Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Ikiwa tuna SMZ na BLW na sheria zinazowahusu, Mtanganyika anasimama wapi?Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania. Kwenye uraia wa Tanzania, raia wote wana haki sawa, hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, tuna Mtanzania tuu, hivyo hoja hii ni ubaguzi.
P
Wazanzibar hawajitambulishi kwa Utanzania ni pale tu penye mafao
Hoja ya Wazanzibar wang'oke au wang'olewe katika taasisi na wizara zisizo za muungano si yangu ni ya Wazanzibar wenyewe.
Kwa muda mrefu Wazenji wamelalamika kukiukwa kwa mambo yaliyopo katika mkataba.
Makama wa Rais Othman Masoud Masoud (OMO) ambaye pia aliwahi kuwa AG wa SMZ anasema, mambo ya muungano yameongezwa kutoka 11 hadi 22 na yakinyumbuliwa yanafikia 36.
Wazanzibar wanasema ongezeko hilo limelenga kuwanyonya kiuchumi na kuwanyima fursa.
Ni kwa mantiki hiyo tunasikiliza hoja za Wazanzibar, yale yasiyo ya muungano waondolewe.
Wazanzibar wana hoja, kwanini waajiriwe maeneo yasiyo ya muungano? Huko ni kuwadhulumu
Pili, ikiwa Wazanzibar wanapinga hawaajiri Mtanzania kwasababu ni Mtanganyika kule visiwani, ni wakati sasa vijana wa Tanganyika wanaotembea na bahasha za khaki wapewe fursa katika taasisi na wizara zisizo husu muungano nao wanufaike na keki ya Tanganyika kama wenzao wa Zanzibar.
Wazanzibar pia waheshimu haki za Watanganyika kwa kuachia nafasi zao.
Huwezi kudai haki wakati huo huo unadhulumu watu haki zao.
Tunaheshimu hoja zao lakini sasa ni wakati Wang'olewe, si ubaguzi ni matakwa yao na tunawaheshimu.
Uzima Tele JokaKuu