Mkataba wa kuendesha Bandari za Tanzania wa DP WORLD ya Dubai hautazihusu Bandari za Zanzibar
Tofauti yangu na baadhi ya watu humu ni huo unaoitwa upuuzi. Hauwezi kuelezewa kwa hoja zenye mantiki na ukaeleweka.

Huo unaoitwa upuuzi ni mradi ulioanza kutafutwa na serikali tangu 2015 mwishoni enzi za urais wa JPM, ni mkakati mpana sana wa kuipeleka nchi katika uchumi wa juu.

Hivyo namtetea Mbarawa kwani sioni mantiki ya yeye kuondolewa kazini zaidi ya chuki tu na roho zetu za kishenzi.
Kwani kitu kuanzishwa na JPM (hata kama ni kweli) ndo ticketi ya kutohojiwa?
 
Wazanzibar wapo bungeni pale Dodoma na sio mmoja wapo wengi tu, kuna kosa kuteua mmoja wao na kumpa uwaziri huku Tanganyika?.

Kuchanganya udongo sio mzaha, labda kwa sababu sisi ni watanzania wa leo hivyo hatuwezi kuona maana ya kitendo kile.

..Waznz wako ktk bunge la Jamhuri kama wawakilishi wa Znz, haki, na maslahi yao.

..Ni sahihi kuwateua ktk wizara za muungano kama fedha, mambo ya nje, mambo ya ndani.

..Ni makosa kuteua Mznz ktk wizara zisizo za muungano, yaani za Tanganyika, kama ujenzi, mifugo, maji.

..Kama kuchanganya udongo ingekuwa ni jambo kubwa sana basi tusingekuwa na KATIBA.

..Kama tumeandika KATIBA basi ni muhimu tukaiheshimu.
 
Mengi uliyoandika yana msingi wa maneno ya kusikia kwa watu, ambao ni kielelezo cha chuki unayoitunza moyoni mwako.
Mwinyi hakuuza Lliondo? Kaandika kitabu akisikitika baada ya kutoa sadaka rasilimali za Tanganyika.
Vipi kuhusu wizi anaoibua CAG kila siku na wenyewe unawahusu wazanzibari?, tunasahau kuwa huku bara tuna kesi zetu za wizi na ushahidi halisi anauweka wazi CAG kila siku.
Huo ni wizi hata kule Zbar CAG kaonyesha
Hao wazanzibar wanaosaini na bandari wapo pale kikatiba hawajajiweka mahali pale. SSH ni mgombea mwenza wa JPM na iwapo asingefariki mpaka leo angekuwa na cheo chake kile kile.
Ni hawa hawa Wanaodai mambo ya muungano yameongezwa na hawataki. Wanasema kuongeza mambo hayo kunawanyima fursa. Leo wanatumikia nafasi za mambo yale yale wasiyoyataka. Mbarawa na Shaka DC ni mifano tu. Huwezi kuwa na Tanganyika ya yote halafu Zanzibar yao.
Chuki zinazoenezwa na Wazanzibar ndizo chanzo , Watanganyika walikuwa kimya muda mrefu sana na kuonekana Wajinga. Hiyo Wizara si ya muungano, Mbarawa anasaini mikataba isiyomhusu, hatuna imani naye
Huu ni muungano halisi ambao Mwalimu Nyerere aliunganisha udongo wa pande mbili, matatizo yote ya kikatiba yanaongeleka na kutatulika.
Wazanzibar hawautaki. Othman Masoud Othman(OMO) juzi kasema muungano si '' Faradhi au Suna'' wanaweza kuvunja tu. Kila siku akina Jussa na OMO wapo majukwaani kuwaalani Watanganyika. Hakuna adui yao mkubwa zaidi ya Tanganyika. Tunawasikili tunawasoma. Tunawasikia tunawasoma .
Leo wakimbize gesi na mafuta kwao, halafu bandari za Tanganyika ni za wote! nope, ujinga huo utabaki na wachache wanaolamba asali
Tuachane na hizi nongwa kwamba eti SSH anasaini mkataba mkubwa wa nchi akiwa mzanzibari, huyo ni rais wa awamu ya sita hasaini pale kama mtu tu baki.
Hoja hapa ni kuwa Rais SSH yupo kikatiba. Huyu anaye negotiate na kusaini yupo kikatiba tu lakini anashughulikia jambo lisilo la muungano. Mwinyi aliuza Loliondo kwasababu hakuwa na uchungu na Tanganyika .
Kuvuja kwa document kunaonyesha kitu! fikiria
Tujadili masuala positive yenye kujenga nchi sio hizi chuki na nongwa zinazojaa mioyoni na kuanza kuonekana muda huu. Huyo Mbarawa leo anaonekana mbaya vipi kuhusu miradi mingi aliyoifanikisha wakati wa JPM?.
Waambie wazanzibar wanaoneza chuki. Mwambie Makamu wa Rais na Makamu wa ACT bwana OMO na akina Jussa waache chuki. Huwezi kuwa na chuki halali akisema mzanzibar, haramu akisema Mtanganyika

Waombe kura ya maoni, wakifanikiwa waondoke tu salama !
Vipi kuhusu ufanisi wake wa kazi uliompa ubunge na uwaziri?, Tuache kufuga chuki na ubaguzi vitakuja kutugeuka siku moja.
Ufanisi unaujua wewe, sisi tunaangalia rasilimali na tushaumwa na nyoka kupitia AH Mwinyi.
 
Hapa ni kuonyesha eti bara tumependelewa sana ilikuondoa lile la swali la kwann za zenj hazijaunganishwa
Kwenye language wanaita ironing language yaani unampa sifa mtu kinyume chake🤣🤣🤣
Hao ni vijana wa chadema
 
..Waznz wako ktk bunge la Jamhuri kama wawakilishi wa Znz, haki, na maslahi yao.

..Ni sahihi kuwateua ktk wizara za muungano kama fedha, mambo ya nje, mambo ya ndani.

..Ni makosa kuteua Mznz ktk wizara zisizo za muungano, yaani za Tanganyika, kama ujenzi, mifugo, maji.

..Kama kuchanganya udongo ingekuwa ni jambo kubwa sana basi tusingekuwa na KATIBA.

..Kama tumeandika KATIBA basi ni muhimu tukaiheshimu.
Mwambie hivi, ni hawa Wazanzibar hawakuheshimu katiba ya 1977 walipobadili katiba yao 2010.
Hawana heshima na Tanzania, leo tuwe na imani nao!

Yasiyo ya muungano wakae pembeni. Ni makosa Mzanzibar kutumikia nafasi yoyote isiyo katika mambo ya muungano. Wazanzibar wenyewe wanasema hivyo kwa kauli ya kuongezwa mambo ya muungano.
 
Point ya rasilimali za Tanganyika haina mashiko, huyo Mbarawa katimiza miradi mingapi huku bara?, Mbona huyo haiongelewi?. Hiyo miradi aliyoimaliza na sasa inahudumia wananchi sio sehemu ya rasilimali za taifa hili?. Chuki na roho mbaya ni tatizo linaloitesa Tanzania ya leo hii.
Hii haimpi fursa 'kuuza nchi' . Kama kafanya hivyo alilipwa mshahara na ni makosa kwasababu hayakuwa mambo ya muungano. Tunasema sasa kwamba inatosha, tuheshimu maamuzi ya Wazanzibar wanaolalamika kuongezwa mambo ya muungano. Katika yasiyo ya muungano waondoke kama ambavyo hakuna Mtanganyika ndani ya SMZ. Unabisha nini wakati katiba inasema kuna ya muungano na yasiyo ya muungano.
Wanaomteua kumpa vyeo na kumlipa mshahara ni mpaka watakapochoka au kumuona hafai ndio wataamua kuachana nae, sio kwa hizi hoja nyepesi za jukwaa hili.
Hatuna imani naye, tutasema. Ataendelea kuwepo pale lakini ajue watu hawana imani na yeye!
Amekuwa distractions katika mambo muhimu, akae pembeni kama Job Ndugai.
Hili si jambo la muungano, hatuna upungufu wa watu wenye uwezo na uchunguna Tanganyika.
Mbarawa ajiuzulu ili kuondoa mijadala hii, akae pembeni hili ni la Tanganyika na Wazanzibar wanasema hivyo

Wazanzibar hawataki kuitwa Watanzania leo unasema si ubaguzi huo. Yasiyo ya muungano wakae pembeni
 
Akili zile zile zilizokemewa na Mwalimu Nyerere, akili za chuki dhidi ya wazanzibari. Tunasahau kuwa wakiondoka hao wazenji adui mpya wa kubaguliwa atakuwa ni wa kabila la jirani yako na jirani yangu.
Ubaguzi huo tumeanza sisi au wao.
Katika Mambo ,22 ya muungano, moja Ni la bandari. Hawa wazanzibari kwa makusudi kabisa wanauza bandari za Tanganyika na kuacha za Zanzibar. Kwa maana hiyo Sasa hivi Mambo ya muungano yatakua 21 badala ya 22.
Kwanza ujue hapo katiba pia imevunjwa.
Anyway, inahitaji upeo mkubwa na MTU anae ijua katiba ya nchi kuyaona haya Mambo.
 
Back
Top Bottom