Uchaguzi 2020 Mpangilio wa Majina ya vyama kwenye Karatasi ya kupigia kura ulizingatia nini?

Uchaguzi 2020 Mpangilio wa Majina ya vyama kwenye Karatasi ya kupigia kura ulizingatia nini?

Naomba niulize .
Hivi ikatokea wakati nipo kwa kile "kiambaza " cha kupiga kura then nikute mgombea wangu hayupo kabisa nafanyaje?
 
Miaka yote huwa wanafuata Alphabet in Ascending order naona mwaka huu CCM wamepindua meza Maana ACT ingekuwa juu
Bado siamini Tume inaweza kufanya ujinga kama huu...hii ni aibu! Hata hivyo nina imani na wapiga kura, huu ujinga wa Tume unaweza kuwarudia wao wenyewe. Kwa kuwa adui nambari wani wa taifa ni CCM na hivyo ukichagua nambari wani umechagua adui.
 
Wameamua kuwaweka wapinzani wawili mbalimbali ili wale watu wanaotetemeka wasije kukosea kupiga tiki.

Tarehe 28 nikiingia chumba Cha kupigia kura, nachukua kalamu, pale namba moja nachora zombie halafu tiki napiga chini kabisaaa.(natania tu)

Hapana Mkuu usifanye hivyo,ukifanya hivyo kura yako itaharibika Mkuu,wewe tiki tu kwenye kile kisanduku cha uliye kusudia kuumpa kura yako!.
 
Yana wasiwasi kweli haya maccm 😂😂😂
2015 walifata mpangilio Alphabetically.

Naona mwaka huu wameamua kufanya kituko, inawezekana wakaweka jina la chadema upande wa nyuma wa karatasi.

Sitashangaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Halafu mwaka jana wakaengua wagombea uchaguzi serikali za mitaa kisa walijaza CHADEMA badala ya Chama cha demokrasia na maendeleo
 
Mbona Kitu mnalalamika,Hii ni moja ishara ya udhaifu.

Ila kila mtu anamjua mgombea anaenda kumpigia. So mtu kuwa wa kwanza au wa mwisho si chanzo cha kumfanya mpiga kura asimpigie mgombea anayemtaka.

Punguzeni kuonesha udhaifu mapema, Huu ni mpangilio tu na sio matokeo ya uchaguzi.
 

Nimeona Mfano wa karatasi ya kupigia kura za Urais inayosambaa mitandaoni na ambayo inadaiwa kutolewa na Tume ya Uchaguzi (NEC).

Nina swali dogo tu ambalo naomba nijibiwe. Huu mpangilio wa Majina ya vyama uliowekwa kwa namba ulitokana na vigezo gani, yaani ni kigezo gani kilizingatiwa ili huyu awe namba 1 na yule awe namba 5 ama awe namba 8?

Nitasema Kweli Daima Fitna kwangu Mwiko .
Mahera akili yake ina kutu
 
Mimi nimejiuliza maswali mengi,nilichogundua ni kwamba hawa jamaa wametumia jinsi wagombea walivyorejesha fomu zao za uteuzi. Nimefuatilia mgombea wa CCM alikuwa wa kwanza kurejesha fomu za uteuzi na mgombea wa Chadema alikuwa wamwisho kukabidhi fomu za uteuzi.ndio maana CCM imeonekana ya kwanza kwenye hizo karatasi na CDM kuwa yamwisho kwenye list.ni mtazamo nilioouona
 
mimi nimejiuliza maswali mengi,nilichogundua ni kwamba hawa jamaa wametumia jinsi wagombea walivyorejesha fomu zao za uteuzi.nimefuatilia mgombea wa CCM alikuwa wa kwanza kurejesha fomu za uteuzi na mgombea wa CDM alikuwa wamwisho kukabidhi fomu za uteuzi.ndio maana CCM imeonekana ya kwanza kwenye hizo karatasi na CDM kuwa yamwisho kwenye list.ni mtazamo nilioouona
Mahera anasemaje ?
 
Hiyo ina shida gani kwani Twaweza walishasema kuwa ccm inaungwa mkono zaidi na wale wasiojua kusoma wala kuandika.

Ccm wamewatafutia watu wao hao urahisi wa kuwapigia kura. Chadema hawana cha kupoteza kwani wanaowaunga mkono karibu wote wanajua kusoma na kuandika hivyo Lissu hata wangemuweka wapi bado kura zake anazo tu.
 
CHADEMA MMEPEWA FURSA ADHIMU, KUANZIA SASA ANZENI KUSHAWISHI WAPIGA KURA SIKU YA KUPIGA WACHAGUE MGOMBEA WA MWISHO NDIYE YEYE, Wasitazame kwengine, wakipewa fomu tu watiki mgombea wa mwisho kwenye karatasi ndiye YEYE HUYO
Kimbelembele cha CCM kiwatoke puani, wapuuzi waahed!
 
Wamekeuka utaratibu wa kufuata alphabet. Hii inaonyesha tume iko biased against CHADEMA in particular and in favor of CCM. Ilikuwa ianze AAFP, ADC, CCM, CHADEMA, DEMOCRASIA MAKINI, DP. Hata hivyo hakuna tatizo. Wasiompenda atawasuprise.
 
Back
Top Bottom