Hoja yako inakosa uhalisia. Fikiria kuna watu wamezaliwa na wazazi vilema, wanaishi kijijini huko, nyumba mbavu za mbwa. Halafu inatokea mtoto ufanikiwe na baada ya hapo usiyabadilishe hayo maisha ya wazazi wako kweli?
Mi sijawahi kuona mzazi anakataa kujengewa nyumba na mtoto wake. Hiyo nadhani umeisema kama assumption tu kwamba, labda baba yake alikataa kujengewa.
Halafu inatia kinyaa, yaani mtu bilionea halafu eti mzee wako anaishi mbavu za mbwa, mabati yameegeshwa kwa mawe badala ya misumari. Halafu bilionea umekuja msibani na gari ya milioni 500. Hiyo kwako wewe ndo akili ya kitajiri?
Mimi wacha nibaki na mawazo ya kimaskini ya kujenga nyumbani kwa wazazi, wewe baki na mawazo ya kitajiri kwamba sio muhimu kujenga kwa wazazi, wacha waendelee kulala nyumba mbavu za mbwa, mimi nakula bata mjini, natumbua na warembo, niwahonge mamilioni!
Msimamo wangu ni ule ule: hakuna sababu itamfanya mtu kutojengea wazazi--hakunaa!
Hoja yako inaanza na logical fallacy.
Strawman argument logical fallacy.
Unaleta habari za mzazi kilema wakati hapa hatuzungumzii mzazi kilema.
Hii pia ni non sequitur logical fallacy.
Umekosea kanuni ya kulinganisha, kwamba unalinganisha habari ya mzazi kilema na mzazi asiye kilema.
Halafu unaendelea kutoa logical fallacy nyingine ya argument from ignorance ya "mimi sijaona mzazi anayekataa kujengewa nyumba".
Ukweli kwamba wewe hujaona haina maana hilo jambo haliwezekani. Inawezekana wewe huijui dunia tu. Hujaona mengi.
Usipende kuwapangia watu baki jinsi ya kuishi. Kubali kwamba kila mtu ana uhuru wa kuishi anavyotaka. Bilionea akikubali kwamba baba yake anaishi nyumba ya mbavu za mbwa, kwa sababu zao ambazo wewe huzijui na wala huna haki ya kuzijua, shika hamsini zako. Kama unapenda sana wazazi wajengewe, jengea wazazi wa kwenu. Kwani umekatazwa?
Wewe una mawazo ya kimasikini ya watoto kuwajengea wazazi. Haya ni mawazo ya kimasikini kwa sababu hujawaza kwamba kila mtu anaweza kubeba mzigo wa kujijengea yeye mwenyewe.
Ukiwaza mfumo wa wazazi kujengewa na watoto, una uhakika gani watoto watakuwepo kuwajengea hao wazazi?
Kuhusu msimamo wako, msimamo wako ni muhimu kwenye maisha yako, usiupe umuhimu sana msimamo wako kwenye maisha ya wengine.
Tatizo lako umejipa umuhimu usio nao katika maisha ya watu.