Mbwembwe nyingi mitandaoni, lakini makazi ya Baba Mkoani Iringa pa kawaida Sana

Lakini mkuu, hili suala usiliweke tu kwenye mizania ya mtoto kumjengea mzazi, lifikirie kwenye angle ya wenye uwezo kujitoa kusaidia wasio na uwezo.

Mbona hata kwenye makampuni kuna kitu wanaita corporate social responsibility (CSR). Utaratibu ambao makampuni ya kibepari wanatumia kuwainua masikini.

Sasa mtu ukiwa tajiri na wazazi wako masikini, kuna ubaya upi wa wewe kuwainua kiuchumi? Walale pazuri, bima ya afya, chakula kizuri, n.k

Yaani nashangaa hili suala la kuwasaidia wazazi kwa malazi linaonekana kuwa ni dhambi.

Wazazi hata siku moja hawatakuomba uwajengee nyumba. Ni wewe mwenyewe kujiongeza.

Hivi nikuulize swali: ina maana wewe kwenye maisha yako unawasaidia watu tu ambao wanakuomba msaada, au kuna watu hawakuombi msaada lakini unaamua kuwasaidia tu kwasababu unaona kabisa wanahitaji msaada?
 

Safi Kabisa
 
Kwahiyo unataka kusema nikipata mchumba nikajenge kwa wazazi wangu ili mchumba akija akute mambo safi? Au sijakuelewa vizuri?
Hata bila kupata mchumba, walau nyumbani kwenu pawe panaonekana.

Yaani kama kulikuwa hakuna hata umeme, kwani ni mbaya kuweka umeme? Iwe tu kwamba unatoa msaada ili nyumbani nao wajione wanaishi. Wao kushindwa kujijenga kimaisha sio dhambi na adhabu ya wewe kutoboresha maisha yao.
 
Sio mbaya kufanya yote hayo lakini pia sio vibaya kutokufanya. Ukute mtu ana sababu zake kwanini hafanyi lolote, hatupaswi kumjudge.
 
Ni aibu kwa mtoto wa kiume kuanzisha mada kama hii. Ila kama we ni wa kike basi hakuna tatizo ila tu utambue kuwa kwenye mafamilia huku kuna mambo mengi sana. Hata kwenye familia yenu kuna mambo mengi tu ya ajabu ajabu
Tulitegemea Bilionea kama huyu tukute Makazi ya Baba yake yawe kama ya Mzee Mengi kule Machameni

Huyu alipaswa ajenge kwao kwanza ndiyo atafute umaarufu, HUWEZI ukawa Maarufu unahongahonga wadada wakali wa Chuo Kikuu halafu huku tukija Maisha ya Baba yake makazi Duni
 
Sio mbaya kufanya yote hayo lakini pia sio vibaya kutokufanya. Ukute mtu ana sababu zake kwanini hafanyi lolote, hatupaswi kumjudge.
Mbona hizo sababu zinawekwa kwenye mabano sana?

Tuelezane hapa points zilizo wazi. Hizo sababu zinaweza kuwa zipi? Tusijifiche tu kwenye kichaka cha, "zipo sababu."
 
Wajuzi wa mambo hapa JF watakuambia, "hakuwa na sababu eti za kumjengea baba yake", kwamba kisa baba yake alishindwa kujijengea yeye mwenyewe!
 
Sasa kama hana uhakika kwamba huyo ni baba yake, si angejikausha tu asiseme amefiwa na baba na wala asiende msibani?

Bado hujaleta sababu za nikwanini mtoto asimjengee mzazi. Unajificha kwenye kichaka cha, "zipo sababu." Ni zipi hizo sababu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…