Moshi: Mama afariki Dunia akiwa nyumbani kwa kukosa pesa ya matibabu, aacha watoto wadogo

Moshi: Mama afariki Dunia akiwa nyumbani kwa kukosa pesa ya matibabu, aacha watoto wadogo

Mwenyekiti wa kijiji hicho amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ni kweli familia ilikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu kutokana na ukata hivyo mama huyo kufariki dunia akiwa nyumbani kwake
"Mwenyekiti na Serikali ya Kijiji hicho nao walikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu". Mwisho wa kunukuu
 
Watu wote walozunguka pale walishindwa msaidie aende hospital ,?mwenyekit anashindwa changisha watu huku mgonjwa yupo hospital mbona wanachangisha pesa za mlinzi mara sijui nin ,🙆🏼‍♂️🙆🏼‍♂️
Kabla hujacomment unajua hali ya wananchi wa hicho kijiji. Au unafikiri vijiji vyote Tanzania vimekaa kama Masaki na Oysterbay?
 
Maisha yamekuwa magumu mara 100 pamoja na watu kusema nchi imefunguka!
Nchi imefunguka ni ukweli usiopingika lakini bado sana wananchi hawajafunguka vichwani mwao. Kwa mfano huyo mume angempeleka mke wake ( ambaye kwa sasa ni marehemu) hospitali, ina maana umauti ungemkuta akiwa hapo OPD akimsubiri mume apate pesa? Asingepewa matibabu halafu alipe deni? (Utaratibu ukoje?)Yuko mdau hapo juu #5 ameuliza lakini naona wachangiaji hatukuelewa undani wa swali lake.
 
Watu wote walozunguka pale walishindwa msaidie aende hospital ,?mwenyekit anashindwa changisha watu huku mgonjwa yupo hospital mbona wanachangisha pesa za mlinzi mara sijui nin ,🙆🏼‍♂️🙆🏼‍♂️
Nina wasiwasi na huyo mwanaume. Inawezekana hana mahusiano mazuri na jamii inayomzunguka, labda ana kaujeuri fulani au alikuwa ametamania siku nyingi aachane na mke wake kimtindo.
 
Nchi imefunguka ni ukweli usiopingika lakini bado sana wananchi hawajafunguka vichwani mwao. Kwa mfano huyo mume angempeleka mke wake ( ambaye kwa sasa ni marehemu) hospitali, ina maana umauti ungemkuta akiwa hapo OPD akimsubiri mume apate pesa? Asingepewa matibabu halafu alipe deni? (Utaratibu ukoje?)Yuko mdau hapo juu #5 ameuliza lakini naona wachangiaji hatukuelewa undani wa swali lake.
Kabla hujacomment unajua hali ya wananchi wa hicho kijiji. Au unafikiri vijiji vyote Tanzania vimekaa kama Masaki na Oysterbay?
 
Kabla hujacomment unajua hali ya wananchi wa hicho kijiji. Au unafikiri vijiji vyote Tanzania vimekaa kama Masaki na Oysterbay?
Ukiacha Masaki na Oysterbay(ambapo kwa mtizamo wako ndo ulitaja kana kwamba ni mahali bora zaidi pa kutolea mfano), vijijini huku kwetu tuna mahusiano ya kushirikiana, kusaidiana, kujaliana kwa mambo mengi- kwa raha na shida. Hata kama umaskini huku vijijini ndiko ulikotamalaki, lakini tuna ubinadamu zaidi. Huyo mwamba alikuwa na lake.
 
Hivi ukienda Hospital unaambiwa utoe ela kwanza ndipo utibiwe ?
Hakuna kitu kama hicho,ingawa lazima uulizwe kama una pesa, na wakigundua kuwa huna,sidhani kama watakuacha ufe,labda wahudumu wawe na roho mbaya...
 
Marehemu Happiness kasmiry kutoka kijiji cha Usari wilaya ya Moshi. Alishikwa na ugonjwa wa tumbo wa kuhara na kutapika kwa siku kadhaa kabla ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake kutokana na Kukosekana kwa fedha ya matibabu.

Mume wa marehemu huyo ajulikanae kwa la John alihakangaika kutafuta pesa ya kumpeleka Hospital kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Mume wa marehemu amesema alikuwa anakabiliwa na ukata mkubwa kutokana na kumuhudumia mama yake mzazi ambae amepooza upande mmoja wa mwili.

Marehemu ameacha watoto watatu wadogo. Mwenyekiti wa kijiji hicho amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ni kweli familia ilikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu kutokana na ukata hivyo mama huyo kufariki dunia akiwa nyumbani kwake
Yaani mwenyekiti wa kijiji anasema kirahisirahisi hivyo! Alishindwa kuchangisha pesa kutoka kwa viongozi au kupata msamaha toka serikalini! Hakuweza kujaribu njia yoyote ili aokoe maisha ya huyo mama! Sidhani watu wote huko kama ni wakatili hivyo.
 
Marehemu Happiness kasmiry kutoka kijiji cha Usari wilaya ya Moshi. Alishikwa na ugonjwa wa tumbo wa kuhara na kutapika kwa siku kadhaa kabla ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake kutokana na Kukosekana kwa fedha ya matibabu.

Mume wa marehemu huyo ajulikanae kwa la John alihakangaika kutafuta pesa ya kumpeleka Hospital kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Mume wa marehemu amesema alikuwa anakabiliwa na ukata mkubwa kutokana na kumuhudumia mama yake mzazi ambae amepooza upande mmoja wa mwili.

Marehemu ameacha watoto watatu wadogo. Mwenyekiti wa kijiji hicho amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ni kweli familia ilikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu kutokana na ukata hivyo mama huyo kufariki dunia akiwa nyumbani kwake
Kifo akizuiliki lakini bora wangempeleka hospitali hajafika huko hata kwa kuweka shamba rehani
 
Watu Wana roho mbaya, majirani wote wameshindwa kumpa msaada hata wa laki akaanze matibabu, mpaka mtu anakufa
Ingekuwa sherehe wangechangangia bora mume angweka shamba poni
 
Ila ajabu sasa ukienda msibani huwezi ukakuta waombolezaji wamekaa na njaa
 
Hivi nyie mmefanikiwa hata kuishi kijijini kweli, au ni story tu mnasikia? Upatikanaji wa pesa kijijini ni mdogo sana, ukisikia mtu fukara ni fukara kweli.
Wanajifanya hawaelewi,
Huko vijijini unaweza ukapita kwenye kaya kumi asubuhi na hakuna mwanakijiji mwenye japo elfu mbili ndani.
 
"Mwenyekiti na Seriklai ya Kijiji hicho nao walikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu". Mwisho wa kunukuu
Kama kweli hivo ndivyo ilivyotokea; basi Mwenyekiti na Serikali ya Kijiji hicho wawajibike haraka kwa kujiuzulu kwani hawatoshi katika nafasi hiyo.
Nasema hivyo kwa sababu:
1. Fedha wanazopataau kukusanya kutoka vyanzo mbalimbali e.g. Faini za makesi, Makusanyo ya vilabu vya pombe, magenge/soko migahawa Makusanyo ya maliasili e.g. mchanga,mawe fedha zinaishia wapi? Mbona hakuna Taarifa ya Mapato na Matumizi(Hili ni kwa vijiji vingi tu hapa Tz.)
2. Huyo mwanaume awajibishwe au afunguliwe mashtaka ya Uzembe uliopelekea kifo cha mke. Nasema hivyo kwa sababu ; hivi hana ndugu/majirani? alishindwa kwenda kukopa? alishindwa kuuza baadhi ya mali(vitu) - hana hata kuku au hata kipande cha ardhi aweke rehani ili watu wamkopeshe? Kama yote hayo yalishindikana bora tu hata angeenda kuiba mahali akamatwe halafu achomekee hali ya mke wake. 😆 😆 😆 😆 😆 Mbona Wachaga wana kamsemo kao kanakosema "Kuliko uzae mpumbavu ni bora uzae mwizi" Mpumbavu kwa kichaga ni Tondo, mwizi ni Mbafu
 
Watu wote walozunguka pale walishindwa msaidie aende hospital ,?mwenyekit anashindwa changisha watu huku mgonjwa yupo hospital mbona wanachangisha pesa za mlinzi mara sijui nin ,[emoji2301][emoji2301]
Hata mazishi yake watachangisha
 
Bima ya afya nibure?ikiwa mtu inamshinda hiyo elfu2 yakufungua kadi iyo ya bima anapata wapi???kunamtu mwaka mzima na hashiki laki yamkupuo
 
Nina wasiwasi na huyo mwanaume. Inawezekana hana mahusiano mazuri na jamii inayomzunguka, labda ana kaujeuri fulani au alikuwa ametamania siku nyingi aachane na mke wake kimtindo.

Inasikitisha sanaa
 
Back
Top Bottom