Mbezi beach, Dar: Jimson Kibiki, apigwa risasi na Majambazi wakati akitoka benki kuchukua hela, wamnyang'anya Mil 4

Mbezi beach, Dar: Jimson Kibiki, apigwa risasi na Majambazi wakati akitoka benki kuchukua hela, wamnyang'anya Mil 4

Daaah kweli mkuu,kauli zake zilikuwa hazIna masihara, nakumbuka aliwahi kuongea mara moja tu kuhusu utekaji wa magari pori la nyakanazi (watumiaji wa barabara hiyo wanapajua)watu walikuwa wanatekwa sana,wanavuliwa nguo zote wanaanza kuimbishwa "mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe"jamaa alisema raia wanaishi kwa hofu ndani ya nchi yao wenyewe wakati polisi wapo Jw wapo inakuwaje eneo linajulikana kuna majambazi wanatamba tu hawakamatwi,hataki huo ujinga!!ikafanyika operation watekaji wakapotea,sasa kwa hali inavyoendelea watu wanapita kwa hofu kwenye lile pori!!!! MAMA NI KIONGOZI MZURI LAKINI AKAZE SAUTI.
mkuu tutaona na kusikia mengi tu. nchi hii kuiongoza s rahisi kama watu wanavyofikiria. JPM aliiweza vizr.
 
Kuuawa huyo mdingi au ujambazi unamuingizaje Magufuli katika hii mada? Maana naona watu tutamkumbuka tutamkumbuka! Acheni ushamba

Au ishu hizo kuna kipindi zinasimama kabisa zisijitokeze hata siku moja kiasi kwamba ikija kutokea iwe gumzo kiasi hiki

Au...!!!?
Utajua hujui

Sent from my DUB-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Dawa yao ni kuwapa wale vyuma tu....Halafu katika zama hizi bado watu wanashindwa kutumia technology kufanya manunuzi? Haina haja ya kwenda bank kuchukua mzigo mkubwa ,wa nini? Kama unaenda kununua kiwanja,gari or malipo yeyote si unafanya bank transfer? Kama vimilioni viwili au vitatu si unatransfer tu kwenda kwenye mobile? Usiangalie gharama jali uhai.
Labda aikuwa anaenda kuwalipa Mafundi/vibarua.
 
comment ya hovyo haijawah kutokea. mtu alipe kodi ya usalama na ulinzi alafu alipe askari kwa ulinzi mwengine. inaonekana hata haki zako huzijui wew

Sasa unata kuniambia kama nimetoka bank posta kuchukua hela naenda kongowe kununua kiwanja ,njia nayopita askari wawe barabarani wamejipanga kwa mstari hadi Kongowe? Unajua ratio ya askari mmoja ni raia wangapi? Swala la ujambazi alimalizwi kwa njia kama unazofikiria wewe...Ujambazi ni mtandao,njia unazosema wewe askari wa kulinda labda kumaliza VIBAKA.
 
Kidogo inaanza kutia wasiwasi.

Ni kama mama hakuwemo kwenye serikali iliyokuwa imeyadhibiti haya mambo, na sasa ni kama anatafuta njia zake mpya kabisa kwa kila kitu, jambo ambalo inaonekana inamchukua muda mrefu na kutoa mwanya kwa watu kujifanyia yao.

Hivi polisi nao wamebadili utendaji kazi wao uliokuwa umedhibiti uhalifu wa aina

Samia atalinganishwa na mtangulizi wake katika baadhi ya mambo, na ataonekana hatoshi kabisa!
Hakika! ataonekana hatoshi. Sasa hivi zile foleni za kijinga zimeanza kuonekana jijini Dar es Salaam.. sijui tunaelekea wapi!
 
RIP anko tutakumiss sana tu haya mambo yalishaisha sasa yanaanza kurudi
Ndiyo hasara ya kumtegemea mtu mmoja kama mganga wa mvua wa kijiji. Suluhisho ni kujenga MIFUMO imara ya utawala itakayohimili mabadiliko yoyote yale iwe ya uongozi wa mtu au chama kilichoko madarakani.
Nchi za wenzetu zilizoendelea huwezi kuona utendaji wa jeshi la polisi unafifia kisa tu rais wa nchi amebadilika au chama kilichokuwa kinatawala hakipo tena madarakani.
Kama ni kweli matukio haya yana tokea awamu hii simply because kuna mabadiliko ya uongozi basi ni dhahiri tuna mfumo mbovu sana wa utawala kupindukia. QED.
 
Acha ujinga wewe mfumo gani umekosekasekana sasa?
 
Back
Top Bottom