Mbezi beach, Dar: Jimson Kibiki, apigwa risasi na Majambazi wakati akitoka benki kuchukua hela, wamnyang'anya Mil 4

Mbezi beach, Dar: Jimson Kibiki, apigwa risasi na Majambazi wakati akitoka benki kuchukua hela, wamnyang'anya Mil 4

Ni ujinga wa hali ya juu kwa kufariki mtu mmoja, serikali nzima inapoteza muelekeo. Igp ni yuleyule, na karibu kila nafasi inaendeshwa na watu wale wale, aliyefariki ni rais, inakuwa aje mambo ya kijinga yanaanza kuibuka kila upande?
Matatizo ya kuthamini mtu badala ya mfumo.
Hawa watu si walikuwa humo humo na rais huyo?

Hata kama hapakuwa na mfumo, kwani hawawezi kugezea tu waliyokuwa wanafanya mazuri ili yaendelee bila huyo mtu mmoja kuwepo?
 
tulianza kusahau zama hizi! inasikitisha sana. nguvu zote hizi kisa milioni 4!

pole sana kwa wanafamilia!

Si semi kuwa polisi wanahusika ila, IGP najua kuna watu unajua watukutu kwenye chombo chako, ni wakati wa kujitoa fahamu na 'kupoteza' baadhi yao! Pitisha fagio moja hatari sana mpaka wanyooke!

naongeza kuwa, wale wenye ndugu zao wanao husika na 'shughuli' mbali mbali kama hizi, tutawapiga mawe na kuwawasha moto.

mama awe makini sana maana kinyonga aliyenaye karibu atampeleka pabaya! sio mtu salama kabisa.
 
Tuliza mshono boss,,kwenye jukwaa la mapenzi nina haki ya kuchangia kutokana na mada inayojadiliwa na hata kwenye siasa vile vile. This is too low kutoka kwako ,so kuleta hapa comment yangu kutoka kwenye jukwaa la mahusiano inakusaidia nini wewe? Magufuli is dead and you should accept that .
Kumwambia mtu "kamfuate huko marehemu" ni dhihaka kubwa kuutolewa na mtu mwenye upeo mkubwa kama wewe...
 
Si mwenyewe raisi alisema ataweka mazingira mazuri kwa wawekezaji? Wawekezaji ndo wameanza kazi zao sasa... huyu Mama aliingia na gear mbaya sana , na itamcost, c alikua anajifanya anaruhusu kila kitu , leo Tz nzima inamlilia magufuli , hata waliomchukia wameanza kumkumbuka
Yaan wee acha tyuuh
 
mkuu tutaona na kusikia mengi tu. nchi hii kuiongoza s rahisi kama watu wanavyofikiria. JPM aliiweza vizr.
JPM huyu huyu aliyeshindwa kuajiri kama kikwete?,akiyeiba kura?,aliyeshindwa kuipandisha GDP?,aliekopa Trillioni 20 kwa miaka mitano tu?
Au munadhani kuendesha nchi ni kuzuia ujambazi tu?
JamiiForums355102718.jpg
 
Hawa watu si walikuwa humo humo na rais huyo?

Hata kama hapakuwa na mfumo, kwani hawawezi kugezea tu waliyokuwa wanafanya mazuri ili yaendelee bila huyo mtu mmoja kuwepo?
Yaani ndio unaona jinsi tulivyooza kimaadili. Mpaka tusimamiwe kama watoto wadogo.
 
Tutakumbuka mengi sana
Alisema mengi na kufanya bila woga
Hili la mauwaji alikomesha kwa kiasi kikubwa sana
Ujambazi na hata Ajali kama zilikuwepo ni kwa sehemu ndogo mno, Tochi za barabarani na semina za madereva zimesaidia sana
 
Mama Samia inafaa kuhusu ujambazi awe mkaliiii mkaliiii kaliiiiii mkaliiiiiiiiiiiiii kaliiiiiiiiiiiiiiiiii na Jeshi la polisi RPC apangue haraka sana ili awape amri haraka sana za kuwa ikiwa ujambazi utatoke mkoa wako, kazi RPC huna, na huo ndio mkataba wako, full stop
 
Kwa nini Mama alaumiwe?

Je, ni kweli kwamba Mama ameagiza Polisi waache kushughulika na UHALIFU na WAHALIFU?

Au, Kamanda Siro na timu yake wameamua kuachia UHALIFU NA WAHALIFU ili Mama Mh. Samia Suluhu Hasan "ALAUMIWE"

LAWAMA ZIELEKEZWE KWA KAMANDA SIRO NA TIMU YAKE.

WA KUWAJIBIKA NA AU KUWAJIBISHWA NI KAMANDA SIRO NA TIMU YAKE.
Nani anapaswa kumwajibisha Siro????
 
Afande sina cha kueleza, taarifa zinajitosheleza hapa chini!
View attachment 1792209
Tukio la kusikitisha limetokea leo mchana maeneo ya Juliana Mbezi beach ambapo Jimson Kibiki amefariki baada ya kupigwa risasi.

Kutokana na vyanzo vya mashuhuda Jimson alivamiwa alipokuwa ametoka bank na kuporwa na majambazi kiasi cha fedha ambacho mpaka sasa hakijajulikana.

Baada ya kupigwa risasi alipatiwa huduma ya kwanza na kusaidiwa kufika kituo cha afya lakini baada ya kufika hospital akapoteza maisha.

Jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi na tutaendelea kukujuza kila kinachoendelea.
Ni muda unepita toka nimesikia matukio haya. Enzi za kikwete.
 
Back
Top Bottom