Mbarali: Dogo aliyepanda juu ya mti ili kumuona Tundu Lissu apewa zawadi ya vifaa vya shule

Mbarali: Dogo aliyepanda juu ya mti ili kumuona Tundu Lissu apewa zawadi ya vifaa vya shule

Ama hakika kutoa ni moyo , makamanda wa Mbarali wamemkabidhi madaftari na vifaa vingine vya shule bwana mdogo aliyelazimika kupanda juu ya mti ili kushuhudia Tundu Lissu akimwaga sera jukwaani .

Unaweza kuona kama ni jambo dogo lakini ni jambo linalofikirisha mno !

View attachment 1572209View attachment 1572210

Unaweza kumsikiliza dogo hapa akihojiwa na vyombo vya habari vya kimataifa
Kweli kutoa ni Moyo

Kumtangaza ulie msaidia ni masimango

Watoto kwenda kwenye kampeni za CCM wanaitwa watoto wakienda chadema wanaitwa mashujaa

Tutunze ndimi zetu tufikiri ukurasa ujayo
 
Kweli kutoa ni Moyo

Kumtangaza ulie msaidia ni masimango

Watoto kwenda kwenye kampeni za CCM wanaitwa watoto wakienda chadema wanaitwa mashujaa

Tutunze ndimi zetu tufikiri ukurasa ujayo
Huyu hatujamsaidia , kwanza hakuwa na uhaba wa vifaa hivyo na wala hakuomba msaada popote , huyu kapewa zawadi na makamanda wenzie wa Mbarali , kama ungeangalia video iliyoambatanishwa usingemfananisha na watoto wa kanda ya ziwa ambako shule hufungwa na watoto hulazimishwa kujaza uwanja
 
Huyu hatujamsaidia , kwanza hakuwa na uhaba wa vifaa hivyo na walavhakuomba msaada popote , huyu kapewa na makamanda wenzie wa Mbarali , kama ungeangalia video iliyoambatanishwa usingemfananisha na watoto wa kanda ya ziwa ambako shule hufungwa na watoto hulazimishwa kujaza uwanja
Mkuu unajua kujitetea

Swala ni matumiz ya watoto kwenye kampen
 
muda si mrefu itatangazwa wanafunzI wasiende kwenye kampeni
 
Chadema mnasema maendeleo sio vitu kwenye sera yenu kwa nini mumempa vitu yaani madaftari na peni huyo mtoto?

Mwangalieni usoni dogo anavyowashangaa!! mbona mnasema maendeleo sio vitu halafu mnanipa vitu? Dogo anaonyesha wazi kachukia na hawaelewi Chadema anauliza nini hiki mlichonipa mkononi wakati mnasema maendeleo sio vitu na nimemsikia mimi mwenyewe Lisu akiongea nilipokuwa juu pale penye mti? Mbona siwaelewi?

View attachment 1572220
Mkuu umeitoa hii picha vizuri kweli kweli ngoja niisevu kabisa!

Lissu rais kipenzi cha watanzania.
 
So what? Kuna watu walishawahi panda juu ya nguzo za umeme tena zile nguzo za umeme wa njia kuu ili kumuona Magufuli lakini haikuwa habari ,sasa hii ndo nini?
 
What a double standard. Si mnasema watoto wabaki shule kujisomea na sio kuhudhuria mikutano ya kisiasa Kama wanavyosombwa na ccm? Nilifikiri mngemchapa viboko ati.
Huyo njia aliyotumia ndo imeleta hamasa alitoka shule kwenda home wkt anarud home akapita mkutanoni tukamfukuza aende home Dogo akazuga anaenda kumbe akaenda kupanda juu ya mti kusikiliza madini ya mh lissu
 
Ama hakika kutoa ni moyo , makamanda wa Mbarali wamemkabidhi madaftari na vifaa vingine vya shule bwana mdogo aliyelazimika kupanda juu ya mti ili kushuhudia Tundu Lissu akimwaga sera jukwaani .

Unaweza kuona kama ni jambo dogo lakini ni jambo linalofikirisha mno !

View attachment 1572209View attachment 1572210

Unaweza kumsikiliza dogo hapa akihojiwa na vyombo vya habari vya kimataifa
Mbona anaonekana kujua mambo mengi kuzidi unri wake
 
Huyo dogo alitakiwa achapwe viboko na makamanda maana hawataki watoto kwenye mikutano yao ya kampeini, hapo sasa ndio utajua CHADEMA imejaa double standard ! Ndio maana tunaojitambua tunasema ni CCM mbele kwa mbele.
 
Hakuna kitu kama hicho huyo ameandaliwa mapema kama yule aliyetoa mikeka na kuku, ni maigizo ya nyumbu mbugani.
Wacha upumbavu wewe, huyo mtoto kasema mwenyewe kuwa alienda hapo mkutanoni baada ya shule kuwaruhusu kwenda kula chakula cha mchana.

Yeye badala ya kwenda kula akaamua kwenda kumuona rais wake.
 
Kama mnakumbuka kisa cha Zakayo mtoza ushuru aliyepanda juu ya mti ili Yesu atakapopita aweze kumwona mtagundua kuna mfanano fulani.
 
Huyu mtoto anaakisi maisha yetu tulipotoka, wengi tuliotoka vijijini tulikuwa hivi.
nakumbuka kampeni ya mwaka 1995 tulilikimbiza gari la nccr mageuzi mvua ikatupiga kisawa sawa
Kabla ya mamvi Edo, alikuwepo Mwenye neema, mzee wa NJI HII, gari haliwashwi linasukumwa...1995

Daah umenikumbusha mbali sana!

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Back
Top Bottom