Mnaotumia Masaa Mengi Kujadili Mpira, Mnapata Dola Ngapi kwa Siku?

Kwa hiyo kama issue dola basi kwenye dini kuna hela.
Mi sijasema kwenye dini kuna hela, nimeshauri kwamba heri kutumia muda mwingi kufikiria njia za kutuongezea kipato kama vile kujifunza kazi au ujuzi mpya. Nimeshauri pia kwamba afadhali kujadili mambo ya rohoni na kujizoeza utauwa ambao una faida ya uzima wa sasa na ule ujao.
 
Nazifuata tu nyayo za Yesu. Yesu alipoongea na watu, mara nyingi alinukuu Maandiko. Kwa mfano Katika Mt 4 4 anasema: "Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu." Hapo alinukuu Kum 8:3.
Bible ndoo taa ya miguu yetu, ndio kitabu kinachotupa mwongozo wa jinsi ya kuenenda.
Samahani , umeolewa?
 
Unapata Dola au ukipata Dola unazipata ili ufanye nini ? Kama Dola zake anazitumia kuangalia na kusikiliza majadiliano ya mpira huoni kwamba kujadili bure kwake yeye hio ni shortcut ?!!!

Samahani , umeolewa?
791612.jpg

Unataka mcha Mungu, siyo?
 
% kubwa ya watanzania, muda sio mali.
Bodaboda wapo kijiweni wanasubiri abiria huku wanapiga story za mpira, hapo utasema wanapoteza muda?
Kuna siku saba, siku moja tuu tena ya masaa kadhaa ndo kupoteza muda?
N wangapi kazi zao zinawaruhusu kukaa na kupiga story, hapo utasema wanapoteza muda?

Binafsi huwezi kunikuta kwenye hizo mada n kwa sababu Mm sio mpenzi wa ligi ya Bongo, ila sio kwa sababu muda ni mali.
Iyo siku moja kila wiki zidisha mara 4 halafu zidisha mara 12. Kwa mwaka utaona umetumia siku 48. Ni kama mwezi mmoja na nusu unajadili mpira tu. Watu wa bodaboda wanaojadili mpira saa ingine wanapoteza wateja kwa sababu mabishano yakiwa makali hakuna anayechangamkia wateja.
 
Mpira wa miguu ni burudani inayowachangamsha wengi, lakini je, umewahi kujiuliza thamani ya muda unaotumia kujadili mpira? Wengine hutumia saa nyingi kubishana kuhusu wachezaji, timu, na matokeo, lakini je, mijadala hiyo inazalisha kipato chochote?

Katika ulimwengu wa sasa, muda ni rasilimali muhimu. Wale wanaonufaika zaidi na mpira ni wachezaji, makocha, watangazaji, na wadhamini—si mashabiki wanaopoteza masaa kwenye mabishano yasiyo na tija.

Biblia inasema: “Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya. Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana.”(Waefeso 5:16-17 BHN). Badala ya kutumia muda mwingi kuzungumzia mpira bila faida, ni vyema kufikiria jinsi unavyoweza kutumia muda wako kwa njia yenye manufaa zaidi, kama kujifunza ujuzi mpya, kuwekeza, au kuunda fursa za kipato. Hebu jiulize tena:

👉Baada ya kubishana kuhusu mpira, akaunti yako ya benki itaongezewa pesa?
👉Je, mjadala wako wa mpira utalipia bili zako za mwezi huu?
👉Dakika unazotumia kubishana kuhusu mpira zingekuletea faida gani kama ungezitumia kwa kazi inayokuongezea kipato?
👉Wachezaji unaowatetea wanajua hata jina lako?
👉Kama ungetumia muda huo kujifunza ujuzi mpya, ungekuwa mbali kiasi gani sasa?

Si afadhali hata ungetumia muda mwingi kujadili mambo ya rohoni ili ujizoeze kuwa na utauwa? Utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye(1 Timotheo 4:7-8).
Tuwaombee watoke katika aina hii ya ulevi uliowafunga akili na ufahamu wa rohoni.
 
Iyo siku moja kila wiki zidisha mara 4 halafu zidisha mara 12. Kwa mwaka utaona umetumia siku 48. Ni kama mwezi mmoja na nusu unajadili mpira tu. Watu wa bodaboda wanaojadili mpira saa ingine wanapoteza wateja kwa sababu mabishano yakiwa makali hakuna anayechangamkia wateja.
Hapana, nakupinga.
Itafika wakati mtasema watu wasipumzike mana wanapoteza muda.
 
Unapata Dola au ukipata Dola unazipata ili ufanye nini ? Kama Dola zake anazitumia kuangalia na kusikiliza majadiliano ya mpira huoni kwamba kujadili bure kwake yeye hio ni shortcut ?!!!

Anayepata dola na kuzitumia kuangalia mpira, pembeni ya kochi lake hapakosekani juice au karanga au supu. Huyu mwingine anajadili bila kutia chochote kinywani.
 
Hapana, nakupinga.
Itafika wakati mtasema watu wasipumzike mana wanapoteza muda.
Wenzako wanaozitafuta dola wakipumzika wanaenda kwenye hoteli za 5 stars Dubai. Hawa wenzetu watabishana wee, wanaondoka vichwa vinauma hata pesa ya kununua panadol hawana.
 
Mpira wa miguu ni burudani inayowachangamsha wengi, lakini je, umewahi kujiuliza thamani ya muda unaotumia kujadili mpira? Wengine hutumia saa nyingi kubishana kuhusu wachezaji, timu, na matokeo, lakini je, mijadala hiyo inazalisha kipato chochote?

Katika ulimwengu wa sasa, muda ni rasilimali muhimu. Wale wanaonufaika zaidi na mpira ni wachezaji, makocha, watangazaji, na wadhamini—si mashabiki wanaopoteza masaa kwenye mabishano yasiyo na tija.

Biblia inasema: “Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya. Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana.”(Waefeso 5:16-17 BHN). Badala ya kutumia muda mwingi kuzungumzia mpira bila faida, ni vyema kufikiria jinsi unavyoweza kutumia muda wako kwa njia yenye manufaa zaidi, kama kujifunza ujuzi mpya, kuwekeza, au kuunda fursa za kipato. Hebu jiulize tena:

👉Baada ya kubishana kuhusu mpira, akaunti yako ya benki itaongezewa pesa?
👉Je, mjadala wako wa mpira utalipia bili zako za mwezi huu?
👉Dakika unazotumia kubishana kuhusu mpira zingekuletea faida gani kama ungezitumia kwa kazi inayokuongezea kipato?
👉Wachezaji unaowatetea wanajua hata jina lako?
👉Kama ungetumia muda huo kujifunza ujuzi mpya, ungekuwa mbali kiasi gani sasa?

Si afadhali hata ungetumia muda mwingi kujadili mambo ya rohoni ili ujizoeze kuwa na utauwa? Utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye(1 Timotheo 4:7-8).
Sisi tunaopenda kujadili Mpira kila Siku hapa JamiiForums umeshatuona hata Siku moja tukija Kwako kukubishia Hodi kukuomba Hela ya Kula?

Na nani kakudanganya kuwa Wote tunaojadili Mpira kutwa hapa JamiiForums hatuna Hela, Kazi wala Hadhi yoyote?

Hivi hapa JamiiForums tunajiwasilisha kwa Uhalisia wetu kamili wa nani ni GENTAMYCINE huko aliko au ni kwa Fake IDs zetu tu?

Kwa taarifa yako pamoja na Wapumbavu wengine wenye mtizamo Hasi na wa Kishamba kama wako ni kwamba kuna Watu unaowaita wajadili Mpira kila Siku hapa JamiiForums wana Maisha mazuri, Kazi nzuri, Hadhi kubwa na Pesa za kumzidi Anayekukaza.

Na wanaweza hata Kukukaza / kukubandua nawe pia na Kukuhonga Fedha ambazo uliyenae au ulionao hawajawahi kukupa.

Mnakera mno nyie Wapumbavu na kutuona Wajadili Mpira hapa JamiiForums ni Watu tu wa kawaida na wasio na mbele wala nyuma. Kwahiyo ulipenda au ukitaka labda tuwe Kutwa tunajadili tu jinsi Unavyokazwa / Unavyoshindiliwa nao ndiyo ufurahi? Hovyo kabisa.....!!

Nimemaliza.
 
Pole sana. Wenye hela hawana kelele nyingi. Saa hizi wamepumzika zao Dubai.
 
Mpira wa miguu ni burudani inayowachangamsha wengi, lakini je, umewahi kujiuliza thamani ya muda unaotumia kujadili mpira? Wengine hutumia saa nyingi kubishana kuhusu wachezaji, timu, na matokeo, lakini je, mijadala hiyo inazalisha kipato chochote?

Katika ulimwengu wa sasa, muda ni rasilimali muhimu. Wale wanaonufaika zaidi na mpira ni wachezaji, makocha, watangazaji, na wadhamini—si mashabiki wanaopoteza masaa kwenye mabishano yasiyo na tija.

Biblia inasema: “Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya. Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana.”(Waefeso 5:16-17 BHN). Badala ya kutumia muda mwingi kuzungumzia mpira bila faida, ni vyema kufikiria jinsi unavyoweza kutumia muda wako kwa njia yenye manufaa zaidi, kama kujifunza ujuzi mpya, kuwekeza, au kuunda fursa za kipato. Hebu jiulize tena:

👉Baada ya kubishana kuhusu mpira, akaunti yako ya benki itaongezewa pesa?
👉Je, mjadala wako wa mpira utalipia bili zako za mwezi huu?
👉Dakika unazotumia kubishana kuhusu mpira zingekuletea faida gani kama ungezitumia kwa kazi inayokuongezea kipato?
👉Wachezaji unaowatetea wanajua hata jina lako?
👉Kama ungetumia muda huo kujifunza ujuzi mpya, ungekuwa mbali kiasi gani sasa?

Si afadhali hata ungetumia muda mwingi kujadili mambo ya rohoni ili ujizoeze kuwa na utauwa? Utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye(1 Timotheo 4:7-8).
Maofisin na vijiweni full kelele
 
Back
Top Bottom