Migogoro ya kimahusiano: Janga kwa Wanawake Tanzania

Hakika tusikae kimya hawa watu wamechanganyikiwa watatumaliza
Namuelewa baba angu alivyokua ananifundisha kupigana kwa kujihami ningali binti mdogo kumbe alijua nikikua nitakutana na mibazazi isiyokua na utu, na mimi nawabutuaga wakiniletea ujinga ujinga, wanaume wa dunia nzima sio wa kuwachekea wana ka uchizi ka asili
 
Au tuitishe mdahalo tuwafanyie counselling hali ni mbaya sana
 
Umesema kweli, wanaume hamjui kufarijiana, ukishare hiyo kwa washikaji zako wanakujaza upepo ukirudi unamtia bisu mtoto wa watu na majuto huanzia hapo,

Tuzunguke koooooote ila ishu hapo ni changamoto ya afya ya akili
 
Kwako wewe mwanamke kuzabwa kibao ni sababu ya kukimbia ndoa.?

Ifike pahala msiolewe kabisa nyie sio wanawake ni wasichana
Unaona kibao ni kawaida? hujui kidogo huzaa kikubwa, na sio kibao tu hata mtu akionekana kosa dogo anapandisha mori, anabadilika sura hiyo ni redflag mwanamke aache ndala mapemaaaa
 
Asile yale masotojo, watu wanatia kidogo kidogo kwenye chakula baada ya muda presha au ini chaliiii
 
Umesema kweli, wanaume hamjui kufarijiana, ukishare hiyo kwa washikaji zako wanakujaza upepo ukirudi unamtia bisu mtoto wa watu na majuto huanzia hapo,

Tuzunguke koooooote ila ishu hapo ni changamoto ya afya ya akili
Siku kweka akipewa nafasi ya kueleza kinagaubaga huu uzi utakuwa hauna maana, wachangiaji wengi wa nyuzi humu hawajaolewa wala kuoa. Kuta zina siri nyingi sana.

Kuna jamaa alienda kijinyonga akaacha ujumbe unaosema "Mke wangu naenda kwa Baba mbinguni, labda ukiishi bila mimi utakuwa na furaha. Tukubali tukatae haya matatizo yanachangiwa sana na wanawake.

Kuna ndugu yangu alifumania mke wake na mfunga mageti jamaa alimkuta mfanyakazi anamdinya mke wake chumbani wanapolala, mshikaj mpaka leo ni mlevi kupindukia.

Yapo mengine mengi tu, kuua kwa kukusudia ni kosa la jinai adhabu yake ni kifo, pia ni dhambi mbele za MUNGU, ndiyo maana bible inatuasa tuishi na wanawake kwa akili, bila kutumia akili hawa viumbe wanakupeleka lupango kweupee.

Tusibase kuongelea upande mmoja, Tusubiri ya kweka nayo yatakuja hivi karibuni.
 
Tunasema siku zote acheni kubeba machungu wanaume zungumzeni

Kuna nguvu ya uponyaji katika kuongea Narudia tena hakuna mwenye haki ya kuua mwingine
 
๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…

Jitahidi uwe jirani na dawa zako za Presha, unaweza jikuta askari anayefia vitani ๐Ÿ˜…

Binafsi nimebaki kucheza na Wajukuu tu, sio zaidi ๐Ÿคช
Hapo umenishauri vizuri Mzee mwenzangu.
 
Tunasema siku zote acheni kubeba machungu wanaume zungumzeni

Kuna nguvu ya uponyaji katika kuongea Narudia tena hakuna mwenye haki ya kuua mwingine
Nakazia hakuna mwenye haki ya kuua mwingine.

Kauli yako inadhihirisha vyema uelewa wa tabia za wanaume kwenye kuweka mambo moyoni, lakini bado hii mikasa tunaendelea kuisikia, kama wanavyosema upendo/mahusiano ya ndoa si jukumu la mwanamke au mwanaume pekee ni ushirikiano.

Kama wanawake wangekuwa na uthubutu wa kuhoji kero zao na za waume wao kuhusu magomvi yao, nafikiri hivi visa vingepungua sana, lakini wakati wanawake wanashinikiza wanaume kuwa wawazi, wanawake wao wako bize kuchochea moto.

Kuna kipindi nilijitahidi kukonsalt na mpenzi wangu, tuweke mambo sawa, wala hakunipa huo muda, nilijaribu kueleza lakini akijua nia yangu alipuuza, kwasababu sikuwa nimeuoa nikamwacha akaenda zake kwa amani.

Kuna kipindi nilitamani wanaume tungeishi wenyewe tu kama malaika, hakuna kuoa, kuolewa wala kuwa kwenye mahusiano, ni mwendo wa kuimba tu milele na milele๐Ÿ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ