Nawasalimu wanajf wote popote mlipo.
Siku ya pili Sasa nimeshindwa kupata jibu la swali tajwa ,maana ni kilio kwa kila ndugu na jamaa kutoka mikoa mbali mbali ambao tunawasiliana muda mwingi achilia wazee wangu walio vijijini,wakati inasemakana mama anaupiga mwingi.
Kwa kuwa JF Kuna wachumi na watu wenye UPEO wa Mambo ya kadha wa kadha naombeni mnijibu swali langu
Mpaka Sasa
1. Vifaa vya ujenzi havikamatiki, naambiwa Mwanza mfuko unacheza kuanzia Elfu ishirini na kuendelea, DODOMA mfuko kuanzia tsh 17000 na kuendelea,ujaweka mabati , nondo n.k, Sasa sijui mikoa ya pembezoni Hali ipo vipi ,jibu Hali itakua mbaya
2.Matumizi ya kila siku ya nyumbani Hali ipo ivyo, nyama kwa Sasa wanakula wachache maana kilo ipo elfu saba mpaka elfu nane
Kwa ujumla kila kitu kiko juu, Bila kusahau miamala ya kwenye simu ,ukitoa tsh 120,000/= Makato ni elfu 5300 na point
Katika mazingira Kama ya Sasa tunatoka vipi, na shida nini Hali kua Kama ilivyo sasa