Mengi uliyoandika yana msingi wa maneno ya kusikia kwa watu, ambao ni kielelezo cha chuki unayoitunza moyoni mwako.
Mwinyi hakuuza Lliondo? Kaandika kitabu akisikitika baada ya kutoa sadaka rasilimali za Tanganyika.
Vipi kuhusu wizi anaoibua CAG kila siku na wenyewe unawahusu wazanzibari?, tunasahau kuwa huku bara tuna kesi zetu za wizi na ushahidi halisi anauweka wazi CAG kila siku.
Huo ni wizi hata kule Zbar CAG kaonyesha
Hao wazanzibar wanaosaini na bandari wapo pale kikatiba hawajajiweka mahali pale. SSH ni mgombea mwenza wa JPM na iwapo asingefariki mpaka leo angekuwa na cheo chake kile kile.
Ni hawa hawa Wanaodai mambo ya muungano yameongezwa na hawataki. Wanasema kuongeza mambo hayo kunawanyima fursa. Leo wanatumikia nafasi za mambo yale yale wasiyoyataka. Mbarawa na Shaka DC ni mifano tu. Huwezi kuwa na Tanganyika ya yote halafu Zanzibar yao.
Chuki zinazoenezwa na Wazanzibar ndizo chanzo , Watanganyika walikuwa kimya muda mrefu sana na kuonekana Wajinga. Hiyo Wizara si ya muungano, Mbarawa anasaini mikataba isiyomhusu, hatuna imani naye
Huu ni muungano halisi ambao Mwalimu Nyerere aliunganisha udongo wa pande mbili, matatizo yote ya kikatiba yanaongeleka na kutatulika.
Wazanzibar hawautaki. Othman Masoud Othman(OMO) juzi kasema muungano si '' Faradhi au Suna'' wanaweza kuvunja tu. Kila siku akina Jussa na OMO wapo majukwaani kuwaalani Watanganyika. Hakuna adui yao mkubwa zaidi ya Tanganyika. Tunawasikili tunawasoma. Tunawasikia tunawasoma .
Leo wakimbize gesi na mafuta kwao, halafu bandari za Tanganyika ni za wote! nope, ujinga huo utabaki na wachache wanaolamba asali
Tuachane na hizi nongwa kwamba eti SSH anasaini mkataba mkubwa wa nchi akiwa mzanzibari, huyo ni rais wa awamu ya sita hasaini pale kama mtu tu baki.
Hoja hapa ni kuwa Rais SSH yupo kikatiba. Huyu anaye negotiate na kusaini yupo kikatiba tu lakini anashughulikia jambo lisilo la muungano. Mwinyi aliuza Loliondo kwasababu hakuwa na uchungu na Tanganyika .
Kuvuja kwa document kunaonyesha kitu! fikiria
Tujadili masuala positive yenye kujenga nchi sio hizi chuki na nongwa zinazojaa mioyoni na kuanza kuonekana muda huu. Huyo Mbarawa leo anaonekana mbaya vipi kuhusu miradi mingi aliyoifanikisha wakati wa JPM?.
Waambie wazanzibar wanaoneza chuki. Mwambie Makamu wa Rais na Makamu wa ACT bwana OMO na akina Jussa waache chuki. Huwezi kuwa na chuki halali akisema mzanzibar, haramu akisema Mtanganyika
Waombe kura ya maoni, wakifanikiwa waondoke tu salama !
Vipi kuhusu ufanisi wake wa kazi uliompa ubunge na uwaziri?, Tuache kufuga chuki na ubaguzi vitakuja kutugeuka siku moja.
Ufanisi unaujua wewe, sisi tunaangalia rasilimali na tushaumwa na nyoka kupitia AH Mwinyi.