Mkoa wa Pwani watoa Mawaziri watano kwenye baraza jipya; ni bahati mbaya au ndiyo tuseme sasa zamu ya watu wa Pwani?

Nauliza hivi,kwani ukitoa Waziri na mwingine asitoe Waziri waliotoa watafaidikaje na wasiotoa wataathirikaje?

Natoa mfano ,mwaka ujao kuna mradi wa Tactic unaanza awamu ya kwanza ni miji na Manispaa 13 tuu zitakuwemo,Mbona Manispaa ya Sumbawanga itakuwemo ilhali hakuna hata Naibu wala Katibu Mkuu wala Waziri kutoka mkoa huu?

Hizo dhana za kipumbavu zinaendekezwa na wajinga,kwani mkoa wenye mawaziri wengi kuna nini cha maana cha kimaendeleo?
 
Kwa kutokuwa na mawaziri au Naibu wamepata hasara gani?
 
Hapa ndipo watu wanapotandikwa Kata Funua wanabaki wanashangaa huku wakiwa hawaamini

Yaani hadi kesho kuna watu wanamchukulia Samia "she's just a woman" anaepangiwa cha kufanya

Hivi mtu na akili yako unaamini kabisa SSH kama Rais atapangiwa baraza na mtu mwingine, na mtu mwingine mwenyewe ni mstaafu!!

Yaani watu hadi wanakuja kushtuka kwamba kumbe "tuna rais" na sio "rais mwanamke", wengi watakuwa wameumia sana...

Hivi zile story za "Hawa watu unatakiwa kuishi nao kwa akili" mnadhani zinaishia kwenye mapenzi tu?!
 
Hao wote ni mikoa tofauti. Wasukuma kuwa 4 Mawaziri ni sawa Sukumaland inamikoa mitano so ni eneo kubwa na watu wengi.
Sasa inakuaje itoe mawaziri wote hao kwenye kabila moja Kisa wanatoka mikoa tofauti ambayo nayo inakaliwa na kabila moja?.

Unaona ina make sense kwa mujibu wa hoja yako ya kimbuzi mbuzi?
 
Wapumbavu ni wengi Sana Nchi hii mkuu.
 
NA hakuna cha maana cha maendeleo huko ,ndio maana wajinga unawapuuza tuu, mawaziri sio wawakilishi wa mikoa.
 
Ndio maana tupo tulipo
Tunarudi nyuma sanaaaa
Kulipana fadhila
 
Samia ni mdini na mbinafsi.Nchi imemshinda hii.
 
Dodoma kuna watatu! Nalo ni tatizo? Nadhani tujikite kwenye uwezo wa wahusika.
 
Madhara yake unayajua ila pengine hutaki kuongea wakati wa kula.
Madhara ni yapi? Akili visoda mna.shida..

Umeulizwa Kigoma ina kuanzia VP, mawaziri kama.wote,chief secretary,Makatibu Wakuu kibao ehee ina nini kikubwa kuizidi Rukwa au Njombe kusiko na mawaziri?
 
Madhara ni yapi? Akili visoda mna.shida..

Umeulizwa Kigoma ina kuanzia VP, mawaziri kama.wote,chief secretary,Makatibu Wakuu kibao ehee ina nini kikubwa kuizidi Rukwa au Njombe kusiko na mawaziri?
Kama haina faida, waachie basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…