Tetesi: Mkutano Mkuu wasogezwa ni tarehe 16/08/2025, something big with part chaja

Nadhani Msoga ndiyo chanzo cha kila shida
Tatizo linaanzia hapa watu kujitengenezea utawala wa kifalme
20250721_125833.jpg
 
MAMBO YA MKATO YA SHEIKH ABOUD JUMBE MWINYI YALIVYOMUHARIBIA, KUJIRUDIA TAREHE 18 AUGUST 2025 KWA SAMIA ?

HISTORIA :

Ugomvi wa Aboud Jumbe na Nyerere ulivyotetemesha nchi-5​

November 24, 2015

Na Elvan Stambuli

Kama nilivyosema wiki iliyopita, hatua ya kwanza iliyoanza kutikisa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ni pale Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Damian Lubuva aliporejeshwa Tanzania Bara na badala yake Rais Aboud Jumbe akateua raia wa Ghana, Alhaj Bashir K. Swanzy na kumpa uraia kushika wadhifa huo, Endelea…

Kuanzia hapo, madai ya Wazanzibari kutaka mabadiliko ya Katiba, kupitia mihadhara, magazeti na redio yalipamba moto.

Kukaanzishwa ‘redio pori,’ wengi watakumbuka matangazo ya redio hiyo ya mafichoni ambayo ilipachikwa jina la KIROBOTO TAPES ya kudai Wazanzibari warejeshewe visiwa vyao.

Ni mashushushu wa kijeshi wa bara ndiyo waliogundua baadaye kuwa ipo msituni, ikazimwa, sikumbuki kama kuna watu walifikishwa mahakamani kwa kumiliki redio hiyo.

Kwa kupitia Mghana, Jaji Bashir Swanzy, Serikali ya Jumbe iliandaa hati ya mashtaka kuhoji muundo na uhalali wa Muungano kwenye Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo kazi yake pekee, kwa mujibu wa ibara ya 126 ya Katiba ya Muungano ya 1977, “ni kusikiliza shauri lililoletwa mbele yake na kutoa usuluhishi juu ya suala lolote linalohusika na tafsiri ya Katiba, iwapo tafsiri hiyo au utekelezaji wake unabishaniwa kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.”

Hati hiyo ya mashtaka ‘ilipotea’ mezani kwa Rais Aboud Jumbe katika mazingira ya kutatanisha sana na kuibukia mikononi mwa Mwalimu Nyerere Msasani Dar es Salaam!

Taarifa za uhakika zinaonesha kuwa waliofanikisha kazi ya kuiba hati hiyo na kuipeleka kwa Mwalimu Nyerere ni baadhi ya vigogo ambao sasa wako katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wakati ule wakiwa SMZ.

Haraka Mwalimu Nyerere aliitisha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mjini Dodoma, Januari 1984 na Rais Aboud Jumbe akabanwa kwa madai ya kutaka kuuvunja Muungano kwa kuuhoji.

Nchi ikatangaziwa kwamba kuna “Kuchafuka Kwa Hali ya Hewa ya kKsiasa Zanzibar.”

Rais Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi mbele ya kikao alihojiwa na NEC na bila kumung’unya maneno, Sheikh Jumbe alikiri kuandaa hati hiyo kama moja ya haki zake za kikatiba, jambo ambalo lilizidi kumtibua Mwalimu Nyerere.

Usikose kusoma muendelezo wa makala haya wiki ijayo...

NONDO ZA ZIADA KUHUSU KADHIA YA SHEIKH JUMBE

View: https://m.youtube.com/watch?v=r9ZQGyVcuW4

UJASIRI WA KUHOJI WA 1984 UTAJIRUDIA TAREHE 18 AUGUST 2025 ?

View attachment 3413390
AEn0k_ttSRrPZfcvsSszSzUsCPvEysD27kUOlChfkxfS3O617XCr42hi0OyxXzHtSbRmvZFYCpGQB5qmdwuoNaErhcuRvQphm8Rx024r2rnHGoBPu7sWAxlMFKlheGtuuGefYsu2xxoodGNh1w=s0-d

Alikuwa pia mwasisi wa Muungano ulioizaa Tanzania miezi michache baadaye. Baada ya Sheikh Abedi Amani Karume kuuawa mwezi Aprili 1972, Jumbe aliteuliwa kuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, na alishikilia madaraka hayo hadi Januari 1984.

Wasomi wa Muungano wameandika kwamba, wakati Rais Karume anauawa, uhusiano wake na Mwalimu Julius Nyerere ulikuwa umeharibika kiasi kwamba Jumbe (kwa upande wa Zanzibar) na Bhoke Munanka (kwa upande wa Tanganyika) ndio walikuwa kiunganishi cha mawasiliano kati ya Mwalimu na Karume.

Hii pengine ndio sababu Mwalimu alitumia ushawishi wake kuhakikisha Jumbe anateuliwa kumrithi Karume.

Hata hivyo, Jumbe atakumbukwa zaidi na historia kwa upinzani wake kwa mfumo wa sasa wa Muungano kuliko, pengine, kwa jambo jingine lolote.

Jumbe alikuwa mwanasiasa wa kwanza, baada ya era ya (uongozi wa) Karume, kutambua kwamba muundo wa serikali mbili ulikuwa umeipokonya Zanzibar mamlaka yake na kuyahamishia Tanganyika.

Alikuwa wa kwanza kutambua kwamba, kuzaliwa kwa CCM katika context (mtazamo) ya Muungano, kulimaanisha mwisho wa mamlaka yaliyokuwa Zanzibar chini ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964.

Sio tu alitambua bali pia Jumbe alichukua hatua kupinga Zanzibar kupokonywa mamlaka yake hayo.

Ili kufanikisha azma yake, Jumbe alilazimika kumwachisha kazi Mwanasheria Mkuu wake aliyempewa na Mwalimu Nyerere, Damian Lubuva, na kumwajiri Bashir Ebassuah Kwaw Swanzy, Raia wa Ghana, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Kwaw Swanzy ndiye aliyeandaa ‘hati ya mashtaka’ dhidi ya Muungano iliyokamatwa na watu wa usalama wa Mwalimu na baadaye kutumika kumsulubu Jumbe kwenye kikao cha NEC ya CCM Dodoma Januari 1984. Kwa sababu ya upinzani huo, Jumbe aling’olewa madarakani pamoja na Waziri Kiongozi wake Ramadhani Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Kwaw Swanzy alitangazwa kufukuzwa nchini.

Mwalimu akatangaza ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa’ Zanzibar na Wazanzibari wengi wapinzani wa Muungano, kama Mwanasheria Mkuu wa kwanza Wolfgang Dourado, kuwekwa kizuizini.

Miaka 10 baada ya kuondolewa madarakani, Alhaj Aboud Jumbe alichapisha kitabu chake juu ya Muungano, ‘Miaka Thelathini ya Dhoruba’, ambako aliweka bayana ugomvi wake na Mwalimu juu ya Muungano.

Jumbe ni kiongozi pekee wa juu wa rika la wapigania uhuru wa Tanzania kuandika memoirs zake juu ya Tanzania na matatizo ya Muungano wake.

Hata Mwalimu hakufanya hivyo na alikufa na siri zake juu ya mambo mengi makubwa yalitokea wakati wa utawala wake.

Kwangu mimi, hii ndio merit (faida) kubwa na mchango mkubwa wa Alhaj Aboud Jumbe kwa kizazi cha sasa na vijavyo Tanzania.

Alikuwa na ujasiri wa kusema na kuandika juu ya ‘The Forbidden Subject’, tena katika kipindi cha Mwalimu Nyerere ambapo ujasiri wa aina hiyo ulikuwa ni jambo la hatari kubwa.

Kwa sababu hiyo hiyo, Jumbe alilazimika kuishi theluthi ya mwisho ya maisha yake ‘kifungoni’ Mji Mwema, Kigamboni, ambako alipelekwa mara baada ya kung’olewa madarakani mwaka ’84.

Sikuwahi kubahatika kuonana na Alhaj Aboud Jumbe wakati wa uhai wake. Hata hivyo, nimejifunza mengi sana kutoka kwake, hasa ujasiri wa kuuhoji Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Jumbe amekuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye mjadala wa Muungano kwa zaidi ya miongo mitatu sasa.

Ninadiriki kusema kwamba, hoja ya Serikali Tatu ilianzia kwa Jumbe. Roho yake ilikuwa kila mahali wakati wa mchakato wa Katiba Mpya kati ya 2011 na 2014.

Kivuli chake kilikuwa kila mahali wakati wa Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014. Pengine kuliko hata Mwalimu Nyerere, Jumbe ndiye aliyetufundisha kuufahamu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Atakumbukwa kama mmoja wa waTanzania maarufu na wapigania uhuru wakubwa wa Zanzibar ya baada ya Muungano.

Adieu Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi. Adieu Mtanzania jasiri. Adieu shujaa wa uhuru wa Zanzibar

Somo la Historia ni zuri sana, twende maktaba :

Kwa nini Rais Aboud Jumbe wa Zanzibarhakualikwa kwenye Bunge la Katiba kesho atakapohutubia Kikwete?​

​

Uzi Thread starterNikupateje​

1
Magazeti karibu mengi ya leo yanaeleza kwamba kesho mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete atahutubia Bunge la Katiba. Huko ataambatana na karibu viongozi wote wakuu wa sasa na wa zamani.

Wametajwa marais wastaafu Jamhuri ya Muungano na marais wastaafu wa Zanzibar. Wametajwa pia mawaziri wakuu wastaafu wa Muungano kuwemo kesho.

Watakaoambatana na Rais kesho kwa mujibu wa gazeti la MWANANCHI ni hawa wafuatao:
Dr. Ali Mohamed Shein (Rais-Zanzibar), Mohamed Gharib Bilal (Vice-Pesident-Union), Seif Shariff Hamad (First Vice-Zanzibar). Hawa ni viongozi walioko madarakani.

Wasioko madarakani ni wafuatao:
Ali Hassan Mwinyi (Rais Mstaafu wa Union na pia mstaafu wa Zanzibar), Benjamin Mkapa (Rais Mstaafu wa Union), Dr. Salmin Amour (Rais Mstaafu wa Z'bar) na Aman Abeid Karume (Rais Mstaafu wa Z,bar).

Pia watakuwemo wajane wa waasisi wa Muungano yaani Mama Maria Nyerere na mama Fatma Karume.

Pia watakuwemo mawaziri wakuu wastaafu yaani:
Salim Ahmed Salim, Joseph Warioba, John Malecela, Cleopa Msuya, Fredrick Sumaye na Mizengo Pinda ambay eni mjumbe humo.

Baada ya kuisoma list hii, nilipitia magazeti mengine nione kama kasoro kama ipo humu tu lakini naona kote ni vilevile.

Kasoro yenyewe ni kwamba sioni jina la Rais wa Zanzibar aliyekaa ikulu ya Zanzibar kwa muda mrefu kuliko mzanzibari yoyote. Naye ni Rais Aboud Jumbe ambaye amekaa pale kuanzia 1972 hadi 1984 yaani miaka 12.

Nina hoja nyingi lakini hapa ninaweza kadhaa tu. Kama ni mtizamo wake wa serikali tatu wa mwaka 1984 basi mbona Malecela amealikwa.

Kama hajiwezi basi kwa nini asingechukuliwa mke wake kama watakavyokuja kina Maria na Fatma, au aina yoyote ya uwakilishi kuonyesha heshima kwa Jumbe.

Tunatakiwa tujifunze kwa wazanzibari. Hebu nenda hata leo kwenye mitaa ya Zanzibar halafu uone jinsi wanavyomuenzi Aboud Jumbe. Mitaa mikubwa yote ukiingia unakutana na picha za marais wao wote kuanzia shujaa Abeid Karume, Aboud Jumbe na wote hadi wa sasa Shein.

Kama huku hapewi hiyo heshima, basi nenda kule mitaa ya Zanzibar halafu uthubutu kukejeli mawazo ya watu kama Aboud Jumbe tuone kama utatoka salama.

Huwezi kuandika histroai ya Muungano bila kumtaja Rais Aboud Jumbe, upende usipende. Hivyo, Rais Aboud Jumbe ana sehemu yake kubwa tu, tena huenda kuliko hao walioalikwa humo bungeni kesho
 
Kwenda zako huko kama unajua kuomba piga maombi ya kumaliza ulofa wako kwanza

Charity begins at home
Yesu alisema kuwa kwanza ombeni Mungu awape riziki yenu kwanza

CHADEMA wamejaa malofa choka mbaya ukiwemo wewe Lisu na Heche na Godbless Lema,askofu Mwamakula, Mnyika,Golugwa nk na wajumbe kibao kamati kuu nk CHADEMA hata hawana shughuli za kuwaingizia kipato cha kueleweka wanategemea tonetone waombee hao kuwa ee Mungu wasaidie wapate riziki ya kueleweka na uwaombee hao viongozi wako wa CHADEMA Mungu awaepushe na majaribu ya yule mwovu ya kutegemea tonetone kuendesha maisha yao

Acha kuwewseka kuomba kwa uchungu maombi yasiyokuhusu nje ya hapo huo ni umbeya kwenye maombi
Pumbavuuu
 
Heheee
Yajayo yanavyofurahisha mnooo
Msoga ndo nani ndo Mungu,ameumba mbingu na nchi ?
Km ye ni Mungu sawa ila km ni mwanadamu basi tambuabyukosemaji wa mwisho Ambae ni Mungu mkuu,na atasema na mtashangaa
Oktoba ndiyo mtamjua msoga ni Mungu au Binadamu.
Kama vipi hamieni Burundi
 
MAMBO YA MKATO YA SHEIKH ABOUD JUMBE MWINYI YALIVYOMUHARIBIA, KUJIRUDIA TAREHE 18 AUGUST 2025 KWA SAMIA ?

HISTORIA :

Ugomvi wa Aboud Jumbe na Nyerere ulivyotetemesha nchi-5​

November 24, 2015

Na Elvan Stambuli

Kama nilivyosema wiki iliyopita, hatua ya kwanza iliyoanza kutikisa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ni pale Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Damian Lubuva aliporejeshwa Tanzania Bara na badala yake Rais Aboud Jumbe akateua raia wa Ghana, Alhaj Bashir K. Swanzy na kumpa uraia kushika wadhifa huo, Endelea…

Kuanzia hapo, madai ya Wazanzibari kutaka mabadiliko ya Katiba, kupitia mihadhara, magazeti na redio yalipamba moto.

Kukaanzishwa ‘redio pori,’ wengi watakumbuka matangazo ya redio hiyo ya mafichoni ambayo ilipachikwa jina la KIROBOTO TAPES ya kudai Wazanzibari warejeshewe visiwa vyao.

Ni mashushushu wa kijeshi wa bara ndiyo waliogundua baadaye kuwa ipo msituni, ikazimwa, sikumbuki kama kuna watu walifikishwa mahakamani kwa kumiliki redio hiyo.

Kwa kupitia Mghana, Jaji Bashir Swanzy, Serikali ya Jumbe iliandaa hati ya mashtaka kuhoji muundo na uhalali wa Muungano kwenye Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo kazi yake pekee, kwa mujibu wa ibara ya 126 ya Katiba ya Muungano ya 1977, “ni kusikiliza shauri lililoletwa mbele yake na kutoa usuluhishi juu ya suala lolote linalohusika na tafsiri ya Katiba, iwapo tafsiri hiyo au utekelezaji wake unabishaniwa kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.”

Hati hiyo ya mashtaka ‘ilipotea’ mezani kwa Rais Aboud Jumbe katika mazingira ya kutatanisha sana na kuibukia mikononi mwa Mwalimu Nyerere Msasani Dar es Salaam!

Taarifa za uhakika zinaonesha kuwa waliofanikisha kazi ya kuiba hati hiyo na kuipeleka kwa Mwalimu Nyerere ni baadhi ya vigogo ambao sasa wako katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wakati ule wakiwa SMZ.

Haraka Mwalimu Nyerere aliitisha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mjini Dodoma, Januari 1984 na Rais Aboud Jumbe akabanwa kwa madai ya kutaka kuuvunja Muungano kwa kuuhoji.

Nchi ikatangaziwa kwamba kuna “Kuchafuka Kwa Hali ya Hewa ya kKsiasa Zanzibar.”

Rais Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi mbele ya kikao alihojiwa na NEC na bila kumung’unya maneno, Sheikh Jumbe alikiri kuandaa hati hiyo kama moja ya haki zake za kikatiba, jambo ambalo lilizidi kumtibua Mwalimu Nyerere.

Usikose kusoma muendelezo wa makala haya wiki ijayo...

NONDO ZA ZIADA KUHUSU KADHIA YA SHEIKH JUMBE

View: https://m.youtube.com/watch?v=r9ZQGyVcuW4

UJASIRI WA KUHOJI WA 1984 UTAJIRUDIA TAREHE 18 AUGUST 2025 ?

View attachment 3413390
AEn0k_ttSRrPZfcvsSszSzUsCPvEysD27kUOlChfkxfS3O617XCr42hi0OyxXzHtSbRmvZFYCpGQB5qmdwuoNaErhcuRvQphm8Rx024r2rnHGoBPu7sWAxlMFKlheGtuuGefYsu2xxoodGNh1w=s0-d

Alikuwa pia mwasisi wa Muungano ulioizaa Tanzania miezi michache baadaye. Baada ya Sheikh Abedi Amani Karume kuuawa mwezi Aprili 1972, Jumbe aliteuliwa kuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, na alishikilia madaraka hayo hadi Januari 1984.

Wasomi wa Muungano wameandika kwamba, wakati Rais Karume anauawa, uhusiano wake na Mwalimu Julius Nyerere ulikuwa umeharibika kiasi kwamba Jumbe (kwa upande wa Zanzibar) na Bhoke Munanka (kwa upande wa Tanganyika) ndio walikuwa kiunganishi cha mawasiliano kati ya Mwalimu na Karume.

Hii pengine ndio sababu Mwalimu alitumia ushawishi wake kuhakikisha Jumbe anateuliwa kumrithi Karume.

Hata hivyo, Jumbe atakumbukwa zaidi na historia kwa upinzani wake kwa mfumo wa sasa wa Muungano kuliko, pengine, kwa jambo jingine lolote.

Jumbe alikuwa mwanasiasa wa kwanza, baada ya era ya (uongozi wa) Karume, kutambua kwamba muundo wa serikali mbili ulikuwa umeipokonya Zanzibar mamlaka yake na kuyahamishia Tanganyika.

Alikuwa wa kwanza kutambua kwamba, kuzaliwa kwa CCM katika context (mtazamo) ya Muungano, kulimaanisha mwisho wa mamlaka yaliyokuwa Zanzibar chini ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964.

Sio tu alitambua bali pia Jumbe alichukua hatua kupinga Zanzibar kupokonywa mamlaka yake hayo.

Ili kufanikisha azma yake, Jumbe alilazimika kumwachisha kazi Mwanasheria Mkuu wake aliyempewa na Mwalimu Nyerere, Damian Lubuva, na kumwajiri Bashir Ebassuah Kwaw Swanzy, Raia wa Ghana, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Kwaw Swanzy ndiye aliyeandaa ‘hati ya mashtaka’ dhidi ya Muungano iliyokamatwa na watu wa usalama wa Mwalimu na baadaye kutumika kumsulubu Jumbe kwenye kikao cha NEC ya CCM Dodoma Januari 1984. Kwa sababu ya upinzani huo, Jumbe aling’olewa madarakani pamoja na Waziri Kiongozi wake Ramadhani Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Kwaw Swanzy alitangazwa kufukuzwa nchini.

Mwalimu akatangaza ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa’ Zanzibar na Wazanzibari wengi wapinzani wa Muungano, kama Mwanasheria Mkuu wa kwanza Wolfgang Dourado, kuwekwa kizuizini.

Miaka 10 baada ya kuondolewa madarakani, Alhaj Aboud Jumbe alichapisha kitabu chake juu ya Muungano, ‘Miaka Thelathini ya Dhoruba’, ambako aliweka bayana ugomvi wake na Mwalimu juu ya Muungano.

Jumbe ni kiongozi pekee wa juu wa rika la wapigania uhuru wa Tanzania kuandika memoirs zake juu ya Tanzania na matatizo ya Muungano wake.

Hata Mwalimu hakufanya hivyo na alikufa na siri zake juu ya mambo mengi makubwa yalitokea wakati wa utawala wake.

Kwangu mimi, hii ndio merit (faida) kubwa na mchango mkubwa wa Alhaj Aboud Jumbe kwa kizazi cha sasa na vijavyo Tanzania.

Alikuwa na ujasiri wa kusema na kuandika juu ya ‘The Forbidden Subject’, tena katika kipindi cha Mwalimu Nyerere ambapo ujasiri wa aina hiyo ulikuwa ni jambo la hatari kubwa.

Kwa sababu hiyo hiyo, Jumbe alilazimika kuishi theluthi ya mwisho ya maisha yake ‘kifungoni’ Mji Mwema, Kigamboni, ambako alipelekwa mara baada ya kung’olewa madarakani mwaka ’84.

Sikuwahi kubahatika kuonana na Alhaj Aboud Jumbe wakati wa uhai wake. Hata hivyo, nimejifunza mengi sana kutoka kwake, hasa ujasiri wa kuuhoji Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Jumbe amekuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye mjadala wa Muungano kwa zaidi ya miongo mitatu sasa.

Ninadiriki kusema kwamba, hoja ya Serikali Tatu ilianzia kwa Jumbe. Roho yake ilikuwa kila mahali wakati wa mchakato wa Katiba Mpya kati ya 2011 na 2014.

Kivuli chake kilikuwa kila mahali wakati wa Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014. Pengine kuliko hata Mwalimu Nyerere, Jumbe ndiye aliyetufundisha kuufahamu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Atakumbukwa kama mmoja wa waTanzania maarufu na wapigania uhuru wakubwa wa Zanzibar ya baada ya Muungano.

Adieu Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi. Adieu Mtanzania jasiri. Adieu shujaa wa uhuru wa Zanzibar

KUCHAFUKA KWA HALI YA KISIASA NDANI YA CCM

KUTOKA MAKTABA :

Maalim Seif Sharrif Hamad waziri kiongozi SMZ mfuasi wa rais Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi, naye alitimuliwa kwa ushiriki wake kuchafua hali ya hewa ya kisiasa, na Maalim Seif baada,ya kutimuliwa CCM aliamua kutoa hotuba hii mwaka 1988

View: https://m.youtube.com/watch?v=dhyHYbEqBSw
 
ccm ni nyoka mzee ,itoke serikalini ikajichue kwanza wakati inajichua chadema iende ikulu
Hivi wakati wa miaka ya 2010, nini kilipelekea Rostam Aziz kujivua nyadhifu zote ndani ya chama kikongwe cha kufanya mapinduzi ?
 
Wagombea wa nafasi ya ubunge ni wengi muda wa kuwajadili na kuwachuja ni mdogo ndio maana wamesogeza mbele acha kuleta taharuki. Ufafanuzi ulikwisha tolewa sababu ya kuchelewa. Kwa taarifa tu kuna Jimbo waliochukuwa form na kurudisha wanafika mpaka 18 ona?
Acha kubeba sababu za kitoto kwenye mambo serious.
 
K
Tunajadil jambo lisilokuwa la kawaida. Akili yako ndogo wewe unaliona la kawaida tu.nyie ndo wale wanaume mnaovaa heleni na kusuka ili mfanane na kina nani sijui
Kama kuahirishwa mkutano tu unaliona ni jambo lisilo la kawaida...kukuita kiazi nimekupendelea.
 
Bibi atakua ana haidi kuwapa mabilioni wamwache aendelee
 
Back
Top Bottom