Migogoro ya kimahusiano: Janga kwa Wanawake Tanzania

Hiki ndicho kinatakiwa kufanyika. Kingine cha kuongezea tuwafunze mabinti zetu KUTAFUTA pesa zao wenyewe. Wasiwe wategemezi kwa wanaume.

Ukiangalia post nyingi humu wanaume wanasema wanawake wanakula pesa za wanaume au wanataka mali za wanaume halafu wanawasaliti ndiyo maana wanauawa.
Wasichana amkeni!!!! Tafuteni pesa msisubiri wanaume ambao wengi ni nusu psychopath!!!!!!
 
Hii post iwekewe LAMINATION. Thank you so much.

Huu ujinga wa kupigia magoti mtoto mdogo wa kiume niliukataa.
 
Naunga mkono hoja

Licha ya kua hakuna mwenye haki ya kuua mwingine

Wanaume nao waache ujinga wa kujimaliza
na wanapogundua wamepigwa waende kwenye sheria

Mwisho kabisa kama mwanamke mwenzangu ukihisi huna nia na mtu usile vyake
 
Yaani mkuu, mtu anaedundwa halafu anabaki huwa simuelewi na sitokaa nimuelewe. Hivi ile hofu tu ya kibinadamu hawana?. Yaani unakaa nyumba moja na mtu anakudunda hadi unazimia? Tena unalala nae kitanda kimoja. Watu wana mioyo jamani.
Sijawahi kuwaelewa na sitakuja kuwaelewa
 
Mimi naona kama 1-0 kama ni ndogo!!! Nadhani ni 3-0!!!!!!
 
Waache mahusiano na wanaume kabisa? Haiwezekani. Kumjua mwanaume ambaye anaweza kukutoa uhai pia ni ngumu. Mwanaume mwenye msongo wa mawazo haongei mengi na si mwepesi wa kukiri changamoto zake, hasa kwa mwanamke asiye msikivu. Kinyume chake, mwanamke anayepitia stress ni rahisi sana kumjua kwasababu atakua anaongea sana hisia zake, bila kujali madhara ya kauli zake. Reaction ya wanawake wa namna hii kwa wanaume zao wanaopitia stress kali mara nyingi huwa ni "makelele" na kauli za "maudhi". Baadhi wanakuendea mpaka ustawi wa jamii/kwa wanasheria kwa mambo ambayo hata hamjakaa kujadili kwa kina hapo ndani.

Hali hii hupeleakea ugomvi, na wakati mwingine, kutoana roho. Binafsi naamini suluhisho la kudumu la haya yote ni jamii kuelimika na kubadilika mitazamo yetu kuhusu nafasi zetu ktk mahusiano.
 
Kwani wewe una umri gani? Hauko umri mmoja na kina Mbaga Jr?
 
Mzee mwenzangu mbona umeandika kwa upande wa makosa ya wanawake tu? Unataka kusema kuwa wanaume huwa hawasababishi maudhi yoyote kwa wanawake ambayo yanaweza kasababisha migogoro kwenye ndoa au mahusiano?
 
Ushauri mzuri sana. Ubarikiwe
 
Baada ya mkutano wa Beijing 1995,wanawake mka ona mko sawa na wanaume kuanzia kifikra mpaka majukumu bila kuelewa kwamba mwanaume atabaki kuwa mwanaume.

Nyumba nying zina Kelele mno,wanaume ndo wahanga lakn huku nje inaonekana mwanamke anaonewa,unatoka kazin umechoka unafika home unapokelewa na kelele yan ni stress tupu,muda mwingine hizo kelele hujui chanzo chake hisia zake zikimtuma yeye ni kubwata tu,wanaume always hatupend kelele ndo mana weng mnaishia kupigwa au kuuliwa mana siku hiz hamuongei kwa adabu,hujui kutofautisha kuongea na mumeo na mfanyakaz wa ndan au mtoto wako.

Weng mna viburi huwez kumgombeza mumeo au kuongea hadharan mambo yakudhalilishana mbele za watoto au mfanyakaz wa ndan tena umenishikia kiuno aisee? Heshima kwa wanawake imeshuka,labda kwasababu na nyie mnavaa suruali kama sisi? Miaka 3 nyuma nikihudhuria sherehe ya jiran yangu yakumpongeza binti yao kumaliza chuo,ulipofika muda wa kutoa nasaha kwa wazaz Baba alimpongeza bintiye na kumpa zawad ilipofika zamu ya Mama,akaanza kumsihi mwanae asome zaid ya hapo na asiwaamin mana wanaume sio watu ahakikishe amepambana awe na pesa...aisee nilijisikia vibaya sana kwamba wamama wanaharibu watoto ebu pata picha anayomjengea binti yake? Huyu binti atakuwaje huko mbele? Heshima kwa mumewe itakuwepo?

Kama wanawake wameshindwa kujitambua wao wakina nan,hili janga la MAUJI halitokoma abadani. Mana tumeamua kuiga mfumo na utamadun wa kimagharibi,tukaacha mila na desturi za mwafrika kuwa mwanamke lazima awe mnyenyekevu kwa mumewe,lakn siku hiz ASASI za kigen zinafunguliwa kila siku zikijifanya kumpandia mwanamke ili hali linazid kuchochea moto mana MAFAHALI WAWILI hawawez kukaa ZIZI moja.
 
Wanataka wasiliwe pesa zao sasa ziliwe za nani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…