Polisi Dar es salaam imetangaza msako mkali wa Majambazi waliosababisha kifo cha Kijana Jimson Kibiki baada ya kumpiga risasi wakiwa kwenye purukushani za kumpora pesa maeneo ya Mbezi Beach.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM Camilius Wambura amesema "tukio lilitokea jana saa saba na nusu mchana alikua ametoka Benki Mikocheni alikochukua kama milioni 8 akaelekea kwenye Benki nyingine Afrikana nafikiri kulikua na matatizo ya kibenki pale kwahiyo akatoka kuelekea nyumbani maeneo ya Juliana"
"Alikua ana milioni nne kwenye mifuko yake ya suruali na milioni nne nyingine kwenye bahasha ndipo alipokutana na hilo tatizo, Watu hao wadhaniwao kuwa Majambazi walimpiga risasi tumboni, akapelekwa Hospitali Mbezi beach kwa huduma ya kwanza baadae Muhimbili ndiko alikofariki"
"Wale ni Watu ambao wameua, lile ni tukio la mauaji.. taarifa ya Polisi ni kwamba tuko mbioni kuwatafuta na kuhakikisha tumewapata na kuchukua hatua za kisheria dhidi yao, kwenye tukio hilo walichukua milioni 4 na kuondoka nazo"