Migogoro ya kimahusiano: Janga kwa Wanawake Tanzania

Migogoro ya kimahusiano: Janga kwa Wanawake Tanzania

Kipenzi, wanaume wa hii nchi sahau kama watabadilika. Malezi wanayopewa huko majumbani, yanawafanya wao wajione miungu watu. Imagine mtu anakua kwenye utamaduni ambao mtoto mdogo wa kiume anapigiwa magoti na mwanamke mkubwa akiwa anapewa chakula. Unategemea huyu mtoto akikua mkubwa atachukulia mwanamke kama binadamu au atamuona kama ng'ombe tu??. Sisi wanawake ndo tuhamasishane kukataa ukatili. Na ukatili hua hauanzi mkubwa,unaanza kidogo kidogo. Tuwaambie mabinti zetu" ukipigwa kofi kimbia, ukitishiwa kwa maneno kimbia".uhai ndo muhimu zaidi vingine vyote vinatafutwa. Ila wanawake unakuta ndo tunaambiana" kofi tu unaondoka,bibi zetu walivumilia vipigo, wanaume wote ndo wapo hivyo". Mwisho wa siku mtu anauwawa. Unyanyasaji utakomeshwa na sisi wanawake sio kusubiri wanyanyasaji watuonee huruma.
Hiki ndicho kinatakiwa kufanyika. Kingine cha kuongezea tuwafunze mabinti zetu KUTAFUTA pesa zao wenyewe. Wasiwe wategemezi kwa wanaume.

Ukiangalia post nyingi humu wanaume wanasema wanawake wanakula pesa za wanaume au wanataka mali za wanaume halafu wanawasaliti ndiyo maana wanauawa.
Wasichana amkeni!!!! Tafuteni pesa msisubiri wanaume ambao wengi ni nusu psychopath!!!!!!
 
Kipenzi, wanaume wa hii nchi sahau kama watabadilika. Malezi wanayopewa huko majumbani, yanawafanya wao wajione miungu watu. Imagine mtu anakua kwenye utamaduni ambao mtoto mdogo wa kiume anapigiwa magoti na mwanamke mkubwa akiwa anapewa chakula. Unategemea huyu mtoto akikua mkubwa atachukulia mwanamke kama binadamu au atamuona kama ng'ombe tu??. Sisi wanawake ndo tuhamasishane kukataa ukatili. Na ukatili hua hauanzi mkubwa,unaanza kidogo kidogo. Tuwaambie mabinti zetu" ukipigwa kofi kimbia, ukitishiwa kwa maneno kimbia".uhai ndo muhimu zaidi vingine vyote vinatafutwa. Ila wanawake unakuta ndo tunaambiana" kofi tu unaondoka,bibi zetu walivumilia vipigo, wanaume wote ndo wapo hivyo". Mwisho wa siku mtu anauwawa. Unyanyasaji utakomeshwa na sisi wanawake sio kusubiri wanyanyasaji watuonee huruma.
Hii post iwekewe LAMINATION. Thank you so much.

Huu ujinga wa kupigia magoti mtoto mdogo wa kiume niliukataa.
 
Hiki ndicho kinatakiwa kufanyika. Kingine cha kuongezea tuwafunze mabinti zetu KUTAFUTA pesa zao wenyewe. Wasiwe wategemezi kwa wanaume.

Ukiangalia post nyingi humu wanaume wanasema wanawake wanakula pesa za wanaume au wanataka mali za wanaume halafu wanawasaliti ndiyo maana wanauawa.
Wasichana amkeni!!!! Tafuteni pesa msisubiri wanaume ambao wengi ni nusu psychopath!!!!!!
Naunga mkono hoja

Licha ya kua hakuna mwenye haki ya kuua mwingine

Wanaume nao waache ujinga wa kujimaliza
na wanapogundua wamepigwa waende kwenye sheria

Mwisho kabisa kama mwanamke mwenzangu ukihisi huna nia na mtu usile vyake
 
Yaani mkuu, mtu anaedundwa halafu anabaki huwa simuelewi na sitokaa nimuelewe. Hivi ile hofu tu ya kibinadamu hawana?. Yaani unakaa nyumba moja na mtu anakudunda hadi unazimia? Tena unalala nae kitanda kimoja. Watu wana mioyo jamani.
Sijawahi kuwaelewa na sitakuja kuwaelewa
 
Wamelelewa kwenye huo huo ukatili unategemea nini?. Mtu amekua anashuhudia baba anampiga mama unategemea asije kumpiga mke wake?. Na kuna wanawake pia wanatetea huu ushetani, hapo ndo utachoka zaidi. Mwanamke ukizaliwa Afrika maisha tayari yameshakupiga 1-0, usipojipambania hakuna atakaekupambania.
Mimi naona kama 1-0 kama ni ndogo!!! Nadhani ni 3-0!!!!!!
 
Sa hivi wameng’ang’ania ka point kao ka tamaa ya mali, hizo takwimu hapo ngapi zinaonesha mauaji yamefanyika sababu ya tamaa/ugomvi wa mali?

Mi natoa wito kwa wanawake wenzangu, it’s either muwe wapole au muache kuhusiana na hawa watu, Walahi mtaisha kweli.
Waache mahusiano na wanaume kabisa? Haiwezekani. Kumjua mwanaume ambaye anaweza kukutoa uhai pia ni ngumu. Mwanaume mwenye msongo wa mawazo haongei mengi na si mwepesi wa kukiri changamoto zake, hasa kwa mwanamke asiye msikivu. Kinyume chake, mwanamke anayepitia stress ni rahisi sana kumjua kwasababu atakua anaongea sana hisia zake, bila kujali madhara ya kauli zake. Reaction ya wanawake wa namna hii kwa wanaume zao wanaopitia stress kali mara nyingi huwa ni "makelele" na kauli za "maudhi". Baadhi wanakuendea mpaka ustawi wa jamii/kwa wanasheria kwa mambo ambayo hata hamjakaa kujadili kwa kina hapo ndani.

Hali hii hupeleakea ugomvi, na wakati mwingine, kutoana roho. Binafsi naamini suluhisho la kudumu la haya yote ni jamii kuelimika na kubadilika mitazamo yetu kuhusu nafasi zetu ktk mahusiano.
 
Imagine, hata mimi nimeanza kubana suruali zangu na kuziwekea zipi kwa chini, hii yote ni kufanya nionekane kijana.

Pia najitahidi sana kusikiliza nyimbo za hawa sijui akina harmonize na diamond n.k, zile nyimbo zangu za Ottu Jazz, OSS, DDC mlimani park nazisikiliza nikiwa mwenyewe tena kwa kijificha Ili nisionekane Mzee.
Kwani wewe una umri gani? Hauko umri mmoja na kina Mbaga Jr?
 
Kwa mtazamo wangu, migogoro pamoja na mauaji kwenye mahusiano ya kindoa ama mahusiano ya mtu na mpenzi wake, yanachangiwa na mambo kadhaa

✓Uchepukaji, mke akiolewa atambue kwamba hatakiwi kuchepuka. Iwapo utachepuka, mumeo akajua, sio rahisi kukusamehe. Atakutafutia angle lazima akuue ama amuue huyo mgoni wake

Na kwa wale waliopo kwenye mahusiano ila hawana ndoa, ukichepuka na huyo mpenzi wako ndiyo alikuwa anakulipia Kodi na kukuhudumia, anaweza kuchukua uamuzi wa kukuua ama kukuumiza

✓Mali, mume akijua una mpango wa kumdhurumu jasho lake, anaweza kukupoteza pia ili abaki na jasho lake

Nashukuru Mungu, mke wangu hadi hapa tulipofikia, sijamwona akiwa na hayo mawili

Kuna mtu(sio bibienu) nilitaka kumfanyia hilo, maana nilijua kumgharamia mjinga yule, useme roho wa Mungu alinijaza ujasiri wa kusamehe, vinginevyo nilitaka kuchukua uamuzi wa kumfuta kabisa.

Anyways, Fimbo ya mbali haiui nyoka
Mzee mwenzangu mbona umeandika kwa upande wa makosa ya wanawake tu? Unataka kusema kuwa wanaume huwa hawasababishi maudhi yoyote kwa wanawake ambayo yanaweza kasababisha migogoro kwenye ndoa au mahusiano?
 
Hiyo Idadi ni ndogo sana ukilinganisha na Idadi jumla ya watanzania milion 60+

Leta takwimu za vifo kwa ajali za Bodaboda Kwa siku

Leta takwimu za vifo kwa ajali za magari

In a nutshell siungi mkono mtu yoyote kuua mtu yoyote. Ila dada zetu kuweni makini sana. Dunia imebadirika watu wana misongo ya mawazo. Kama mtu anaweza kujiua anashindwaje kukuua.


Acheni Tabia za kudanga mwisho wake ni mbaya!

Acheni Tabia za kuww kimaslahi na wanaume

Kama humpendi mtu acha kula Hela zake


Na nyie wanaume acheni Tabia za kutoa Kwa mwanamke usichoweza kupoteza. Give what you can afford to lose! Toa kama sadaka usisubiri returns hata likitokea lolote uwe in safe zone.
Ushauri mzuri sana. Ubarikiwe
 
Angalizo msomaji wangu bandiko ni refu kidogo
Naomba uwe mvumikivu katika usomaji wako
Karibu sana kwenye mada 😊

Hello Great Thinkers 🫡

Katika pita pita zangu huko IG nimekuta kuna dada mmoja amepost kuhusu vifo vinavyotokana na migogoro ya kimahusiano hapa Tanzania 🇹🇿

Nimekuwa shocked baada ya kuona takwimu zinaogopesha na kushangaza
Ikanisukuma niende kwenye mtandao ku search na nione hali ilivyo kwa kujihakikishia mimi tomaso nimeshtushwa
Sikujua hali ni mbaya kwa ukubwa huu!

Nimepigwa butwaa
Hali inatisha

Chanzo cha takwimu (LHRC Tanzania)

Niweke sawa hapa
Hizi takwimu ni kati ya mwaka 2019_2023

Hebu tuangalie hizi takwimu za mauaji yanayohusisha wenza wa kimapenzi Tanzania

2019: LHRC ilirekodi wanawake 12 waliouawa na waume/wenza wao ambapo 8 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu

2020: LHRC ilirekodi wanawake 32 waliouawa na waume/wenza wao, ambapo 23 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
Hii ilikuwa zaidi ya mara mbili ya matukio yaliyorekodiwa mwaka 2019

2021: LHRC ilirekodi jumla ya matukio 35 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika hao, 31 walikuwa wanawake na 4 wanaume, huku wanawake wakiwa takribani 89% ya waathirika
Pia, 72% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu

2022: Kulikuwa na matukio 33 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika, 31 walikuwa wanawake na 2 wanaume, wanawake wakiwa takribani 94% ya waathirika. 52% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu

2023: LHRC ilirekodi matukio 50 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi, ikiwa ni ongezeko la matukio 17 ukilinganisha na mwaka 2022
Kati ya waathirika hao, 45 walikuwa wanawake na 5 wanaume, wanawake wakiwa 90% ya waathirika. Takribani 46% ya matukio yalihusishwa na wivu.

Mjumuisho 2019–2023: Jumla ya matukio 162 ya mauaji yaliyorekodiwa katika takwimu hizi. Kati ya waathirika waliotajwa, wanawake ni 151

Mjadala👇

Sitaki kusema hakuna wanawake wanaofanya ukatili
Tumeona wapo na siwezi kufumbia macho hili hata kidogo

Wanawake wenzangu JF hakuna haja ya kukatisha maisha ya mtu kwa sababu tu ya mapenzi au migogoro mbalimbali
Ukiona mzigo ni mkubwa, tafuta msaada
Usimue mtu
Huna haja ya kuua, hilo sio jukumu lako

Kwa sababu hata usipomuua, kwa nature ya mwanadamu kila mtu lazima atakufa siku yake

Nina hakika wanaofanya mauaji huishia kwenye majuto ya milele

Tuje kwa wanaume ambao ni tishio...

Enyi wanaume, acheni kuua wanawake
Hawa ni mama zenu, dada zenu, wadogo zenu
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine kwa sababu tu amesalitiwa, amevunjwa moyo au amekataliwa

Ukihisi umefika sehemu huwezi kujidhibiti, tafuta msaada
Tafuta hata wataalamu wa saikolojia
Kama umechanganyikiwa na hujui ufanye nini, ongea uponeeee

Acha kubeba uchungu peke yako. Tafuta mtu wa kuongea naye
Kama unaogopa jambo lako kutangazwa, tafuta hata mtu asiyekujua, funguka na zungumza

Usiue Please
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine

Kama unaona hakuna future kwenye mahusiano, jikatae mapema na muachane kwa amani

Niseme hili👇
Wanaume, mkubali mkatae, mna udhaifu ambao mnatakiwa kuushinda
Kujifunza kustahimili maumivu rejection usaliti na kuvunjika moyo ni sehemu ya kukomaa

Chukulieni mfano hata hapa jukwaani
Watu wanaoongoza kuwakalia kooni wengine ni wanaume nyie hapo🫵
Nasikia wengine wanapita mpaka PM wakisambaza picha za wanawake ambao hawana hata uhakika nao
Kitu ambacho ni nadra kwa wanawake kufanya

Kuweni wakomavu
Jifunzeni kustahimili

Mbona wanawake wanahangaika na maisha?
Unakuta mama kaachiwa watoto, anakomaa na haui mtu
Amedhulumiwa anatulia

Anamfumania mume wake kitandani, tena na house girl kwenye kitanda chake mwenyewe lakini mama anapiga moyo konde

Mnazalisha nje huko, wanawake wanapiga moyo konde

Enyi wanaume, nyie mna roho za barafu?
Wanawake wana roho za chuma?

Sitetei yeyote
Sitetei mwanamke msaliti wala mwanaume msaliti

Lakini ukiona umeshindwa kabisa kuendelea na mahusiano, achaneni kwa amani

Tatizo ni nini mpaka hali imefika hivi?

Karibu tujadili kwa pamoja
Na kuelemishana 🙏🙏

ShesRise_1 ✋️
Baada ya mkutano wa Beijing 1995,wanawake mka ona mko sawa na wanaume kuanzia kifikra mpaka majukumu bila kuelewa kwamba mwanaume atabaki kuwa mwanaume.

Nyumba nying zina Kelele mno,wanaume ndo wahanga lakn huku nje inaonekana mwanamke anaonewa,unatoka kazin umechoka unafika home unapokelewa na kelele yan ni stress tupu,muda mwingine hizo kelele hujui chanzo chake hisia zake zikimtuma yeye ni kubwata tu,wanaume always hatupend kelele ndo mana weng mnaishia kupigwa au kuuliwa mana siku hiz hamuongei kwa adabu,hujui kutofautisha kuongea na mumeo na mfanyakaz wa ndan au mtoto wako.

Weng mna viburi huwez kumgombeza mumeo au kuongea hadharan mambo yakudhalilishana mbele za watoto au mfanyakaz wa ndan tena umenishikia kiuno aisee? Heshima kwa wanawake imeshuka,labda kwasababu na nyie mnavaa suruali kama sisi? Miaka 3 nyuma nikihudhuria sherehe ya jiran yangu yakumpongeza binti yao kumaliza chuo,ulipofika muda wa kutoa nasaha kwa wazaz Baba alimpongeza bintiye na kumpa zawad ilipofika zamu ya Mama,akaanza kumsihi mwanae asome zaid ya hapo na asiwaamin mana wanaume sio watu ahakikishe amepambana awe na pesa...aisee nilijisikia vibaya sana kwamba wamama wanaharibu watoto ebu pata picha anayomjengea binti yake? Huyu binti atakuwaje huko mbele? Heshima kwa mumewe itakuwepo?

Kama wanawake wameshindwa kujitambua wao wakina nan,hili janga la MAUJI halitokoma abadani. Mana tumeamua kuiga mfumo na utamadun wa kimagharibi,tukaacha mila na desturi za mwafrika kuwa mwanamke lazima awe mnyenyekevu kwa mumewe,lakn siku hiz ASASI za kigen zinafunguliwa kila siku zikijifanya kumpandia mwanamke ili hali linazid kuchochea moto mana MAFAHALI WAWILI hawawez kukaa ZIZI moja.
 
Hiki ndicho kinatakiwa kufanyika. Kingine cha kuongezea tuwafunze mabinti zetu KUTAFUTA pesa zao wenyewe. Wasiwe wategemezi kwa wanaume.

Ukiangalia post nyingi humu wanaume wanasema wanawake wanakula pesa za wanaume au wanataka mali za wanaume halafu wanawasaliti ndiyo maana wanauawa.
Wasichana amkeni!!!! Tafuteni pesa msisubiri wanaume ambao wengi ni nusu psychopath!!!!!!
Wanataka wasiliwe pesa zao sasa ziliwe za nani...
 
Back
Top Bottom