Mbwembwe nyingi mitandaoni, lakini makazi ya Baba Mkoani Iringa pa kawaida Sana

Huyo mzee alikuwa wapi kujenga nyumba yake iwe ya maana. Vijana jengeni maisha yenu kwanza achaneni na wazazi omba omba kama mleta mada
Waafrika wengi washakubali umasikini wa kutumia watoto kama mafao ya uzeeni.

Mara nyingi mzazi badala ya kujenga nyumba kabla ya kuzaa mtoto, ili hata mtoto akue kwenye mazingira mazuri, mzazi anazaa mtoto kwa matumaini kwamba huyo mtoto ndiye atakuja kumjengea nyumba mzazi.

Hii ni hoja ya kijinga sana. Halafu ishakubalika na watu wengi sana.
 
 
Walau sio mbaya kukiwa hata na muonekano.
 
Safi kabisa.
 
Hoja yako inaanza na logical fallacy.

Strawman argument logical fallacy.

Unaleta habari za mzazi kilema wakati hapa hatuzungumzii mzazi kilema.

Hii pia ni non sequitur logical fallacy.

Umekosea kanuni ya kulinganisha, kwamba unalinganisha habari ya mzazi kilema na mzazi asiye kilema.

Halafu unaendelea kutoa logical fallacy nyingine ya argument from ignorance ya "mimi sijaona mzazi anayekataa kujengewa nyumba".

Ukweli kwamba wewe hujaona haina maana hilo jambo haliwezekani. Inawezekana wewe huijui dunia tu. Hujaona mengi.

Usipende kuwapangia watu baki jinsi ya kuishi. Kubali kwamba kila mtu ana uhuru wa kuishi anavyotaka. Bilionea akikubali kwamba baba yake anaishi nyumba ya mbavu za mbwa, kwa sababu zao ambazo wewe huzijui na wala huna haki ya kuzijua, shika hamsini zako. Kama unapenda sana wazazi wajengewe, jengea wazazi wa kwenu. Kwani umekatazwa?

Wewe una mawazo ya kimasikini ya watoto kuwajengea wazazi. Haya ni mawazo ya kimasikini kwa sababu hujawaza kwamba kila mtu anaweza kubeba mzigo wa kujijengea yeye mwenyewe.

Ukiwaza mfumo wa wazazi kujengewa na watoto, una uhakika gani watoto watakuwepo kuwajengea hao wazazi?

Kuhusu msimamo wako, msimamo wako ni muhimu kwenye maisha yako, usiupe umuhimu sana msimamo wako kwenye maisha ya wengine.

Tatizo lako umejipa umuhimu usio nao katika maisha ya watu.
 
Huyo mzee alikuwa wapi kujenga nyumba yake iwe ya maana. Vijana jengeni maisha yenu kwanza achaneni na wazazi omba omba kama mleta mada
We ungejiskiaje mumeo aje kwenu kujitambulisha halafu unakuta mfano kwa mzee wako ni nyumba mbavu ya mbwa, mabati yameegeshwa kwa mawe badala ya misumari.

Wazee wako bahati mbaya standard seven, hawana kazi ya maana. Halafu wamekusomesha mtoto, unafanikiwa, upo zako mjini unakula bata, huoni umuhimu wapate hata nyumba ya milioni 20. Huo ndo ujanja?

Na ukienda kumtambulisha mumeo, bado utajiskia sawa tu kumkaribisha kwenu nyumba mbavu za mbwa?
 
Nitajisikia sawa kwasababu ni kwetu. Kwani mume anakuja kuishi kwenye nyumba ya wazazi wangu? Kama walishindwa kujenga mi nifanyeje sasa
 
Walau sio mbaya kukiwa hata na muonekano.
True.
Sio powa nyumba zimechoka kinoma vumbii.

Yaani mpaka jamaa zako ikitokea msiba unaona aibu kwenda nao kijijini maana ni choka mbaya.

Tuliwai PATA msiba miaka kumi na tano iliyo pita ikawa aibu watu wanasema pamoja na maisha mazuri town..kwao na mzee ni choka mbaya
Haya ni mawazo ya enzi za FEUDAL MODE OF PRODUCTION.

Pengine,
Kwa ufupi ni mawazo ya kijima (primitive era)
 
Mkuu, kwenye hili utazungumza falsafa zote, na nitaishia kutokukuelewa.

Huko vijijini mzazi hata asipokuwa kilema, haimfanyi awe na uwezo wa kujijengea nyumba. Kuna maeneo ni wakulima wa msimu mmoja, ni ngumh sana mtu kupata kipato cha kujenga nyumba nzuri ya kuishi.

Sasa mtu ufanikiwe kiuchumi, halafu ushindwe kuibadili hiyo hali ya ulipozaliwa? Kwamba waendelee kuishi kwenye nyumba zao mbavu za mbwa, kisa wameshindwa kujijengea wenyewe?

Kuna element ya kujisahau. Mtoto anaweza kuwa tajiri ila akasahau kuwajengea wazazi. Na wazazi huwa hawana kawaida ya kuwakumbusha watoto wao kuwajengea. Ila unapojiongeza na kuwajengea, huwa wanashukuru sana na wanakuwa na furaha mno.
 
NI ngumu sana ndio maana hao jamaa wakipata wanakumbuka sana nyumbani nilifurahia kile kitu kwa kweli sasa viti kama hivi mikoa mingine hakuna kabisaa wanawaza maisha yao tu mtu anakomaa anakwambia atajengaje nyumba kwa Mwanaume mwingine akimaanisha Baba yake daah..
 
Of course huwezi kunielewa.

Huijui dunia. Una mawazo ya kijima.

Habari ya kutegemea watoto kujengea wazazi ni umasikini. Jengeni jamii inayowezesha kila mtu kujijengea. Wazazi waweze kujenga kabla ya kuzaa watoto.

Zaidi, unachopenda wewe, unachotaka wewe, si muhimu. Labda ni muhimu kwenye maisha yako, lakini si muhimu kwenye maisha ya wengine.

Watu tofauti wana matakwa tofauti, waacheni waishi wanavyotaka, msiweke viwango vyenu ndiyo viwe viwango vya kila mtu.

Huelewi wapi?
 
Hiyo hali ikitokea msiba lazima uogope. Yaani huku mjini mtu unaonekana wa maana, una marafiki wazito wazito. Halafu umefiwa, wadau wanaenda nyumbani kwenu wanakuta vumbi vumbi tu hakutamaniki. Mfano nyumba mbavu za mbwa kama hivo. Mtu lazima ujisikie aibu kuu!

Nabaki kusema: hakuna utetezi wa kutokujengea wazazi.
 
Hizo ni fikra zako wewe, si kila mtu anajali hivyo wala anatakiwa kujali hivyo.

Kwanza huyo unayemuita baba yake mtu una uhakika gani kuwa ni baba yake kweli?

Ulifanya DNA test?

Unajuaje kuwa hakuna habari tofauti za ndani ya familia ambazo wewe huzijui?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…