Mkoa wa Pwani watoa Mawaziri watano kwenye baraza jipya; ni bahati mbaya au ndiyo tuseme sasa zamu ya watu wa Pwani?

Mkoa wa Pwani watoa Mawaziri watano kwenye baraza jipya; ni bahati mbaya au ndiyo tuseme sasa zamu ya watu wa Pwani?

Onyesha basi hiyo National representation imekosekana wapi? Tuna mikoa 31, hebu tuonyeshe mapungufu yapo wapi?
Hivyo unamaanisha mikoa mingine kama Mara, Shy haina watu wa kuwa Mawaziri ila pwani na Tanga ndiyo wanasifa
 
Mkoa mzima wa Arusha kuna naibu waziri mmoja tu;
Mkoa mzima wa Manyara kuna naibu waziri mmoja tu.
Hivi mkoa wa Morogoro kuna naibu waziri hata mmoja?

Mkoa wa Tanga kuna mawaziri watatu.

Mkoa wa Pwani ndio kama alivyoonyesha mleta mada.

Hivi tunapeleka wapi nchi katika pande hizo za kisiasa?
Badala ya kurekebisha makosa tunaendeleza kwa kulipisa kisasi?
Tunataka kuwaachia watoto na wajukuu nchi ya namna gani?
Baraza la Mawaziri la Pwani na Zanzibar.
 
Enzi zile sasa
1. Bitteko-home kabisa
2. Kalemani- Wa sebuleni
3. Mabula- wa nyumbani
Achana na hao wa Shinyanga sijataka kuwajumuisha.
Hao wote ni mikoa tofauti. Wasukuma kuwa 4 Mawaziri ni sawa Sukumaland inamikoa mitano so ni eneo kubwa na watu wengi.
 
Hahahah!!!!dawa chungu lkn mtainywa tu,wakat wa yule jambazi wenu hamkuyaona co???
Sijajua hasa kigezo cha kuteua mawaziri ni nini lakini kuna mikoa haina waziri hata mmoja na mikoa mingine mawaziri 5.

Kwa mfano, mkoa wa Tanga ina mawaziri 3, Pwani ina mawaziri 5 huku mara ikiwa na Naibu waziri mmoja.

Angalia mfano hapa Pwani.
1. Dr. Jaffo..kisarawe
2. Mchengelwa..Rufiji
3. Ridhiwani..Chalinze
4. Ulega..mkuranga
5.kipanga..mafia

Mwanza ni mkoa wa pili kwa pato la Taifa Tanzania, una waziri mmoja wa Ardhi. Je Pwani ni bora sana kuliko Mwanza?

Ukija kwenye utenguliwaji, wote wanaotenguliwa ni wafuasi wa Issa Bim Mariam, Chamriho, Kalemani, Ndungulile, Job Ndugai, Waitara, Lukuvi, Mkumbo, Mwambe, Prof Majalala na wanaoteuliwa wote ni wa Uarabuni.

Ama mama amekuja kuhakikisha watu wa upande wake wanapendelewa?
 
Hakuna palipo andikwa ulazima wa kila mkoa kutoa waziri.

Mwacheni mkuu wa nchi afanye anavyo jisikia maana tukisema tunahitaji katiba mpya mnaanza kumbwela mbweela
Kuna wakati nawaonea hiruma ccm, ila ukigusa katiba mpya, nasema, ACHA WAISOME NAMBA, maana wanadhani katiba wao haiwahusu.
 
2025 nani anafika? Marehemu wanaotembea.
Ishi maisha ya ucha Mungu leo kesho si yako. Hukumu ipo
 
Kuna wakati nawaonea hiruma ccm, ila ukigusa katiba mpya, nasema, ACHA WAISOME NAMBA, maana wanadhani katiba wao haiwahusu.
Huo ndiyo ujinga uliowaingia akilini mwao.

Wanakuwa kama kuku au bata yaani hawachelewi kusahu
 
Kiufupi watu wa pwani wanaupiga mwingi na ndio wenye chama cha CCM. Mzanaki mwenzangu aliwekwa tu pale.

Zama zinabadilika sana kutoka Sukuma Gang mpaka Pwani Gang.
 
1. Ridhiwani Kikwete Mbunge wa Chalinze

2. Mchengelwa Mbunge wa Rufiji

3. Jafo Mbunge wa Kisarawe

4. Kipanga Mbunge wa Mafia

5. Juma Ulega Mbunge wa Mkuranga

Je, upi mchango wa mkoa wa Pwani kwenye uchumi wa Tanzania? Upi mchango wa Pwani kwenye kura za Uchaguzi Tanzania? Upi mchango wa Wabunge Hawa kwenye mikakati ya Taifa?

Lakini pia nikimaliza kushangaa Pwani najiuliza ni kweli sub ya Mchengelwa pale ofisi ya RAIS Utumishi ni Jenister Mhagama? Kwamba Jenister akatatue changamoto za Utumishi nchini?
Umesahau na jirani zao Tanga. Kuna zaidi ya watatu
 
Back
Top Bottom