PostGE2025 Mauaji ya 29/10 yamebadilisha sana maisha ya Samia sio yule wa 2024

PostGE2025 Mauaji ya 29/10 yamebadilisha sana maisha ya Samia sio yule wa 2024

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Na mwezi huu wa 10 tarehe 29 tunakiamusha tena sisi Gen Z hadi tufanikishe jambo letu la ukombozi wa Tanganyika na kumwadabisha huyu mmama.
Kiamsheni tu!
Ila kwa taarifa ni kwamba October mwaka jana polisi hawakumaliza akiba yao ya risasi.
Bado wanazo risasi za kutosha tu hata mkija wengi mara kumi ya wale waliotoka mwaka jana bado risasi za kuwatosha zipo kwahiyo namna mtakavyokuja ndivyo polisi watakavyowapokea!.
 
MAUAJI YA KIDINI YALIYO FANYWA NA CCM OCT29 NA MENGINEYO CHINI YA SAMIA ni ngumu kujisafisha ni lazima yatasafishwa kwa damu zao hivyo wanaishi kwa hofu kuu ....tena wana muda mchache sana ..vinginevyo Samia afanye kama Museven kujibakisha madarakani yeye na familia yake ... SAMIA NA WAHALIFU WENZIE WAMEBAKISHA MIEZI 18 TU KUTOKA SASA ,WATAANZA KUCHANGANYIKIWA KWA HOFU NA INAWEZA KUWAPELEKEA KUMWAGA DAMU ZAIDI..ILA MWISHO WAO NI MBAYA NA MBOVU.
DUA LA KUKU HALIMSHIKI MWEWE.
Samia ataendelea kulitumikia taifa la Tanzania kulingana na matakwa ya katiba .
Na muda wake wa kustaafu ukifika atastaafu kwa heshima kama walivyostaafu Marais waliomtangulia.
 
Awamu hii hatushindwi.Nguvu ya umma lazima ishinde maana ni nguvu ya Mungu.Shetani lazima tumshinde.
Ile ya October mwaka jana ilikuwa nguvu ya nani?
Ilikuwa Nguvu ya soda au nguvu ya shetani ndio maana mkachezea mikwaju ya polisi na JWTZ?!
 
Hasara ni kwa familia yako, by the way huna cha kupoteza huna wanaokutegemea nenda kajitowe sadaka tu.
Acha kabisa kutishia watanzania wanaodai haki. Wewe unaonekana ni jitu zima lakini akili zako ni kama za mtoto mdogo.
 
Kwani mauaji ya Rwanda yanavyo itwa mauaji ka kibabila waliokufa ni wakabila moja ‽ tumia akili wacha kutumia kijambio kufikili..wewe unadhani hiyo oct29 kwa sababu gani Risasi za moto tu ndiyo zilitumika hakuna risasi za plastiki zilizo tumika tofauti na kanuni za kutuliza gasia ... kanuni za kutuliza gasia zinaeleza kuwa njia salama zinatakiwa kutumika kwanza kabla ya kutumia njia hatari pale tu njia salama zinapo zidiwa nguvu ..ila oct29 ni RISASI ZA MOTO TU NDIYO ZILITUMIKA.
Mimi nawapongeza sana polisi na JWTZ kwa kile walichokifanya October mwaka jana!
Wasingechukua hatua mapema nchi ingeharibika kutokana na genge la magaidi lilokuwa limeingia mitaani likipora mali katika maduka na kuchoma moto mali za raia wasiokuwa na hatia.
Kiukweli vyombo vya ulinzi na usalama vilichukua hatua sahihi na hata hivyo ukiangalia vurugu na uharibifu wa mali uliofanyika utakubali kwamba watu waliouawa ni wachache sana. Yaani 518 tu?
Inatakiwa vurugu zikitokea vifo viongezeke angalau wafe watu 1000+.
 
Ukimuua hata mjusi roho na nafsi inakusuta kwamba uenda ya kua huyu mjusi ana watoto wanaomsubiria awapelekee chakula sasa nimemuua wale watoto wake wataishije? sio kwamba nimemkosea Mungu ngoja nikatubu maana imeandikwa usiue na haijaandikwa usiue nini ila usiue maana haukuwahi kuumba wewe
Kwahiyo watu wanaochinja ng'ombe,mbuzi,kondoo na KUKU wanapata dhambi eti kwasababu imeandikwa "USIUE?!"
Mara ngapi kila siku tunaambiwa polisi wameua watu "wanaosadikiwa kuwa ni majambazi" na hatulalamiki?!
Ukiona nyoka anaingia ndani mwako umwache tu kisa imeandikwa "USIUE?!
Hiyo ni akili ya namna gani?!
 
Tumpe muda, i think ni majonzi mengi yanayomkabiri kuanzia vifo vya watu 518 kwa mujibu wa report ya tume ya jaji chande, Kifo cha rafiki yake aliekuwa mbunge, kifo cha mume wake, kifo cha rafiki mfanyabiashara or anything else "Chivayo". Kwa kweli yuko na majonzi sana Tumpe muda wa kutosha.
 
Mimi nawapongeza sana polisi na JWTZ kwa kile walichokifanya October mwaka jana!
Wasingechukua hatua mapema nchi ingeharibika kutokana na genge la magaidi lilokuwa limeingia mitaani likipora mali katika maduka na kuchoma moto mali za raia wasiokuwa na hatia.
Kiukweli vyombo vya ulinzi na usalama vilichukua hatua sahihi na hata hivyo ukiangalia vurugu na uharibifu wa mali uliofanyika utakubali kwamba watu waliouawa ni wachache sana. Yaani 518 tu?
Inatakiwa vurugu zikitokea vifo viongezeke angalau wafe watu 1000+.
Siku ukijua kuwa samia ana waogopa hao hao jwtz na polisi ndiyo utskuwa umeanza kupata akili...maana ni swala la myda tu
 

Attachments

  • IMG-20261007-WA7872.jpg
    IMG-20261007-WA7872.jpg
    182.1 KB · Views: 8
Samia alikuwa mcheshi mtu wa watu, mtu wa kuonekana hadharani mara kwa mara.

Alikuwa ni mtu wa safari za ndani na za nje, Oman Dubai ilikuwa sebleni kwake, alizunguka mikoani kutembelea na kuwasalimia wananchi.

Alipenda mikutano, alionekana akizunguka kukagua na kuzindua miradi hadi CHADEMA na Wanaharakati wakasema 'Mama anaupiga mwingi'.

Tulishuhudia akicheza mziki wa taarabu na wananchi wake sehemu mbalimbali.

Leo amekuwa kama kakakuona, anaonekana kwa nadra sana, life style has changed.

Hata akifanya safari anafanya kwa kujificha ficha, nasikia jana alikuwa Harare Watanzania tumefichwa.

Nimeamini kweli damu ya mtu ni mzigo, ile nuru aliyokuwa nayo kabla ya 29/10 imetoweka kama mawingu ya el nino.
GWaji boy alisema wakampuuza
 
Tatizo ccm hawataki kukubali ukweli
 

Attachments

  • HTPQvGJXwAIYLze.jpg
    HTPQvGJXwAIYLze.jpg
    75.8 KB · Views: 10
  • FB_IMG_1789866421800.jpg
    FB_IMG_1789866421800.jpg
    11.4 KB · Views: 7
MAUAJI YA KIDINI YALIYO FANYWA NA CCM OCT29 NA MENGINEYO CHINI YA SAMIA ni ngumu kujisafisha ni lazima yatasafishwa kwa damu zao hivyo wanaishi kwa hofu kuu ....tena wana muda mchache sana ..vinginevyo Samia afanye kama Museven kujibakisha madarakani yeye na familia yake ...SAMIA KABAKISHA MIEZI 18 TU KABLA YA YEYE NA WAHALIFU WENZIE KUANZA KUCHANGANYIKIWA KWA HOFU NA MISUKOSUKO INAYE KWENDA KUWAKUTA NA KWA SABABU HIYO UENDA WAKALAZIMIKA KUJARIBU KUZIDI KUMWAGA DAMU ZAIDI ILI KUJINUSURU

..sio mauaji ya kidini.

..ni mauaji yaliyotekelezwa na wachache wenye tamaa za madaraka ya nchi.

..wauwaji hawakuwa wakiangalia dini ya mtu.
 
..sio mauaji ya kidini.

..ni mauaji yaliyotekelezwa na wachache wenye tamaa za madaraka ya nchi.

..wauwaji hawakuwa wakiangalia dini ya mtu.
Tumia akili ni mauaji ya kidini ..ndiyo maana kuna sheikh mmoja alikufa waislamu mashekh walilaani sana kifo cha huyo shekh kuwa laani waandamanaji nq siyo wauaji
 
Samia alikuwa mcheshi mtu wa watu, mtu wa kuonekana hadharani mara kwa mara.

Alikuwa ni mtu wa safari za ndani na za nje, Oman Dubai ilikuwa sebleni kwake, alizunguka mikoani kutembelea na kuwasalimia wananchi.

Alipenda mikutano, alionekana akizunguka kukagua na kuzindua miradi hadi CHADEMA na Wanaharakati wakasema 'Mama anaupiga mwingi'.

Tulishuhudia akicheza mziki wa taarabu na wananchi wake sehemu mbalimbali.

Leo amekuwa kama kakakuona, anaonekana kwa nadra sana, life style has changed.

Hata akifanya safari anafanya kwa kujificha ficha, nasikia jana alikuwa Harare Watanzania tumefichwa.

Nimeamini kweli damu ya mtu ni mzigo, ile nuru aliyokuwa nayo kabla ya 29/10 imetoweka kama mawingu ya el nino.
Mbona akiwa anahutubia kwao Kizimkazi huwa anaonekana kuwa na tabasamu lenye bashasha sana?
 
Nyie mmeua wangapi kila uchaguzi mkuu Pemba na Unguja?
Toka mfumo wa uchaguzi wa vyama vingi,hakuna hata uchaguzi ambao ulipita bila kuua wazanzibar, isipokuwa 2025!

Maumivu mnayopitia sahivi,upande wa pili walipitia kila uchaguzi.

..wanaouwa ni Ccm, na ndani yake kuna Wazanzibari, na Watanganyika.

..Walitangulia kuuwawa Wazanzibari kwasababu kipindi hicho chama kilichokuwa na nguvu kilikuwa Cuf na kilikuwa kinatishia ugali wa Ccm Zanzibar.

..Watanganyika tulichelewa kuuwawa kwa wingi kwasababu kwa kipindi kirefu hakukuwa na chama kinachotishia kuipokonya Ccm madaraka huku Tanganyika.

..Watanganyika na Wazanzibari tunapaswa kuungana dhidi ya Ccm.
 
Samia alikuwa mcheshi mtu wa watu, mtu wa kuonekana hadharani mara kwa mara.

Alikuwa ni mtu wa safari za ndani na za nje, Oman Dubai ilikuwa sebleni kwake, alizunguka mikoani kutembelea na kuwasalimia wananchi.

Alipenda mikutano, alionekana akizunguka kukagua na kuzindua miradi hadi CHADEMA na Wanaharakati wakasema 'Mama anaupiga mwingi'.

Tulishuhudia akicheza mziki wa taarabu na wananchi wake sehemu mbalimbali.

Leo amekuwa kama kakakuona, anaonekana kwa nadra sana, life style has changed.

Hata akifanya safari anafanya kwa kujificha ficha, nasikia jana alikuwa Harare Watanzania tumefichwa.

Nimeamini kweli damu ya mtu ni mzigo, ile nuru aliyokuwa nayo kabla ya 29/10 imetoweka kama mawingu ya el nino.
Hata sijui kwa nini umeona ni vizuri kumpamba kama ulivyofanya hapa!
Kama alikuchota akili kwa uigizaji wake mzuri, ingefaa ueleze hivyo waziwazi kuliko kumfanya mtu mwovu kama huyu aoinekane kuwa kabadilika tu ghafla bila ya sababu zozote.

Samia ni mwanasanaa aliyekubuhu, ambaye ndani yake hana chembe hata ndogo ya hayo mazuri unayojaribu kumpamba nayo.
Kule kupapasa mito ya kitandani hospitalini alikolazwa Tundu Lissu Nairobi; inabidi picha hiyo uiweke sambamba na hii ya kuwaambia wazazi walioruhusu watoto wao kwenda kuuliwa na serikali yake; au na Tundu Lissu huyo huyo ambaye kamweka gerezani zaidi ya mwaka sasa kwa kesi anayojuwa ni ya kutunga tu!

Hii mada yako ya kujajaribu kumpamba mtu ambaye hastahiri inasikitisha sana; pamoja na kwamba inajulikana kuwa nia ya mada ni kuonyesha mhusika alivyo mwovu.

Usanii wa Samia ulijulikana toka wakati anavutana na Mbowe gerezani na kumburuza hadi Ikulu!
Tundu Lissu na wengine wote waliosoma usanii huo toka mwanzo hawawezi kukubaliana na mapambo haya unayomvalisha mtu mwovu huyu.
 
Back
Top Bottom