Msaada wa kisheria kuwapata watoto baada ya kuhitilafiana na baba yao

Msaada wa kisheria kuwapata watoto baada ya kuhitilafiana na baba yao

Shida nyie viumbe hamjawahi kujua kudhibiti kiburi mpatapo kauwezo kidogo, tumesikia story ya upande mmoja tu, tungepata na ya upande wa pili we could judge better
Inakuaga burst ya vinyongo mtu alivyo navyo, kama leo hana unamsimanga, mara kidogo umenyang'anya bra uliyonunuaga kwenye birthday unadhani akipata atakuacha???
 
Hivi mwanamke akiwa anajitafutia hata vi buku buku huwa ni jambo linalomkera sana mwanaume? Wanaume huwa wanainjoi kuona mtu unakua omba omba kwake mara akunyime....inaleta good feelings bila shaka 🤔

Pole kwa changamoto.
Tumesikia story ya upande mmoja. Hatujamsikiliza mume ana lipi la kusema. Usipende kutoa hukumu kwa kusikiliza maelezo ya mwanamke tu. Ksa uzoefu wangu kwenye hii migogori ya masuala ya malezi na ndoa mara nyingi story ya mwanaume ndio inakuaga ya kweli
 
Jamaa ameona mbali na anajua uhalisia wa akina nyie mnaofanya kazi. Mkishaanza kupata visenti mnabadilika, mnaota mapembe na kumdharau mwanaume. Binafsi jamaa hajakurupuka.
Na hao watoto skiwaacha kwa mama wataishia kuwa mashoga tu. Single mother hawezi kulea mtoto wa kiume kuwa mwanaume
 
wanawake mkijipata mna ujeuri sana wachache wanaojielewa nyie hata siyo wa kuwatetea
 
Sasa anasema watoto sio wake halafu kawachukua kawapeleka wapi?

Akamatwe mara moja asije kuwadhuru kwani ameshasema kuwa damu si yake
Lkn umesikiliaza upande mmoja, upande wa jamaa hujasikiliza.
 
A coin has two sides bro, kwa akili tu ya kawaida vitendo vya mwamba kweli si vya kiutu ila kwa mtu timamu hawezi fanya hayo matukio without the reasons behind, as long as mwanamke hajalitamka la changamoto ya akili basi halipo.. Kuna sababu zingine zinapelekea mwamba kua hivo, tungezijua tungetoa judgement sahihi
Duh. Mambo so mambo.
Kumbe inbidi tumsikilize na jamaa tena.
 
Wanawake Wakiendelea kuendekeza Ubinafsi na Umimi ndani ya Ndoa, Ndoa zitaendelea kuwashinda.
 
Salaam wana jamvi,

Nahitaji msaada wa kisheria ama taratibu gani nifuate ili kuweza kupata haki ya kulea watoto wangu!

Story kwa ufupi iko hivi:

Mimi na mwanamke (34) nimeolewa ndoa ya kanisani, nimebahatika kupata watoto wawili (mkubwa miaka 4.7, mdogo miaka 2.5). Mimi na Mr tumekuwa kwenye migogoro isiyoisha kwa muda mrefu (ndoa ina miaka 6), na chanzo hasa ni mwenzangu hataki nifanye kazi, wala biashara yoyote, wala shughuli yoyote inayoniingizia kipato. Kwa muda wote huo nimekuwa mtulivu na kumsikiliza anachotaka ili tu amani iwepo, lakini haikuwezekana. Majukumu yake anatimiza kwa kusuasua, yaani ni mpaka awe na furaha ndipo atoe. Mkipishana kidogo anakususia kila kitu mpaka kutoa matumizi.

Kuna wakati ukimuomba fedha kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani na watoto anakujibu vibaya, nanukuu: “Watoto sio wangu, watafutie baba yao” na “Sifanyi kazi kwa ajili ya matumbo yenu”. Hali hiyo na kauli hizo zimenifanya kuishi maisha ya kuogopa kumkwaza ili tu nipate mahitaji ya muhimu (chakula).

Ukimuomba mtaji wa biashara anadai nilee watoto bado wadogo.

Kutokana na changamoto hizo na maisha kuwa magumu, niliamua kutafuta kazi, maana nilifanikiwa kusomeshwa mpaka chuo kikuu, nina degree ya ………

Mwaka huu Mungu akajaalia nikapata kazi serikalini. Baada ya kumwambia nimepata kazi alichukia sana, ndipo akaamua kutorosha watoto. Sijui alipowapeleka na wala sijui wanaishi na nani. Ndugu zake hawanipi ushirikiano, wapo upande wa ndugu yao.

Mr amehama na nyumba na hapokei simu zangu kabisa. Ni miezi miwili imepita, lakini kuna maneno ya pembeni yalinifikia kwamba ili anipe watoto ni lazima niache kazi, vinginevyo sitawaona tena.

Hatua nilizofanikiwa kuchukua:
  1. Nilikwenda kutoa taarifa polisi kwenye dawati la jinsia.
  2. Nimejaribu kuongea na wakubwa zake ili angalau tukae kikao cha kusuluhisha kifamilia, lakini amekataa kuwekwa kikao mpaka siku nitakapokubali kuacha kazi.
Msaada ninaohitaji:
  • Nataka kujua process gani nifuate kisheria ili nipatiwe watoto wangu nilee mwenyewe, mpaka pale watakapofikia umri wa kuchukuliwa na baba yao.
  • Je, mgogoro huu hautaleta athari kwenye kazi yangu? Vipi kama ataenda kuniharibia ofisini ili niachishwe kazi?
  • Je, naweza kumueleza mkuu wangu wa kazi juu ya changamoto ninayopitia ili pia niweze kupata ruhusa wakati nitakapohitaji kufuatilia watoto?
Mimi kuacha kazi haiwezekani kutokana na mazingira niliyoishi, na pia mimi binafsi ninayo malengo yangu. Isitoshe nina wazazi wanaonitegemea.

Naombeni msaada tafadhali, siwezi kukaa kwa amani bila kujua mahali walipo watoto.

Ahsanteni.

1. Kuna sababu Kwa Nini ana hasira hivyo, hiyo wewe unajua, maana angepewa nafasi ya kujieleza tungeelewa, ila ndo mambo yenu wanawake.

2. Anaonekana anakupenda sana, ila ana chuki mno, na huo Upendo hauwezo ondoa chuki, achana na suluhu kabisa, atakuja kukudhuru huyo mtu.

3. Anzia Kanisan, asipoonekana sogea kwa Mtendaji, mpaka utafika kwa Mahakama, Mahakama probably itakurejeshea watoto wako kama unawaitaji, yeye kupambana na watoto ni kutaka tu kukuvuta.

4. Kamwe usije thubutu kuacha kazi, nyie hamuwezani, usitafute kuja kuwa mtumwa wake kabisa, katika mazingira hayo Mambo ni magumu.

Hitimisho:

Naona kama umenivutia vile kwa maelezo yako, na wewe sio mke wa mtu, so Sina Dhambi, what about nikifaham zaidi? Nasema wazi Kabisa mapaka Mshana Jr asikie.
 
Kuna mazingira siyo mara zote inakuwa hivyo.
Mathalani mke ni askari na kapangwa boda.
Hatujui kazi ya huyu mdada kama Yuko ktk majeshi au la na pia ustawi unapeleka hoja ya malezi na mazingira kama watoto wako boarding watawatoaje kwa haraka. Mume anaweza kuchukua watoto. Kukingana na uthibitisho wa hoja na mara nyingine kuna rushwa
Owky ila huyo kawaficha watoto. Tayari ni offence. Kaeni ongeeni mfikie muafaka. Utakuka watoto kawaficha kwa wazazi au dada zake. Hao ndugu zaidi ya fedha zake hakuna lingine wanachokitaka. Ukitaka kujua itokee afe halafu uone mateso watakayopewa hao watoto.
 
Na ukiomba waje wakusimange
Shida yenu mnafikiri kwamba wanaume tunawaza kama nyie. Movements za usawa wa kijinsia zimewapumbaza kwa kuwaambia mwanaume na mwanamke wapo sawa kwenye kila kitu, kitu ambacho sio ukweli. Tumetofautiana sana, kibaolojia na saikolojia.

Nyie mnavyomwangalia mwanaume asiekua na hela kama useless creature. Mnavyojiona mpo entitled kwenye hela na mali za mwanaume, sisi saikolojia yetu haipo hivyo. Sisi hatuna shida na mishahara wala hela zenu, sisi tunachotaka ni heshima, uaminifu na utiifu tu. Wewe hata ukia tajiri nchi nzima, mumeo hana shida na hela zako. Wewe maintain to hayo mambo matatu (heshima, uaminifu, utiifu) hakuna kitakachoaribika
 
Wanaume kama hauna uwezo na hautaki mwanamke anafanya kazi/biashara, usioe mtoto wa masikini, mwanamke atavumilia vingi ila sio kuona wazazi wake wanapigika hela ya mahitaji muhimu.
Atajikaza na kubana kahela unakompa kasipotosha lazima mtiti uanze. Hasira na stress za kuona familia inataabika na yeye wala ww hamna msaada lazima irudi ndani kwenu.
 
Mleta mada najua ni ngumu ila fuata ushauri wa walokuambia tulia usitafute hao watoto! Kwa tabia ulizozieleza hapo za kususa kutoa hela ya matumizi (uchoyo, ubinafsi) hatoboi hata miezi sita na hao viumbe atakurudishia tu.
 
Shida yenu mnafikiri kwamba wanaume tunawaza kama nyie. Movements za usawa wa kijinsia zimewapumbaza kwa kuwaambia mwanaume na mwanamke wapo sawa kwenye kila kitu, kitu ambacho sio ukweli. Tumetofautiana sana, kibaolojia na saikolojia.

Nyie mnavyomwangalia mwanaume asiekua na hela kama useless creature. Mnavyojiona mpo entitled kwenye hela na mali za mwanaume, sisi saikolojia yetu haipo hivyo. Sisi hatuna shida na mishahara wala hela zenu, sisi tunachotaka ni heshima, uaminifu na utiifu tu. Wewe hata ukia tajiri nchi nzima, mumeo hana shida na hela zako. Wewe maintain to hayo mambo matatu (heshima, uaminifu, utiifu) hakuna kitakachoaribika
Nimekuelewa mkuu, asante sana 🙏
 
Halimkeri alichoniangusha mwanaume mwenzangu ni hataki mkewe afanye kazi huku kutoa matumizi na kumpendezesha mkewe hataki.

Kama hutaki mkeo aajiriwe na ana passion ya biashara mpe mtaji afanye biashara huyu jamaa ni mpumbavu sana
Wewe ndio mpumbavu, ni mmoja wa masimp mliyokua brainwashed na movements za usawa wa kijinsia kwa kukalilishwa kwamba mwanamke ni innocent creature na popote kwenye mgogoro wa mwanaume na mwanamke basi mwanaume ni villain na mwanamke ni victim.

Mwanaume anaejielewa hawezi kutoa hukumu ya mgogoro kwa kusikiliza maelezo ya upande mmoja, especially maelezo ya mwanamke pekee ambao wanajulikana kabisa silaha yao ni ku-play victim
 
Juvenile court wanahusika na issue ya custody ya watoto. Kila wilaya huwa zina mahakama za watoto unatakiwa kupeleka maombi ya kuomba uishi na hao watoto. Kwenye maombi yako unatakiwa kuthibitisha kuwa watoto wakiishi kwako wataishi vizuri kuliko kwa baba yao. Mahakama inazingatia maslahi ya watoto kabla ya kuamua waishi na nani. Watafute mawakili watakusaidia kuandaa maombi.
 
Back
Top Bottom