunga Kanuni za Bangalore za Mwenendo wa Mahakama. Kwa wakati huu, yeye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Bodi ya Kampuni ya Earth, Energy and Environment Mediation Limited yenye makao makuu yake London, Uingereza, ambayo inashughulikia njia bora za kuzuia au kutatua migogoro barani Afrika inayohusiana na ardhi, mafuta, madini, maji au mazingira. Vilevile, Jaji Samatta ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe. Katika baadhi ya hukumu, makala na hotuba zake amesisitiza sana juu ya umuhimu wa uhuru wa mahakama, usawa mbele ya sheria na upatikanaji wa haki kwa unafuu na wepesi kwa kila mtu katika jamii. Katika kitabu hiki, anazungumzia kwa ufasaha, lakini kwa lugha nyepesi kuelewa, na kwa namna isiyomchosha msomaji, masuala mengi muhimu sana katika uwanja wa utoaji wa haki. Miongoni mwake ni uhuru wa mahakama; rushwa; ugumu wa kazi na maisha ya jaji; mikwaruzano baina ya mihimili ya dola na utumiaji wa kiuonevu wa mamlaka ya dola. Hiki ni kitabu kwa mwanasheria na kwa mlei. Ni kitabu kwa mtawala na mtawaliwa. Kwa kweli, ni kitabu kwa kila mtu.
5 July 2018
Ikulu mbele ya John Pombe Magufuli
Umuhimu wa utawala wa sheria - Jaji Barnabas A. Samatta
Sheria zinazopelekwa mbele ya bunge (bills) lazima kwanza zichunguzwe kwanza kama zinakiuka katiba, sheria na haki anasisitiza jaji mstaafu B.A Samatta na kusisitiza kila mmoja ktk ngazi za maamuzi wasisitize haki ikiwemo maDC, maRC n.k maana nikusikiliza radio au kutazama TV amri wanazotoa watendaji zingine zina kukakasi mkubwa anamalizia jaji mstaafu B. A Samatta almaarufu "B.A.S" anavyojulikana na washikaji wenzie wa karibu.