Mjamzito afariki kwa kukosa pesa ya mafuta gari la wagonjwa, wakati Mama ananunua magoli

Mjamzito afariki kwa kukosa pesa ya mafuta gari la wagonjwa, wakati Mama ananunua magoli

Mama enu hana makosa anaweka hela kule akili zenu zilipolala.
Usikute hata huyo mjamzito nae alikuwa anafurahiaga magoli yakinunuliwa
 
Kwa hiyo wewe ungekuwa dereva wa hiyo ambulance ungetoa fedha yako ununue mafuta?
kina vitu havihitaji hata kuuliza ndugu! ile aio starehe ya kwamba mtu anahitaji hiyo pesa akalewee ile ni shida inayohusu afya moja kwa moja!.
nyie kama mnaona kilichofanyika ni sahihi hizo ni peo zenu,lkn usije ukategemea rais akashuka akaja kukuambia kuwa huyu anahitaji msaada msaidie halafu swala la malipo baadae! unauliza kama vile hauna hekima mkuu!
 
umeelewa nilichoandika ama kusoma unajua ila kuelewa ni zero....????
ulitaka nieleweje ng'ombe wewe
nipo serikalini umeshawahi sikia Rc, dc au mkurugenzi au waziri, amekosa mafuta nyang'au wewe wao wana thamani kuliko watanzania wengine? yaani serikali wanakosa mafuta ya ambulance lakini mafuta ya kukimbiza mwenge yapo nyoka mkubwa wewe.
 
Ni masikitiko makubwa hivi ile Kizimkazi Festival ilitumia kiasi gani?!
Wakati anaupiga mwingi, kwa kununua magoli ya Yanga na Simba kuna watu wana safa sana kwa huduma za afya. Kule Kilosa Mama kafariki kwa kukosa pesa za mafuta ya Gari ya kubebea wagonjwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka ametoa siku tatu vyombo vya usalama kuchunguza tukio la mama mjamzito aliyefariki baada ya familia yake kukosa pesa za kuweka mafuta gari la wagonjwa.

Shaka alipokea tuhuma hizo kutoka kwa mume wa marehemu, Seleman Makuani wakati akisikiliza kero za wananchi katika Kata na Kijiji cha Kidodi, mkoani humo.

Hii hakuna anaye jali kabisa.


Utu, Upendo,na kujali ni changamoto kubwa kwa watanzania kuliko madhaifu ya serikali , na udhaifu wa serikali unadhidi siku Hadi siku kwa sababu Ina watendaji waliokosa utu,Upendo na kujali, kwa maana hiyo wa kuchunguzwa haraka haraka ni dereva wa ambulance, afisa usafilishaji wa hospital, DMO, na makatibu tawala wa hospital, kwa ufupi ushenzi siyo at the nation level,ila ni hospital husika ambako ndio wamiliki wa ambulance
 
Wakati anaupiga mwingi, kwa kununua magoli ya Yanga na Simba kuna watu wana safa sana kwa huduma za afya. Kule Kilosa Mama kafariki kwa kukosa pesa za mafuta ya Gari ya kubebea wagonjwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka ametoa siku tatu vyombo vya usalama kuchunguza tukio la mama mjamzito aliyefariki baada ya familia yake kukosa pesa za kuweka mafuta gari la wagonjwa.

Shaka alipokea tuhuma hizo kutoka kwa mume wa marehemu, Seleman Makuani wakati akisikiliza kero za wananchi katika Kata na Kijiji cha Kidodi, mkoani humo.

Hii hakuna anaye jali kabisa.
Inauma sana kumpoteza mpendwa wako. Hivi kweli serikali inashindwa kuwa mfuko wa dharura kwa ajili watu kama hawa?
 
Inamaana kumbe Ambulance huwa ni lazima ulipie kwanza? Sikuwahi kujua hiyo kitu, kumbe ni biashara za watu. Mimi nilikuwa najua endapo mgonjwa atazidiwa na inabidi kuhamishwa kwenda kituo kingine basi ambulance hutumika kama msaada wa haraka kufika huko bila malipo yoyote yale. Sasa hizo kodi tunazo lipa kila siku zinaenda wapi? Ambulance ilipaswa iwe bure kabisa sio kulipishana mafuta, dawa tulipie kodi tutoe hadi masuala ya dharura kweli! Hii nchi inasikitisha sana
 
Ila ujauzito ni mchakato maandalizi ya kujifungua ni muhimu sana hasa kwa wanaume tusiishie kutia mimba tu tuwajibike unakuta jitu linatia mimba Kila baada ya miaka miwili hospital akiambiwa achangie japo dawa na vipimo anakuambia Sina pesa inasikitisha sana.
Kweli mkuu, Hii changamoto yake ni elimu. Lazima kujipanga sio kujaza jaza tu kuna muda serikali inatupiwa lawama nzima wakati lawama inabidi iende pande zote
 
Haya mabango kila njia, hizo fedha zingetosha kusogeza huduma za afya karibu zaidi. Ni mwanamke anaongoza bado vifo vya wamama wajawazito, vya kizembe kukosa fedha za mafuta. Huku unajijaza kwenye mabongo!!! Ni aibu kubwa.
 
Wizara ya afya iangalie uwezekano wa kupunguza gharama za Ambulance!!
Route za ndani ya mji 60000,Moro-Dar 230000
Inatakiwa ilipwe yote ndo mgonjwa aondoke! Ni watanzania wangapi wanamudu?
Au basi ingewekwa kwenye Bill ya mgonjwa,yaani asafirishwe ndugu wakiwa wanatafuta pesa!
Wananchi ukiwaambia tuungane tuwajibishe serikali wanakwambia wao hawataki siasa
 
Daah So sad,ishu ya kununua magoli huwa naichukia sana hii nchi kuna shida sana yaan vitu vya kipuuzi vinapewa kipaumbele kuliko vitu vya maana
 
kwenye hili nitamtetea jamaa hata kama kujipanga ndio lkn 180000 hiyo nauli hata dar mwanza ni kubwa! hapa kuna namna ambulance imepewa wapigaji kuna upuuzi umefanyika kwa maksudi hapa!.
Niliwahi kuwa na jamaa yangu hospitali ya rufaa Morogoro aliyepata ajali ya pikipiki, inatakiwa aende Muhimbili kwa ambulance. Hapo kuna majeruhi wengine wawili wa ajali ya gari, wanaunganishwa wote kwenye ambulance na kila mgonjwa alitakiwa kutoa 350K. Yule jamaa yetu ilibidi tumpakie Abood kesho yake kwani kesi yake ilikuwa ni ya fracture tu ya mkono
 
Back
Top Bottom