Rais mama mh. mama Samia awe mkali sana sana. Na pia Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wamsaidie sana mana akicheza yataibuka makundi ya uhalifu kama enzi za awamu ya Tatu na IGP wake mzee wa ngunguri. Uhalifu wa kupora fesha taslmu kwenye baadhi ya nchi za ulimwengu wa tatu huo ni mtaji mkubwa sana kwa watendaji wa vyombo vya ulinzi wasio waaminifu , watu wanapora halfu wanagawana na wasimamiaji wa sheria . Inakua kama kamradi ka kupata pesa haramu. Na pia magenge ya wahalifu wakitajirika wanageuka kuwa wafadhili wa vyombo vya kusimamia sheria na kujifanya kuwa marafiki wema wa kufadhili au kuviwezesha .
Tujiulize Waliodhibiti ujambazi kwa miaka mi tano ya awamu ya Tano ni wale wale leo awamu ya Sita kwa nini waibuke mapema wakati jeshi ni lile lile . Je , ni hujuma au ni kupuuza kuwa hakuna wa kuwatisha tena?
Lakini pia Waziri wa Mambo ya ndani ana kauli za kuchanganya jamii na kuona kuwa Jeahi lake halina weledi wa kupambana na wavunja sheria zaidi ya uonevu. Waziri awe karibu na wahanga wa kupambana na uhalifu ambao wanajitoa kwa mishahara midogo badala ya kukaa na wale waliojifungia ofisini na kuchonga madili yao.
Mzee Siro amejitahidi sana awamu ya Tano kutokomeza uhalifu.
Uhalifu mkubwa hua unakua na wafadhili nyuma. Watafutwe na kutangulizwa mbele mapema kabla. Kuna miji iliyokua imejaa majambazi watupu kama Arusha,Moshi, Mbeya na Mwanza na watendaji wa vyombo vya dola wakifanyia kazi huko walikua wanatajirika haraka sana ,sijui huko kuna mishahara zaidi au ni ukaribu wao a wahalifu wanaojivika ngozi ya kondoo. !!
Namkubali sana Ahmed Msangi aliyekua upelelezi Morogoro Enzi hizo kwa sasa sijui yupo wapi ila anafaa kumrithi Siro. Huyu hanaga simile na majbazi.
Watanzania wote tuwakatae kabisa wahalifu kuanzia wavunjaji ,waporaji mpaka majambazi. Hawa kwa kweli wanaleta hofu kubwa kwenye jamii.
Lakini pia kuna wale wafanyabiashara haramu wasiopenda ushindani , hasa Arusha na Moshi wapo nao ni tatizo sana mana akiibuka mtu kibiashara hua wanamtumia majambazi , hawa nao wasiachwe wasakwe watangulizwe haraka haraka.
Uchumi mzuri utaendana na kutokomeza wahalifu wote.
Piga chuma majambazi yote na vibaka wote piga gesi.