Member gani ameku-inspire katika jambo fulani

Member gani ameku-inspire katika jambo fulani

Akipunguza huba iliyokithiri kwa Wanamagharibi, atafika mbali sana. Madini yake nachota kama kawaida, lakini aache kabisa kuivaa Urusi.

Nikitulia, ntamuuliza atwambie jinsi Tanzania ilivyonufaika na wataalamu wabobevu na madaktari bingwa kutoka Urusi enzi hizo.

Yaani ile ukiambiwa tu fulani huyu kasomea Urusi, unasema Ewaaa! Mtu si huyu sasa!

Lakini hizo zote jamaa hazioni. Yeye anaona tu vifaru vya Abrams na makombora ya ATACAMS. Bure kabisa!

Nachelea hata kusema kwamba nchi yetu inaendelea kuwa maskini kwa sababu ya uwepo wa vimbunga vya watu wa namna yake.
Mkuu, mbona hata wewe umeshindwa ficha huba lako kwa urusi?
 
Jf, kuna watu wametu-inspire, mambo mengi bila hata wao kujua. Kupitia mada hii wataje/mtaje member, aloku-inspire ktk jambo fulani.

LIST YANGU:

1. WALONI-INSPIRE KTK SANAA YA UANDISHI

Robert Heriel Mtibeli, MALCOM LUMUMBA, yoga, Nifah, Da'Vinci.

2.WALONI-INSPIRE KTK UCHESHI
Ushimen, KENZY, eron, Extrovert, Evelyn Salt, @Toyeye, Kalpana, Joanah, mzabzab & nk...

3. CRITICAL THINKING
Kiranga.

4.MAARIFA YA ZIADA
Mshana Jr, DR Mambo Jambo.

5.MEDANI ZA KIVITA
T14 Armata.

6. HISTORIA & SIASA ZA KIMATAIFA
MALCOM LUMUMBA, zitto junior.

7. KUSAMBAZA LIKE
raraa reree, min -me.

8.BUSARA & HEKIMA
Aaliyyah, Manyanza, Grahams, Carleen, Kelsea, Etugrul Bey,financial services.

9. SIMULIZI
@OMUGHAKA, Analyse.

10. UPENDO
Smart911 & Mahondaw.

Nawe wataje, member walokuinspire ktk jambo fulani.

Ahsante Sana Mkuu.

Karibu Makande
 
Mkuu, mbona hata wewe umeshindwa ficha huba lako kwa urusi?
Mkuu, mimi sina huba yoyote na Urusi wala Putin. Mimi nina ruwaza tangamano (reasonable understanding) kuhusu sera za Urusi na Putin.

Hivi unachukuliaje sera ya Marekani kwamba kama nchi fulani itaachana na matumizi ya dola zake, basi itabebeshwa mzigo wa ushuru kwa 100%?

Kwa nini zisiwepo sera mujarabu katika diplomasia ya biashara, badala ya kutanguliza ubabe butu kama huo?

Unadhani Marekani yenyewe ingefurahia kufanyiwa hivyo, kama ndiyo ingekuwa na hali ya nchi hizo?

Wakati ambapo Urusi anajaribu kuziinua nchi zingine ili wakue pamoja, Marekani anazikandamiza na kuzidhoofisha ili azitawale na kujinufaisha kwazo.

Kinachoudhi zaidi ni pale ambapo Marekani anazitisha waziwazi nchi zinaoonekana kuiunga mkono Urusi, kana yenyewe ndiyo ina hakimiliki ya dunia.

Kwa nini Marekani asitumie ushawishi wa kidiplomasia ili kuzivuta nchi hizo kwenye sera yake?

Kama haiwezi kuzishawishi, basi ni wazi kwamba ama hana uwezo wa kuzisaidia au hana nia hiyo.

Kwa nini basi katika hali kama hiyo iwe makosa kuonesha huba kwa Russia na kuwaponda akina T14 Armata ambao, kwa sababu ya kujishibisha mali haramu za huyo Kiranja wa Magharibi, wanakesha kutwa kucha wakiwapigia upatu wa bati?
 
Sijui ID yake humu ila ameniinspire sana si mwingine ni Billionaire Donald Trump
 
Mkuu, mimi sina huba yoyote na Urusi wala Putin. Mimi nina ruwaza tangamano (reasonable understanding) kuhusu sera za Urusi na Putin.

Hivi unachukuliaje sera ya Marekani kwamba kama nchi fulani itaachana na matumizi ya dola zake, basi itabebeshwa mzigo wa ushuru kwa 100%?

Kwa nini zisiwepo sera mujarabu katika diplomasia ya biashara, badala ya kutanguliza ubabe butu kama huo?

Unadhani Marekani yenyewe ingefurahia kufanyiwa hivyo, kama ndiyo ingekuwa na hali ya nchi hizo?

Wakati ambapo Urusi anajaribu kuziinua nchi zingine ili wakue pamoja, Marekani anazikandamiza na kuzidhoofisha ili azitawale na kujinufaisha kwazo.

Kinachoudhi zaidi ni pale ambapo Marekani anazitisha waziwazi nchi zinaoonekana kuiunga mkono Urusi, kana yenyewe ndiyo ina hakimiliki ya dunia.
Mkuu, marekani anatetea maslahi yake, na reaction yake ni ajili ya kulinda maslahi yake.
 
Back
Top Bottom