Mbezi beach, Dar: Jimson Kibiki, apigwa risasi na Majambazi wakati akitoka benki kuchukua hela, wamnyang'anya Mil 4

Mbezi beach, Dar: Jimson Kibiki, apigwa risasi na Majambazi wakati akitoka benki kuchukua hela, wamnyang'anya Mil 4

Watu si mlitaka Uhuru wa kufanya kazi bila bugdha.?.
Sasa hivi na majambazi nao wamepewa Uhuru wa kufanya kazi zao.
Nadhani soon mzunguko wa Ela utaongezeka mtaani kwa Uhuru tuliopewa.

Si mwenyewe raisi alisema ataweka mazingira mazuri kwa wawekezaji? Wawekezaji ndo wameanza kazi zao sasa... huyu Mama aliingia na gear mbaya sana , na itamcost, c alikua anajifanya anaruhusu kila kitu , leo Tz nzima inamlilia magufuli , hata waliomchukia wameanza kumkumbuka
 
Kuuawa huyo mdingi au ujambazi unamuingizaje Magufuli katika hii mada? Maana naona watu tutamkumbuka tutamkumbuka! Acheni ushamba

Au ishu hizo kuna kipindi zinasimama kabisa zisijitokeze hata siku moja kiasi kwamba ikija kutokea iwe gumzo kiasi hiki

Au...!!!?

Unakasirika nini wakati huo ndo ukweli magufuli ameshaanza kukumbukwa hadi na wale wasiompenda kwan ni siri?
 
mkuu, JPM kauli zake tu majukwaani zilikuwa zinatisha. samia anapoongea na wananchi zile kauli hana. mfano kuhusu hili la ujambazi JPM aliongea live kuwaambia askari kwanini jambazi anapora na silaha alafu anafanikiwa kukimbia, kwanini msiwanyang'anye hizo silaha ' haraka haraka' tena neno haraka haraka akalirudia kama mara 3 hivi. alimaamisha jambaz lazima afe. sasa kama ww ni jambazi ukisikia hii kauli rais anaiongea live lazima uogope. kama tunahitaji kusikia maneno matamu kila siku haya ndio madhara. kauli za JPM ndio zilikuwa zinatulinda

Apumzike kwa amani Baba yetu , tutamkumbuka Daima
 
Yaani hata kudhibiti majambazi nalo nimekuwa kero kwa serikali hii
Mengi yamebadilika ila hili la ujambazi wangeshikilia pale pale kama ni kuuwawa wauwawe tu maana matukio yalipungua sana na kuyasahau

Hii thread leo imenifuraisha kuliko zote , Magu alikua jembe bwana , hakuna wa kuifuta legacy yake, apumzike kwa amani
 
Kidogo inaanza kutia wasiwasi.

Ni kama mama hakuwemo kwenye serikali iliyokuwa imeyadhibiti haya mambo, na sasa ni kama anatafuta njia zake mpya kabisa kwa kila kitu, jambo ambalo inaonekana inamchukua muda mrefu na kutoa mwanya kwa watu kujifanyia yao.

Hivi polisi nao wamebadili utendaji kazi wao uliokuwa umedhibiti uhalifu wa aina

Samia atalinganishwa na mtangulizi wake katika baadhi ya mambo, na ataonekana hatoshi kabisa!
Ni ujinga wa hali ya juu kwa kufariki mtu mmoja, serikali nzima inapoteza muelekeo. Igp ni yuleyule, na karibu kila nafasi inaendeshwa na watu wale wale, aliyefariki ni rais, inakuwa aje mambo ya kijinga yanaanza kuibuka kila upande?
Matatizo ya kuthamini mtu badala ya mfumo.
 
Kuna banker kauza ramani.

Mkuu Sio kazima Awe Banker wajumuishe pia Marafiki zake ...Kama Kuna Biashara kafanya au Kuna Mtu alikuwa anafanya nae au Alienda Kuchukua Hela ili amlipe Mtu fulani ili apate kitu fulani, haya Mambo wanatokanayo Mbali Mkuu...Inawezekana Jamaa walikuwa wanamfuatilia tangu anaingia bank? Hakuna anaejua!Tangu huko alipotoka! Au Mtu wa Mwisho Kuwasiliana nae nk nk!
MUNGU atusaidie haya Mambo
 
Rais mama mh. mama Samia awe mkali sana sana. Na pia Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wamsaidie sana mana akicheza yataibuka makundi ya uhalifu kama enzi za awamu ya Tatu na IGP wake mzee wa ngunguri. Uhalifu wa kupora fesha taslmu kwenye baadhi ya nchi za ulimwengu wa tatu huo ni mtaji mkubwa sana kwa watendaji wa vyombo vya ulinzi wasio waaminifu , watu wanapora halfu wanagawana na wasimamiaji wa sheria . Inakua kama kamradi ka kupata pesa haramu. Na pia magenge ya wahalifu wakitajirika wanageuka kuwa wafadhili wa vyombo vya kusimamia sheria na kujifanya kuwa marafiki wema wa kufadhili au kuviwezesha .
Tujiulize Waliodhibiti ujambazi kwa miaka mi tano ya awamu ya Tano ni wale wale leo awamu ya Sita kwa nini waibuke mapema wakati jeshi ni lile lile . Je , ni hujuma au ni kupuuza kuwa hakuna wa kuwatisha tena?

Lakini pia Waziri wa Mambo ya ndani ana kauli za kuchanganya jamii na kuona kuwa Jeahi lake halina weledi wa kupambana na wavunja sheria zaidi ya uonevu. Waziri awe karibu na wahanga wa kupambana na uhalifu ambao wanajitoa kwa mishahara midogo badala ya kukaa na wale waliojifungia ofisini na kuchonga madili yao.


Mzee Siro amejitahidi sana awamu ya Tano kutokomeza uhalifu.
Uhalifu mkubwa hua unakua na wafadhili nyuma. Watafutwe na kutangulizwa mbele mapema kabla. Kuna miji iliyokua imejaa majambazi watupu kama Arusha,Moshi, Mbeya na Mwanza na watendaji wa vyombo vya dola wakifanyia kazi huko walikua wanatajirika haraka sana ,sijui huko kuna mishahara zaidi au ni ukaribu wao a wahalifu wanaojivika ngozi ya kondoo. !!

Namkubali sana Ahmed Msangi aliyekua upelelezi Morogoro Enzi hizo kwa sasa sijui yupo wapi ila anafaa kumrithi Siro. Huyu hanaga simile na majbazi.

Watanzania wote tuwakatae kabisa wahalifu kuanzia wavunjaji ,waporaji mpaka majambazi. Hawa kwa kweli wanaleta hofu kubwa kwenye jamii.
Lakini pia kuna wale wafanyabiashara haramu wasiopenda ushindani , hasa Arusha na Moshi wapo nao ni tatizo sana mana akiibuka mtu kibiashara hua wanamtumia majambazi , hawa nao wasiachwe wasakwe watangulizwe haraka haraka.
Uchumi mzuri utaendana na kutokomeza wahalifu wote.
Piga chuma majambazi yote na vibaka wote piga gesi.
 
Wewe ndio ufikirie zaidi ya hapo.Mpesa inatoa au kuweka zaidi ya
Acha upopoma wewe mandazi, sio kila jambo hutaka transfer, wewe kwa akili yako unafikiri aliyeuawa hakujua ya kuwa kuna kufanya transfer ?

Just imagin mtu unasherehe labda ya Harusi wanakamati wanataka wakahemee vitu sokoni, madukani n.k transfer unafanyeje hapo ?

Tujaribu kufikiria zaidi ya hapo
5m Ukitaka zaidi unaomba tu wana uplift bado ujani convince hata kidogo.Nimefanya harusi ya 40m na bado sikutoa that amount bank.Pia kwa taarifa yako mimi ni mhasibu nasukuma more than 300m per day through online banking acha ushamba
 
Una maana watu walikuwa wanapigwa risasi na majambazi na kufa, ndugu zao wanakaa kimya na kuzika kimya kimya. Kweli?
Kama wanaripoti lakini hayaandikwi ulitaka waanzishe magazeti yao?
 
Back
Top Bottom