Kinachoongelewa kinaweza kupambwa kwa lugha nzuri sana lakini ni ubaguzi unaofichwa kwa maneno matamu.
Vipi huyo Mbarawa kama angekuwa ni mtendaji mzuri katika hizo wizara, hizo fikra za kibaguzi zingezaliwa?, kuna mtu angekumbuka kuwa ni mzenji?.
Tutatue matatizo yetu bila ya kuitazama asili ya mtu. Ukibagua mtu leo ujiandae kesho kukabiliana na ubaguzi huo huo.
Hivi Ubaguzi upo wapi? Wazanzibar wanalalamika kuwa mambo ya muungano yameongezwa hadi 32
Wazanzibar hawawezi kuajiri Mtanganyika hata mfagiaji.
Huu ubaguzi mbona ni wa upande mmoja?
Ali Salehe wa ACT aliposimama na kusema ana furaha Mradi wa Bagamoyo umekufa, hilo unalionaje
Halafu hawa wenye chuki ndio wa kusaini mikataba ya 'nia' njema na Tanganyika
Kujiita Mzanzibar na si Mtanzania huo si ubaguzi, kujiita Mtanganyika ni ubaguzi. hee!
Lakini si ubaguzi ni ukweli. Kwamba hakuna Mtanganyika anayeweza kusimamia rasilimali za Zanzibar
Hivi si Wazanzibar waliondoa mafuta na gesi , wakaondoa Bandari kinyamela. Huo si ubaguzi!
Wazanzibar walioondoa gesi na mafuta walilinda rasilimali zao , huo unaona si ubaguzi.
Watanganyika kukumbuka Mwinyi alivyouza Liliondo kwa Waarabu na sasa wanauziwa bandari eti ni ubaguzi
Watanganyika wanapoona rasilimali zao zinasaiiniwa na Wazanzibar wale wale waliouza Liliondo kuna shida gani wao kusema. Hii si wizara ya muungano, hakuna ubaguzi.
Mbarawa ni wakati AJIUZULU sasa, Watanganyika hawana imani nawe katika mkataba wa Bandari