Mkataba wa kuendesha Bandari za Tanzania wa DP WORLD ya Dubai hautazihusu Bandari za Zanzibar
Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania. Kwenye uraia wa Tanzania, raia wote wana haki sawa, hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, tuna Mtanzania tuu, hivyo hoja hii ni ubaguzi.
P
Ikiwa tuna SMZ na BLW na sheria zinazowahusu, Mtanganyika anasimama wapi?
Wazanzibar hawajitambulishi kwa Utanzania ni pale tu penye mafao

Hoja ya Wazanzibar wang'oke au wang'olewe katika taasisi na wizara zisizo za muungano si yangu ni ya Wazanzibar wenyewe.

Kwa muda mrefu Wazenji wamelalamika kukiukwa kwa mambo yaliyopo katika mkataba.

Makama wa Rais Othman Masoud Masoud (OMO) ambaye pia aliwahi kuwa AG wa SMZ anasema, mambo ya muungano yameongezwa kutoka 11 hadi 22 na yakinyumbuliwa yanafikia 36.

Wazanzibar wanasema ongezeko hilo limelenga kuwanyonya kiuchumi na kuwanyima fursa.

Ni kwa mantiki hiyo tunasikiliza hoja za Wazanzibar, yale yasiyo ya muungano waondolewe.
Wazanzibar wana hoja, kwanini waajiriwe maeneo yasiyo ya muungano? Huko ni kuwadhulumu

Pili, ikiwa Wazanzibar wanapinga hawaajiri Mtanzania kwasababu ni Mtanganyika kule visiwani, ni wakati sasa vijana wa Tanganyika wanaotembea na bahasha za khaki wapewe fursa katika taasisi na wizara zisizo husu muungano nao wanufaike na keki ya Tanganyika kama wenzao wa Zanzibar.

Wazanzibar pia waheshimu haki za Watanganyika kwa kuachia nafasi zao.

Huwezi kudai haki wakati huo huo unadhulumu watu haki zao.

Tunaheshimu hoja zao lakini sasa ni wakati Wang'olewe, si ubaguzi ni matakwa yao na tunawaheshimu.

Uzima Tele JokaKuu
 
Ikiwa tuna SMZ na BLW na sheria zinazowahusu, Mtanganyika anasimama wapi?
Wazanzibar hawajitambulishi kwa Utanzania ni pale tu penye mafao

Hoja ya kwamba Wazanzibar wang'oke au wang'olewe katika taasisi na wizara zisizo za muungano si yangu ni ya Wazanzibar. Kwa muda mrefu Wazenji wamelalamika kukiukwa kwa mambo yaliyopo katika mkataba.
Makama wa Rais Othman Masoud Masoud (OMO) ambaye pia aliwahi kuwa AG wa SMZ anasema, mambo ya muunagano yameongezwa kutoka 11 hadi 22 na yakinyumbuliwa yanafikia 36.
Wazanzibar wanasema ongezeko hilo limelenga kuwanyonya kiuchumi na kuwanyima fursa.

Ni kwa mantiki hiyo tunasikiliza hoja zao, yale yasiyo ya muungano waondolewe.
Pili, ikiwa Wazanzibar wanapiga hawaajiri Mtanzania kwasababu ni Mtanganyika, ni wakati sasa vijana wa Tanganyika wanaotembea na bahasha za khaki wapewe fursa katika taasisi na wizara zisizo husu muungano.

Wazanzibar pia waheshimu haki za Watanganyika kwa kuachia nafasi zao. Huwezi kudai haki wakati huo huo unadhulumu watu haki zao. Tunaheshimu sana hoja zao lakini sasa ni wakati Wang'olewe, si ubaguzi ni matakwa yao na tunawaheshimu.

Uzima Tele JokaKuu

Mkataba huu hautatuliki bila kwanza kutatua suala la katiba, Muungano, Tume huru etc
 
Si bungeni wala mitandaoni nimewasikia au kuwasoma wa Zanzbari wakilalamika(kama ilivyo kawaida yao} kusahaulika katika neema na uhondo tunaoambiwa na Mzanzibari mwenzao utaletwa na ujio wa DP World katika bandari zetu> Kulikoni?
 
Si bungeni wala mitandaoni nimewasikia au kuwasoma wa Zanzbari wakilalamika(kama ilivyo kawaida yao} kusahaulika katika neema na uhondo tunaoambiwa na Mzanzibari mwenzao utaletwa na ujio wa DP World katika bandari zetu> Kulikoni?
Mambo ya Tanganyika hayawahusu, wao mambo yao safi kabisa.
 
Wanasema wanaupenda muungano[emoji16]

Unajua kwanini makatibu wakuu,mawaziri, wakurugenzi wakuu wa wilaya wakuu wamashirika wengi wanatokea Zanzibar
 
Mambo ya Tanganyika hayawahusu, wao mambo yao safi kabisa.
Bandari ni mojawapo ya mambo 22 ya Muungani na halijaondolewa bado si la Tanganyika peke yake. Kama vile wanavyodai wapate mgao wa misaada na mikapo inayotoka nje mbona katika hili la bandari kupewa DP World ambapo tunaambiwa kuna faida nyingi kwa nini hawalalamiki hawalalamiki kuwa wamesahauliwa?
 
Wanasema wanaupenda muungano[emoji16]

Unajua kwanini makatibu wakuu,mawaziri, wakurugenzi wakuu wa wilaya wakuu wamashirika wengi wanatokea Zanzibar
Si mumetawala nchi hii kwa miaka yote hiyo tena munataka nini?
 


Majibu yote haya hapa
 
Is it a planned conspiracy theory?!
Acha niendelee kumsikiliza profesa wangu Bob Marley na lecture za Time Will Tell na Redemption Songs
 
Wamechoka kulalamika, machozi yamekauka sasa wanatumia mbinu nyingine.
Usiwe na wasiwasi nyie endeleeni kujadili DP-W
 
Mama Tibaijuka kasema kutokana na mkataba Zanzibar nayo imo, sasa mbona mnatuchanganya.
 
Wanaotaka DP World waje Kuwekeza Bandarini Tanzania tujuane na wale Wasiotaka Wawekeze wajuane pia.

Kuanza na Mimi GENTAMYCINE baada ya Kupima, Kusoma, kuufanyia Utafiti mdogo tu huku nikijiridhisha na Ufanisi wao na kwa Maendeleo chanya kwa Taifa Kiuchumi, Kimaendeleo na Kiajira leo natamka rasmi kuwa Mimi sasa ni TEAM DP WORLD WAWEKEZE Tanzania.

Naomba niwajue na Wenzangu pia. Na ukiona GENTAMYCINE nakubali Kitu jua kipo sahihi kwa 100% kwani Mwenyezi Mungu kanibariki na Maono makubwa, Hisia Kali na Utambuzi wa haraka hivyo DP World hawana baya wala tatizo tuwakaribisheni tu.
 
Back
Top Bottom